Kilimo cha mpunga Morogoro/Kimara-Mbeya

Kilimo cha mpunga Morogoro/Kimara-Mbeya

Okay nashukuru snaa sasa Mkuu nilihitaji October nitokee maeneo hayo now nipo makete nilihitaji nipate walau uelewa kidogo hata wilaya kijiji yaani eneo husika wanalo Lima mpunga.... Najua unaweza ukawa na experience ya maeneo hayo Kaka 🙏
 
Habari ya mapambano kijana mwenzangu!
Kulingana na hoja yako, ninapenda kuchangia baadhi ya mambo niyajuayo juu ya kilimo hiki cha mpunga. Mimi ni mkulima wa zao hili ktk mkoa wa Songwe wilaya ya Momba bonde la Kamsamba.
SIFA ZA BONDE HILI
~Ardhi yenye rutuba
~Uhakika wa maji
~Mavuno mengi
~Mpunga unaotoa mchele mzuri na wenye soko kubwa, ni mchele namba 1 kwa soko la mikoa ya nyanda za juu kusini.
~Gharama za wastani ktk uendeshaji
~Matumizi ya mbolea si ya lazima
~Miundombinu ya barabara iko vizuri
~Rasilimali watu inapatikana
~Shamba la 200000 unaweza panda na kuvuna mara2 kwa msimu

GHARAMA/EKA1
✓Kukodi shamba 100000-200000
✓Kukatua/kulima(ng'ombe) 40000
✓Kusawazisha/kuvuruga 40000
✓Mbegu plastik mbili 20000 kwa tahadhari ila plastik moja inatosha
✓Kitalu cha mbegu 10000
✓Kung'oa mbegu 25000
✓Kupanda 70000-100000
✓Kung'olea/palizi 25000-40000
✓Kufyeka 50000
✓Kusomba 25000
✓Kupiga 50000
Hizi ndizo hatua muhimu za kuzingatiwa ktk kilimo cha mpunga.

RATIBA YA MSIMU
>Kusafisha shamba Disemba mwanzoni
>Kuandaa kitalu na kuotesha mbegu Disemba mwanzoni.
>Kulima Disemba mwishoni, januari au februari mwanzoni.
>Kuvuruga na kupanda wiki moja au zaidi baada ya kulima
>Palizi/kung'olea wiki 3 na kuendelea baada ya kupanda.
>Kuvuna mwezi April hadi Mei.

Kama kuna swali au mchango wowote wa ziada unakaribishwa.
Ekari moja unapata gunia ngapi za mpunga? Na ukikoboa unapata gunia ngapi? Ukiuza unapata bei gani kwa gunia?

Nilikuwa napasikia kamsamba. Ndo nasema nikajaribu
 
Ekari moja unapata gunia ngapi za mpunga? Na ukikoboa unapata gunia ngapi? Ukiuza unapata bei gani kwa gunia?

Nilikuwa napasikia kamsamba. Ndo nasema nikajaribu
Wazo la kuja kamsamba bado lipo?
 
Okay nashukuru snaa sasa Mkuu nilihitaji October nitokee maeneo hayo now nipo makete nilihitaji nipate walau uelewa kidogo hata wilaya kijiji yaani eneo husika wanalo Lima mpunga.... Najua unaweza ukawa na experience ya maeneo hayo Kaka [emoji120]
Ili ufikie malengo ya ndoto zako, kalime kwenye umwagiliaji.
Nina miaka mingi kwenye kilimo hiki.

Ninalima zaidi ya ekari 100 kwa mwaka, lakini mapato ninayopata kwa kutegemea mvua no kidogo kulinganisha na umwagiliaji.

Acha kupanda mbegu za asili,tumia mbegu za kisasa kwa mavuno mengi,Jenga mazoea ya kununua mbegu kwenye taasisi zinazozalisha mbegu

DAKAWA MOROGORO EKARI1:

Kukodi350000
Kulima40000
Kuvuruga70000
Kupandikiza80000
Mbolea 2bags sh100000
Palizi2 140000
Kuvuna kwa machine 100000

MAVUNO
Juu 40bags
Kati 30
Chini 25

Sasa angalia gharama na mapato ukilima kwenye umwagiliaji na kwenye mvua.
 
Haya wakulima wenzangu.
Karibuni DENE ENTERPRISES CO. LTD kwa mahitaji yote ya bidhaa bora za nafaka kama mchele, mpunga, mahindi, maharage. Pia tunaagiza vifaa vyote vya kilimo. Tuagize nasi tutakufikishia kwa uaminifu kabisa kwa bei nafuu.
Badili mfumo wako wa kilimo. Lima kisasa uongeze tija kwenye mazao ili upate faida. Jipatie vifaa vya kisasa vya kilimo sasa kutoka DENE ENTERPRISES Co. Ltd
Tufollow katika ukurasa wetu @deneenterprises
 
Hebu ni SMS kwa namba hii 0693389482 nataka nine Lima kamsamba maana McHale wake ni mzuri saana. Nataka niwekeze hapo mkuu
Saiz ndio tupo kwenye mavuno, labda kwa mwakani
 
Hebu ni SMS kwa namba hii 0693389482 nataka nine Lima kamsamba maana McHale wake ni mzuri saana. Nataka niwekeze hapo mkuu
Umakini unahitajika sana kulimia Kamsamba ni kweli mpunga wake ni mzuri lakini kuna changamoto kubwa sana ya ukame mahala pale
 
Ili ufikie malengo ya ndoto zako, kalime kwenye umwagiliaji.
Nina miaka mingi kwenye kilimo hiki.

Ninalima zaidi ya ekari 100 kwa mwaka, lakini mapato ninayopata kwa kutegemea mvua no kidogo kulinganisha na umwagiliaji.

Acha kupanda mbegu za asili,tumia mbegu za kisasa kwa mavuno mengi,Jenga mazoea ya kununua mbegu kwenye taasisi zinazozalisha mbegu

DAKAWA MOROGORO EKARI1:

Kukodi350000
Kulima40000
Kuvuruga70000
Kupandikiza80000
Mbolea 2bags sh100000
Palizi2 140000
Kuvuna kwa machine 100000

MAVUNO
Juu 40bags
Kati 30
Chini 25

Sasa angalia gharama na mapato ukilima kwenye umwagiliaji na kwenye mvua.
Naomba kufahamu scheme za umwagiliaji kilimo cha mpunga nchini.
Na namna ya kukodi shamba.

#MaendeleoHayanaChama
 
Back
Top Bottom