Kilimo cha miwa Kilosa

Kilimo cha miwa Kilosa

SHIGOTTO

Senior Member
Joined
Sep 4, 2018
Posts
156
Reaction score
282
Ndugu zangu, poleni na majukumu ya kikazi, nimepatwa na wazo la kulima miwa pale Kilosa kwa ajili ya kuuzia kiwanda cha Mkulazi kwa ajili ya kutengeneza sukari.

Nimepata shamba la heka sitini ambalo nina mpango wa kulinunua, nakuja kwenu kujua kama kuna mtu aliyewahi kulima au kusikia juu ya changamoto ya kilimo hiki?

Naaminishwa kuwa kiwanda kitaanza kazi ndani ya mwaka huu kama kuna ushauri naukaribisha!
 
Shamba unataka nunua kata gani na kijiji gani?

Ukifanikiwa lima hilo shamba lote basi jua umeshatoka kimaisha.

Ni kweli kiwanda kitaanza kazi week chache zijazo, kutokana na ukubwa wa kiwanda malighafi haitowahi kujitosheleza.

Usijiulize mara mbili, nunua shamba sasa kabla kiwanda hakijawashwa. Kiwanda kikishawashwa bei ya mashamba itapanda sana.

Kama una swali lolote karibu.
 
Shamba unataka nunua kata gani na kijiji gani?

Ukifanikiwa lima hilo shamba lote basi jua umeshatoka kimaisha.

Ni kweli kiwanda kitaanza kazi week chache zijazo, kutokana na ukubwa wa kiwanda malighafi haitowai kujitosheleza.

Usijiulize mara mbili, nunua shamba sasa kabla kiwanda hakijawashwa. Kiwanda kikishawashwa bei ya mashamba itapanda sana.

Kama una swali lolote karibu.
Shamba nanunua kijiji cha Msowelo unaingilia Dumila then unaenda kilometa kadhaa unaingia mkono wa kushoto kabla hujavuka daraja kuna njia mpya imechongwa kuelekea mashambani, ni hivyo tuu ndugu yangu!
 
shamba nanunua kijiji cha msowelo unaingilia Dumila then unaenda kilometa kadhaa unaingia mkono wa kushoto kabla hujavuka daraja kuna njia mpya imechongwa kuelekea mashambani, ni hivyo tuu ndugu yangu!
Kila la heri.
 
Utapigwa aisee
 
Hao wapuuzi wamesababisha vifo vya Baba zetu kwa pressure tokana na madeni na kutokuweka miundombinu ya umwagiliaji kwa wakati hivyo Miwa kufa kwa kukosa maji huku kiwanda kikiwa bado kufanya kazi na wakiwa wanadaiwa na Azania bank kwa pesa walizowakopesha pitia AMCOS ile ya kizushi ya akina God, Zungu na yule Mstaafu wa TARI Dakawa.

Wazee walishtaki sana kwa viongozi wa kitaifa akiwemo PM ila hakuna kilichofanyika. Kiwanda na project hiyo inapigwa vita na viwanda vya Mtibwa Sugar na Kagera Sugar kwani Industry ya Sukari imehodhiwa na kale kajamaa kaarabu koko ka Mtibwa na Kagera Sugar. R.IP wazee wetu akina Mzee Mbuji, Mzee Makonyora, Mzee Nderingo, Mzee Msoma, Mzee Mtimkavu n.k hadi leo wanenu tunadaiwa na Azania Banki, hakuna maji kwenye mashamba, Miwa mingi imekufa na miwa tunauza kwa hasara pale Mtibwa Sugar.
 
Back
Top Bottom