Kilimo cha Mitiki: Utaalamu na biashara yenyewe

Kilimo cha Mitiki: Utaalamu na biashara yenyewe

nimekuwa nafuatilia threads zinazohusu kilimo na kuvutiwa na jinsi mnavyochangia-mfano Elnino na Malila na members wengine. naomba kuuliza kama nitaamua kulima MITIKI (teak wood). Sasa naomba mwenye utaalamu anisaidie kunielewesha yafuatayo:

  1. Je unapotaka kupanda mitiki je mbegu zinauzwa wapi?
  2. Je mbegu unazipanda kwenye vimfuko vidogovidogo na udongo wake (i.e kitalu). je mche unapotolewa kwenye kitalu unaupanda moja kwa moja shambani au kuna process nyingine?- i.e. yaani namaanisha hatua (steps) za kutoa kwenye kitalu kwenda shambani
  3. Je unatakiwa kuweka umbali gani kati ya mtiki/mche mmoja na mwingine kama unataka ikue kwa ajili ya mbao.. na je spacing ni kiasi gani kama unataka ikue na uvune kama milingoti
  4. Je kwenye ekari moja unaweza kupanda miche mingapi?
  5. Je KIWASTANI inachukua miaka mingapi mpaka uvune kupata mbao na pili kupata milingoti
  6. Je kuna paper au website ninayoweza kupata maelezo zaidi?
nitashukuru sana kwa mwenye kufahamu kunipa maelezo!

Nataka kujua juu ya aina ya udongo mzuri ambao unastawisha mitiki
 
Hongera sana mkuu.kwa ushauri kdgo mana hata mm niko tanga,wilaya ya korogwe.kuhusu mitiki ningekushauri kama hill shamba lako lipo kwenye bonde kdgo na udongo mweusi,lkn kama ukiweza kupanda mikaratusi utakula hela nzuri mapema zaidi ya mitiki na maeneo mengi ya huku kwetu ya stawi vzuri.mi nashukuru nimeanza kupanda mwaka huu tena kipindi hichi cha mvua na pia nakushauri upate miche ya mda mfupi(miche ya kikonyo)
mikaratus inavumwa baada ya muda gani?
 
Mkuu hili tulishajadili sana humu. Jitume kutafta habari sio kila kitu utafuniwe!
Mitiki nayochukulia mkopo ni mingi kiasi cha ekari tano na mikopo hutolewa kuanzia miti ya miaka mitatu na hata ukiwa na ekari moja utapewa mkopo kulingana na ushawishi wa biashara utakayofanya na wepesi wa kurejesha mkopo.

daah! umemshushua jamaa hadi naogopa kuuliza swali.
 
Naomba msaada kwa mwenye kujua utaalamu wa upandaji miti aina ya mitiki na jinsi ya kuifanya ikue haraka haraka.

Tafadhali naomba anielekeza kuna project naifanya.
 
Acha hatua tano kila baada ya shimo unapopanda, matawi yake ni lazima kuyakata kila yanapoota ili mti ukue kuelekea juu kwa haraka na vile vile kunyooka, usiache tawi hata moja zaidi kuchwa cha mti(sina jina lingine la kuita)
 
miti.jpg

Utangulizi
Mbegu za mitiki zinapatikana Tanzania Tree Seed Agency wako Msamvu Morogoro.Kilo moja ya mbegu za mitiki inatosha kuotesha kwenye shamba la hekta moja, ambayo ni wastani wa miti 1000 mpaka 1500 kama itaoteshwa na kutunzwa vizuri

Matayarisho:
  1. Loweka mbegu kwa muda wa siku 3 mpaka 7 ukiwa unabdili maji kila baada ya masaa 12. Hii ni kwasababu ganda la nje la mbengu ya mtiki ni gumu sana na lina sumu mbaya.
  2. Baada ya masaa 72 anika mbegu zako juani kwa masaa 12.
  3. Tengeneza kitalu, weka mbolea ya wanyama au mboji, kisha panda mbegu zako kwenye kitalu.
  4. Mwangilia maji kila siku asubuhi na jioni, mbegu zitaanza kuota baada ya siku 10 hadi 20.
  5. Miche ikifikia urefu wa futi moja, unaweza sasa kuiotesha kwenye shamba lako ulilotayarisha kwa ajili ya kuotesha miti.
  6. Kabla ya kung’'oa miche hakikisha unamwaga maji mengi, ili mizizi isikatike sana, kisha chukua kisu chenye makali ya kutosha na kata ncha ya juu ya mti na ondoa majani, hii inasaidia mti kuchipuka upya hasa eneo ambalo halina maji mengi.
  7. Otesha miti futi 6x6 mitiki inaposongamana, hurefuka haraka ikikimbilia jua angani, hivyo kwa vipimo hivyo miti yako itakuwa mirefu sana na iliyonyooka, baadaye unaweza kuipunguza na kuuza fito za kujengea.
  8. Ili upate mbao bora hakikisha unaondoa matawi yanayochipuka pembeni hadi mti ufike zaidi ya futi 10 kwani ndiyo yanafanya mbao kuwa na mabaka (vidonda)
Bei ya Kilogram Moja (Kg 1) ya mbegu za Mitiki ni TZS 12,500

Tanzania Tree Seed Agency wapo Dodoma Rd, mkoa wa Morogoro kama unaenda Kihonda. Kituo kinaitwa "Misitu" au "Vybes"
 
Kaka Mack vipi baada ya mda gani nitaweza vuna iyo miti ya mitiki? Na je majani yake mbuzi wanakulaaana maeneo nayifikiria panda yana mifugo mingi sana
 
Hivi wanayosema miti inayovunwa baada ya miaka 50 ni miti gani wanasema ina fedha nyingi sana.
 
Hivi wanayosema miti inayovunwa baada ya miaka 50 ni miti gani wanasema ina fedha nyingi sana.

Miaka 50 ni mingi sana, miti ipo aina nyingi na kwa ajili ya matumizi mbalimbali km mbao, nguzo, mkaa, kutengenezea mapambo n.k. Mara nyingi miti kwa ajili ya nguzo ndio huwa na bei sana.
 
Mitiki inastawi vizuri katika udongo wa asili ipi, na hali ipi ya hewa?
 
Mitiki inastawi vizuri katika udongo wa asili ipi, na hali ipi ya hewa?
Hali ya hewa ya mikoa ya pwani, pia uzuri wake hustawi ktk aina nyingi za udongo hata km ni kichanga.
 
Back
Top Bottom