Kilimo cha Mitiki: Utaalamu na biashara yenyewe

Kilimo cha Mitiki: Utaalamu na biashara yenyewe

Salaam wadau.Naomba kupata maelekezo kuhusu mikoa ya Tanzania ifaayo kwa Kilimo cha miti jamii ya mitiki.Je mkoa wa kagera hususan Wilaya ya Misenyi inawezekana kwa Kilimo hiki? MTU mwenye ekari moja ya Ardhi anaweza kuanzisha mradi huu?
 
Unaweza kuvuna kuanzia miaka saba (7) na kuendelea, pia sidhani km majani yake yanaweza kulika na mifugo.

Mkuu inachukua mda gani toka kusia mbegu kwenye kitalu hadi kuing'oa inapofikisha hiyo futi 1 kwa ajili ya kupanda shambani.
 
Mimi nitakupa bei kwa kilo. Kg moja ya mtiki ni Tsh 6000/,sijui kama watakuwa wame-update,ila inatoa miche kati ya 1000 mpaka 1500. Miche ya mitiki inasumbua sana uotaji wake,unaweza ukawatika kilo nzima ukapata miche mia. Sasa inabidi ufuate maelekezo ya kitalaam sana.

Siwezi kukuhakikishia kama utapata au utakosa,ila pines/mlingoti nina hakika hakuna kabisa. Pine iliyopo ni ile ya kutoka Zimbabwe ambayo huuzwa Tsh 500,000/ kwa kilo kwa sababu huvunwa baada ya miaka nane.

Ukishindwa Morogoro,jaribu Lushoto na Kilombero. Kule kilombero ni private firm unaweza kupata kiasi hicho bila taabu.

Nimekupa yale ninayofahamu,akiwepo mwenye taarifa zaidi atupe.

Malila, heshima kwako, waweza nisaidia contact details za hawa watu wenye mbegu au miche ya pines toka zimbwabwe. Nitashukuru sana kwa msaada wako kiongozi
 
Mkuu kisima habari yako, je hapo moro uko maeneo gani na vip bado unazo miche ya mitiki? kama unayo unauzaje kwa mche?
Salama mkuu!
Moro naishi Turiani karibu kabisa na mtibwa teak forest.
Mbegu zipo zakutosha kulingana na shehena ya uhitaji wako.
Bei yangu inavary kulingana na wingi wa miche(stamps) utakazo.
Mathalani kama order yako itafikia miche 3200(ambayo unaweza panda ekari5) ntakuuzia kwa sh250 kila mche na kutakuwa na offer ya miche 300 bure!
Ikiwa order yako ni zaidi ya miche 16000 bei itapungua hadi 200@mche na kutakuwa na nyongeza ya miche 1000.
Utaratibu ni unalipia 50% ya mzigo na 50% nyingine utamalizia on delivery day.
Kama utahitaji huduma ya kupandiwa kitaalam, mimi na team yangu tupo tayari kukuhudumia popote lilipo shamba.
Karibu sana mkuu!
 
Sehemu nyingi inastawi.......ila zaidi kwenye mvua za kutosha, joto la wastani na udongo wenye kina kirefu. Mashamba makubwa ya Teak yapo Tanga (Longuza), Morogoro (Turiani, Ifakara etc). Kazi kwako.....ukipata kijitabu cha mbegu cha Tanzania Tree Seed Agency kimeorodhesha maeneo kwa ufasaha zaidi.
Napata wapi hiki kijitabu mkuu??
 
Kitabu hicho kimeonyesha zone ambapo miti hiyo hulimwa.
Kwa hiyo hakitokusaidia kitu, cha muhimu Pima udongo wako kabla ya kupanda. Nakupa mfano kuna jamaa Mbezi ya Kimara anamepanda mitiki na imekubali Sana.
Ukirudi ktk kitabu hakuna sehemu ilioonyesha Kimara
 
Mkuu salam. Umeongea kitu cha maana sana. Naomba unisaidie procedure za kupima udongo na kujua kama ninachotaka kupanda kinafaa kwenye huo udongo. Na jinsi ya kuchukua udongo na kwa hapa Dar maabara inayofaa iko wapi. Utakuwa umenisaidia sana kiongozi.
 
Nakushauli gawanya Mara Saba Namaanisha chukua mchanga sehemu Saba. Kila sehemu chukua kilo Moja, kwatua kwa jembe. Peleka Sua.
Mimi Sua kila kifuko walinichaji laki Moja full ushauli.
 
Nakushauli gawanya Mara Saba Namaanisha chukua mchanga sehemu Saba. Kila sehemu chukua kilo Moja, kwatua kwa jembe. Peleka Sua.
Mimi Sua kila kifuko walinichaji laki Moja full ushauli.
Ubarikiwe mkuu
 
Nakutahadhali Kama unataka kupanda mitiki. Usipende kununua miche bora uweke kitaluchako ambacho utaiandaa mwenyewe tangu udogo, mtiki no vyema kupewa chanjo zote ikiwa ktk kitalu.
Ikifikia kupelekwa Shambani itastahimili shida zote
 
Nunua mbegu zako nitakuambia jinsi ya kufanya ziote na ni rahisi.
Je utaniruhusu kutoa somo japokuwa si mtaalam kwa faida ya wengine
 
Nakutahadhali Kama unataka kupanda mitiki. Usipende kununua miche bora uweke kitaluchako ambacho utaiandaa mwenyewe tangu udogo, mtiki no vyema kupewa chanjo zote ikiwa ktk kitalu.
Ikifikia kupelekwa Shambani itastahimili shida zote
Tatizo ni kuwa mbegu za TTSA hazieleweki. Hazioti vizuri kama vijitabu vyao vinavyosema. Nahitaji mwakani kupata mbegu za teak za kutoka nje kama Zimbabwe au South Africa. Kama una connection nao utanisaidia
 
Back
Top Bottom