Hapana huwa silimi bali nafanya biashara ya kununua mchele, lakini mbuga karibu zote nazifahamu.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hapana huwa silimi bali nafanya biashara ya kununua mchele, lakini mbuga karibu zote nazifahamu.
Kilimo hiko gharama sana, jitahidi ukijiingiza huko uwe makin sana
Ukiwa umekoborewa gunia moja la hizo plastic saba unatoa plastiki ngapi za kukoborewa?Shamba ukilipa huduma nzuri ni zaidi ya gunia 15 za plastiki 7
Ekari moja unapata gunia ngapi za mpunga? Na ukikoboa unapata gunia ngapi? Ukiuza unapata bei gani kwa gunia?Habari ya mapambano kijana mwenzangu!
Kulingana na hoja yako, ninapenda kuchangia baadhi ya mambo niyajuayo juu ya kilimo hiki cha mpunga. Mimi ni mkulima wa zao hili ktk mkoa wa Songwe wilaya ya Momba bonde la Kamsamba.
SIFA ZA BONDE HILI
~Ardhi yenye rutuba
~Uhakika wa maji
~Mavuno mengi
~Mpunga unaotoa mchele mzuri na wenye soko kubwa, ni mchele namba 1 kwa soko la mikoa ya nyanda za juu kusini.
~Gharama za wastani ktk uendeshaji
~Matumizi ya mbolea si ya lazima
~Miundombinu ya barabara iko vizuri
~Rasilimali watu inapatikana
~Shamba la 200000 unaweza panda na kuvuna mara2 kwa msimu
GHARAMA/EKA1
✓Kukodi shamba 100000-200000
✓Kukatua/kulima(ng'ombe) 40000
✓Kusawazisha/kuvuruga 40000
✓Mbegu plastik mbili 20000 kwa tahadhari ila plastik moja inatosha
✓Kitalu cha mbegu 10000
✓Kung'oa mbegu 25000
✓Kupanda 70000-100000
✓Kung'olea/palizi 25000-40000
✓Kufyeka 50000
✓Kusomba 25000
✓Kupiga 50000
Hizi ndizo hatua muhimu za kuzingatiwa ktk kilimo cha mpunga.
RATIBA YA MSIMU
>Kusafisha shamba Disemba mwanzoni
>Kuandaa kitalu na kuotesha mbegu Disemba mwanzoni.
>Kulima Disemba mwishoni, januari au februari mwanzoni.
>Kuvuruga na kupanda wiki moja au zaidi baada ya kulima
>Palizi/kung'olea wiki 3 na kuendelea baada ya kupanda.
>Kuvuna mwezi April hadi Mei.
Kama kuna swali au mchango wowote wa ziada unakaribishwa.
Huu uzi ni mtamu ila umetekelezwa.Ekari moja unapata gunia ngapi za mpunga? Na ukikoboa unapata gunia ngapi? Ukiuza unapata bei gani kwa gunia?
Nilikuwa napasikia kamsamba. Ndo nasema nikajaribu
Wazo la kuja kamsamba bado lipo?Ekari moja unapata gunia ngapi za mpunga? Na ukikoboa unapata gunia ngapi? Ukiuza unapata bei gani kwa gunia?
Nilikuwa napasikia kamsamba. Ndo nasema nikajaribu
Ili ufikie malengo ya ndoto zako, kalime kwenye umwagiliaji.Okay nashukuru snaa sasa Mkuu nilihitaji October nitokee maeneo hayo now nipo makete nilihitaji nipate walau uelewa kidogo hata wilaya kijiji yaani eneo husika wanalo Lima mpunga.... Najua unaweza ukawa na experience ya maeneo hayo Kaka [emoji120]
Nafuu umemwambia ukweli mashamba ya katavi bei juu na mpunga wake soko liko chini sanaKatavi huwezi pata shamba la kukodi kwa laki moja, sasa ni kuanzia 200, 000 hadi 250,000 kutegemea na mbuga
Wewe uko kamsamba mkuu?Wazo la kuja kamsamba bado lipo?
Naishi mbalizi ila nalimia kamsambaWewe uko kamsamba mkuu?
Hebu ni SMS kwa namba hii 0693389482 nataka nine Lima kamsamba maana McHale wake ni mzuri saana. Nataka niwekeze hapo mkuuNaishi mbalizi ila nalimia kamsamba
Saiz ndio tupo kwenye mavuno, labda kwa mwakaniHebu ni SMS kwa namba hii 0693389482 nataka nine Lima kamsamba maana McHale wake ni mzuri saana. Nataka niwekeze hapo mkuu
Umakini unahitajika sana kulimia Kamsamba ni kweli mpunga wake ni mzuri lakini kuna changamoto kubwa sana ya ukame mahala paleHebu ni SMS kwa namba hii 0693389482 nataka nine Lima kamsamba maana McHale wake ni mzuri saana. Nataka niwekeze hapo mkuu
Naomba kufahamu scheme za umwagiliaji kilimo cha mpunga nchini.Ili ufikie malengo ya ndoto zako, kalime kwenye umwagiliaji.
Nina miaka mingi kwenye kilimo hiki.
Ninalima zaidi ya ekari 100 kwa mwaka, lakini mapato ninayopata kwa kutegemea mvua no kidogo kulinganisha na umwagiliaji.
Acha kupanda mbegu za asili,tumia mbegu za kisasa kwa mavuno mengi,Jenga mazoea ya kununua mbegu kwenye taasisi zinazozalisha mbegu
DAKAWA MOROGORO EKARI1:
Kukodi350000
Kulima40000
Kuvuruga70000
Kupandikiza80000
Mbolea 2bags sh100000
Palizi2 140000
Kuvuna kwa machine 100000
MAVUNO
Juu 40bags
Kati 30
Chini 25
Sasa angalia gharama na mapato ukilima kwenye umwagiliaji na kwenye mvua.