faithosaso
New Member
- May 8, 2015
- 3
- 1
nimekuwa nafuatilia threads zinazohusu kilimo na kuvutiwa na jinsi mnavyochangia-mfano Elnino na Malila na members wengine. naomba kuuliza kama nitaamua kulima MITIKI (teak wood). Sasa naomba mwenye utaalamu anisaidie kunielewesha yafuatayo:
nitashukuru sana kwa mwenye kufahamu kunipa maelezo!
- Je unapotaka kupanda mitiki je mbegu zinauzwa wapi?
- Je mbegu unazipanda kwenye vimfuko vidogovidogo na udongo wake (i.e kitalu). je mche unapotolewa kwenye kitalu unaupanda moja kwa moja shambani au kuna process nyingine?- i.e. yaani namaanisha hatua (steps) za kutoa kwenye kitalu kwenda shambani
- Je unatakiwa kuweka umbali gani kati ya mtiki/mche mmoja na mwingine kama unataka ikue kwa ajili ya mbao.. na je spacing ni kiasi gani kama unataka ikue na uvune kama milingoti
- Je kwenye ekari moja unaweza kupanda miche mingapi?
- Je KIWASTANI inachukua miaka mingapi mpaka uvune kupata mbao na pili kupata milingoti
- Je kuna paper au website ninayoweza kupata maelezo zaidi?
Nataka kujua juu ya aina ya udongo mzuri ambao unastawisha mitiki