SoC01 Kilimo cha mtaji wa Tsh bilioni 25 ndicho kilimo kitakachokuwa uti wa mgongo wa Tanzania

SoC01 Kilimo cha mtaji wa Tsh bilioni 25 ndicho kilimo kitakachokuwa uti wa mgongo wa Tanzania

Stories of Change - 2021 Competition

zambezi_21

Member
Joined
Jul 18, 2021
Posts
7
Reaction score
14
Ni kweli kwamba Dunia kwa Sasa ipo katika mapinduzi ya nne ya viwanda na sekta inayoongoza mapinduzi haya ni sekta ya teknologia na habari. Matajiri wakubwa wa Dunia kwa kiasi kikubwa ni Vijana na wazee ambao wamewekeza katika sekta hii kwa kiasi kikubwa,hapa nawazungumzia watu Kama Jeff Bezos,elon musk,mark zuckerberg,bill gates na wengine ambao ndio kwa sehemu kubwa wanamiliki utajiri wa Dunia.

Nchi nyingi za Africa Zina mchango mdogo Sana katika mapinduzi ya viwanda yanayotokea kwasasa tofauti na hapo wajasiria mali wengi waafrika imekua ni vigumu kwao kwa kupitia sekta ya teknologia na habari kutengeneza uchumi unao endana na Hawa matajiri wanao endesha uchumi wa Dunia kutokana na mifumo mibovu ya kiuchumi katika nchi za Africa lakini pia ugumu wa bidhaa zetu kuheshimika na kukubalika katika soko la Dunia.

Kwa namna moja au nyingine waafrika na watanzania hususani, inabidi kabla ya kushiriki kikamilifu katika sekta hii kiongozi ya teknologia na uchumi,tuanzie katika sekta ya kilimo Kama nchi tajiri zilipo anzia, kwa wakati huo huo tuchanganye kilimo na technologia na habari hapa ndipo tutajenga uchumi wa kweli.

Kilimo kinachoendelea hapa tanzania kwa asilimia kubwa sicho ambacho kinauwezo wa kuinua uchumi wetu na kujilinganisha na walioendelea. Tanzania tuna aridhi ambayo inafaa kilimo hekta million 13.5, zipo nchi ambazo ukubwa tuu wa nchi haufiki hecta million 13 lakini wanazalisha mazao ya kilimo Mara 2 zaidi yetu.

Uwekezaji mkubwa katika kilimo unaleta tija katika uchumi wa nchi kwani kilimo ni sekta ambayo inashabihiana mojakwamoja na ukuaji wa viwanda pamoja na mambo mengine. Katika nchi zilizoendela wakulima wanauwezo wa kuzalisha mazao pamoja na kuyaongezea thamani hapo hapo shambani mpaka kuwa bidhaa ambayo inaweza ikapelekwa moja kwa moja kwa mlaji.

Shambani la hekta 10000 linaweza kuzalisha chakula mpaka tani 110,000 Za nafaka kwa mwaka. Hili ndilo shamba la mkulima na mtanzania wakawaida anapashwa kudhamiria kuliendesha. Shamba hili pia kwa kutumia teknologia mbali mbali lina weza kuzalisha umeme wa mega watt 15 Kwa kutumia mtambo wa umeme ambao unatumia makuti ya mazao Kama mahindi,alizeti na mengine (biogas power plant au straw power plant). Kwa maana nyingine baada ya kulima mkulima atavuna kwa kutumia combine havester,ambapo kwa ukubwa huu wa hekta 10,000 combine havester aina ya (Claas Lexion 770 TT)Inaweza kuvuna shamba lote,mashine hii inavuna inapukuchua nakumwaga kwenye gari la nafaka. Baada ya hapo mkulima atatumia ( Claas Quadrant 3200 RC T) Kukusanya makuti yaliyoachwa chini. Makuti hayo baadhi yataenda kuingia kwenye mtambo wa kuzalisha umeme straw power plant au biogas power plant. Baada ya makuti haya kutumika kuzalisha umeme ule uji utakao bakia Kama taka za mwisho ni bidhaa adhimu Sana ambapo mkulima atatumia tena shambani Kama liquid fertilizer. Baadhi ya makuti yanataingizwa kwenye machine kuyakandamiza na kukausha maji halafu kutumika kutengenezea bidhaa mbali mbali Kama mbao (chip wood) au matofali (straw block)

Shambani pia mkulima ataweza kuweka viwanda mbali mbali kama kiwanda cha mafuta ya alizeti (vegetable oil distillation factory) Kiwanda cha gas (katika kutengeneza umeme wa biogas patazalishwa kwa wingi gesi ya methane ambayo utaweza kuzalisha umeme ama kuiandaa kwa ajili ya matumizi ya nyumbani) pia kiwanda cha unga (wheat and corn flour milling factory)

Shamba hili litahitaji matrekta makubwa ambayo ndiyo yanaongoza kwa ufanisi duniani. Hapa nazungumzia trakta Kama Case IH Quadtrac 620 walau moja,Case IH Quadtrac STX 375 pia moja,Case IH Maxxum 130 CVR moja na mengine pia machine za kuandalia na kupandia shamba Kama Gregoire Besson Semi Mounted Plough, Farmet Kompaktomat K1570, Bourgault 3420-100 Paralink Hoe Drill, Horsch Maestro 36 row na nyingine hizi zote ni za kuandaa shamba pamoja na kupanda

Pia shamba la ukubwa huu linahitaji Agricultural Drone Korec eeBe SQ,hii ni drone ya teknologia ya Hali ya juu Sana,kazi yake kwa kutumia kamera zake maalumu inaonesha uwiano wa maji baada ya kumwagilia,rutuba katika udongo,adhari za magonjwa na wadudu,kiwango cha mbolea kinachohitajika sehemu maalumu. Kwa kutumia GPS system technology taarifa hizi itazituma katika mashine zingine zote ili kujua sehemu fulani kipindi kingine panahitaji maji zaidi au mbolea zaidi au dawa zaidi. Na mwisho wa siku kwa kutumia data kutoka kila mashine Kama vile combine havester ambayo pia wakati inavuna inapima pia na wingi wa mavuno pamoja na ukubwa wa puche iliyovunwa kwenye GPS location flani kwahiyo unajua sehemu fulani ulipata mavuno machache au mengi kwa sababu gani. Hapa pia panahitajika Agricultural Drone DJI MG 1 walau ziwe kumi, hizi hutumika kwa ajili ya kupulizia dawa na kumwagilia liquid fertilizer, zinaruka umbali wa mita 3 kutoka kwenye mmea na moja inamwagilia upana wa mita 5, pilot mmoja anaweza kuziendesha 5 kwa pamoja. Hizi zinawasiliana na mashine zingine zote kujua wapi pakuwekwa kiasi gani cha mbolea au dawa japo pia mbolea hii unaweza pia kiimwagilia kwa kutumia irrigation system inayofungwa mwanzoni.

Shamba hili linahitaji miundo mbinu madhubuti shambani kwa maana ya barabara, silos za kuhifadhia nafaka ( grain silo plant) walau 3 za tani 5000, na 3 za tani 3000. Magari ya usafirishaji,magari ya moto (fire truck ya kuzima moto)mizani ya kupia nafaka,kituo cha kujazia mafuta,Majengo ya viwanda,Majengo kwa ajili ya kuhifadhia makuti( jengo la chuma lisilo na umeme ili kuepuka hatari ya moto) na jengo la karakana kwa ajili ya kutengeneza mbao,matofali na bidhaa zitokanazo na mbao. Pia Majengo ya makazi kwa ajili ya wafanya kazi,ofisi pia kanteen ya chakula.

Mradi wa shamba hili unahitaji walau mtaji wa billion 11 za kuanzia (initial investment)na kwa kipindi cha miaka walau mitano na kuendelea faida yake kubwa inapaswa irudi shambani ambapo kwa ukamilifu wake billion 25 zitatosha kuwa mtaji wa kuendesha shamba hili kwa uwezo wake kamilifu. Mtaji huu kwa kiasi kikubwa utategemea msamaha wa kodi katika kuingiza machine zote za kilimo nchini. Shamba hili linauwezo wa kuzalisha tani 110,000 za chakula kwa mwaka kwa ajili ya masoko ya ndani Kama azam,azania na milling factory zingine pia baadhi ya mazao kwa ajili ya masoko ya nje,hapa patalimwa mahindi,ngano,shairi,maharage,alizeti pamoja na viazi. Shamba hili linauwezo wakuzalisha tani 350,000 mpaka 400,000 za makuti ambazo zingiweza kupotea aridhi lakini hapa zitatengeneza umeme mpaka mega watt 15 au 45,000,000 Nm³ Methane gas. Kwa bajeti hiyo niliyoiweka ya kuanzia (initial investment) ya billion 11,hapa unaweza kuweka mtambo wa umeme wakuzalisha mega watt 1.5 kwa maana nyingine unaweza ukahudumia umeme kwa mkoa mzima kupitia shamba hili

Pamoja na faida zingine katika shamba hili, kwa kutumia mashine na matrekta makubwa yaliyopo shambani hapa itawasaidia wakulima wote wa pembembezoni mwa shamba wenye mashamba yenye ukubwa wa ekari 1000 na kuendelea kutumia mashine hizi wakati hazina kazi shambani,ambapo kwa muda mrefu wa kuendelea kufanya hivo wakalima Hawa watajijengea uwezo wa kuweza kuagiza mashine zao wenyewe kutoka nje za ukubwa huo. Pia umeme utakao zalishwa hapa unaweza kuelekezwa katika vijiji vya Jirani na mwingine kuwekwa katika grid ya taifa kwa makubaliano na tanesco. Pia kwa kutumia machine Kama seed dressing machine na zingine patazalishwa mbegu bora kabisa kwa ajili ya wakulima wa pembeni na kwa ajili ya biashara,pia mbolea inayotoka katika mtambo wa umeme na gesi unaweza kulitosha shamba Hili pamoja na wakulima wa pembembezoni na kwa ajili ya biashara pia.

Kiuhalisia unahitaji muda mrefu wa ujuzi katika kilimo kuweza kuendesha shamba la ukubwa huu. Hakuna linaloshindikana,kwa kupitia mashamba madogo ya hekari chini ya elfu moja watanzania wanaweza kudhamiria kujijenga kiujuzi na pia kwa kuwatembelea wenzetu na kutumia wataalamu wa ndani ikawezekana watanzania wakawaida kabisa kumiliki na kuendesha mashamba ya namna hii. Mtaji wa pesa nyingi namna hii unapatikana huko huko shambani. Wapo watanzania wengi waliowekeza katika mazao ya muda mrefu hapa nazungumzia machungwa,maembe,maparachichi mkonge na mengine tena wakiwa wameanza kwa kipato kidogo lakini leo hii wanatengeneza mabilioni ya shilingi. Bila kubadilisha mitazamo yetu katika kuiendea sekta hii ya kilimo na kuamua kudhamiria kufanya kilimo chenje kujenga uchumi wetu mkubwa wa taifa zima,wazungu wataendelea kutucheka na kutushangaa kwamba kwanini tumejifunga akili zetu na kushindwa kudhubutu kutumia aridhi yetu kujiendeleza na kuweza kushindana na mataifa makubwa kiuchumi. Binafsi nathubutu kusema kwamba aridhi tuliyonayo kwa ajili ya kilimo ni mali kubwa tuliyopewa na Mwenyezi Mungu kuliko madini,mafuta au gesi ambazo kila siku tunakimbizana nazo.

Screenshot_20210724_164838.jpg
 
Upvote 9
Watanzania wengi tunafanya subsistence farming, mimi nahisi uwe mkakati wa serikali kufanya large scale farming,yenyewe ndio ina capacity/resources za kufanya hivyo ..au la kuwe na system ya ku provide assistance kwa wale wote wenye ideas za kufanya large scale farming kwa mfano vijana wanaotoka vyuo vya kilimo wana mawazo kibao serikali ifanye ku-exploit utaalamu wao kunufaisha jamii at large. You have my vote mkuu nimeipenda thread
 
Apo kwenye agricultural drone za kupiga picha unaweza kutumia satellite ambazo zitakua zinapiga picha shamba lako kila siku. Picha hizi zitasaidia sana kuonyesha ni maeneo yapi ya shamba yana struggle na yapi yananenda vzuri. Taarifa za satellite zinaweza kuwa intergrated moja kwa moja kwenye drone za kupuliza dawa na mbolea na kuwezesha drone hizi kupuliza dawa au mbolea kwenye eneo linalohitaji na sio shamba lote.

Kampuni kama PLANET LABS (www.planet.com) inatoa huduma ya picha hizi ambapo kwa siku satellite zao zinaweza kupiga picha shamba lako atleast mara 2. Kwa kufanya utafiti wa picha hizi na taarifa zingine watakazokupa ikiwemo za hali ya hewa bas kilimo chako kitakua cha uhakika zaidi.
 
Mpigie kura , lol
 
Watanzania wengi tunafanya subsistence farming, mimi nahisi uwe mkakati wa serikali kufanya large scale farming,yenyewe ndio ina capacity/resources za kufanya hivyo ..au la kuwe na system ya ku provide assistance kwa wale wote wenye ideas za kufanya large scale farming kwa mfano vijana wanaotoka vyuo vya kilimo wana mawazo kibao serikali ifanye ku-harness utaalamu wao kunufaisha jamii at large. You have my vote mkuu nimeipenda thread
Serikali ilishashindwa commercial or large scale farming tangu kutaifishwa kwa mashamba ya Londral Brothers, Brook Bond ect. Walioweza kuwekeza katika commercial farming Tanzania baada ya kabla na baada ya Uhuru ni Karimjee Agriculture
 
Mimi hata sioni kwa nini serikali inataifisha mashamba mbona tuna ardhi kubwa tu
 
Watanzania wengi tunafanya subsistence farming, mimi nahisi uwe mkakati wa serikali kufanya large scale farming,yenyewe ndio ina capacity/resources za kufanya hivyo ..au la kuwe na system ya ku provide assistance kwa wale wote wenye ideas za kufanya large scale farming kwa mfano vijana wanaotoka vyuo vya kilimo wana mawazo kibao serikali ifanye ku-exploit utaalamu wao kunufaisha jamii at large. You have my vote mkuu nimeipenda thread
Shukrani kwa vote. Serikali inapart kubwa ya kufanya katika Hili lakini hata sisi Vijana tunayonafasi kubwa ya kuonesha nia na uwezo ili iwe rahisi serikali kuingilia na kutoa msaada
 
Apo kwenye agricultural drone za kupiga picha unaweza kutumia satellite ambazo zitakua zinapiga picha shamba lako kila siku. Picha hizi zitasaidia sana kuonyesha ni maeneo yapi ya shamba yana struggle na yapi yananenda vzuri. Taarifa za satellite zinaweza kuwa intergrated moja kwa moja kwenye drone za kupuliza dawa na mbolea na kuwezesha drone hizi kupuliza dawa au mbolea kwenye eneo linalohitaji na sio shamba lote.

Kampuni kama PLANET LABS (www.planet.com) inatoa huduma ya picha hizi ambapo kwa siku satellite zao zinaweza kupiga picha shamba lako atleast mara 2. Kwa kufanya utafiti wa picha hizi na taarifa zingine watakazokupa ikiwemo za hali ya hewa bas kilimo chako kitakua cha uhakika zaidi.
Yes hii ni nzuri pia Sana... Kilimo na hizi technology vinaenda sambamba
 
Azimio la Arusha la Mwalimu kwa Tanganyika lilikuwa kama kiwiko cha Mukoko kwa Utopolo FC...
 
tunaoneshaje nia na uwezo?
Vijana wengi wa Kitanzania hawana mwamko wa kufanya long-term investment,wengi wanapendelea kupata return ya pesa ya chap chap. Mradi Kama huu wa hecta 10000 za shamba kwa mtu mmoja ni mradi ambao unapata chance ya kuufanya au kuujariba Mara moja in ur life. Unahitaji maandalizi ya muda mrefu,nimezungumzia hapo kwamba mtaji unaweza kupatikana katika miradi ya kulima mazao ya muda mrefu Kama maparachichi au mkonge n.k

Now kwa mfano mtu anayelima mkonge uwekezaji wake mkubwa ni kupata shamba nakulisafisha na kupanda,baada ya hapo ni palizi tuu.. ni uwekezaji simple lakini itakubidi usubiri 3 years kupata return. Heka moja pekee unapata ml 2-3 per mvuno mmoja na unavuna twice per year. Ukiwa na heka 10 ni 40+ ml per year.

Huwezi kuanza na shamba kubwa la namna hii kabla hujaweza kurun shamba la hata heka 500. Mazao utakayolima itabidi ufanye research mbali mbali upate tofauti ya kilimo cha kisasa na kilimo traditional nakujua changamoto zote,hizi research sio za kusoma tuu nakusafiri kuobserve,inabidi uingie field ufanye,u will need at list 10+ years kujijenga kuweza kuwana uwezo.

dio Mana nimesema nikitu ambacho unapata chance ya kukifanya once in your life time kwa sababu kinahitaji muda mrefu... Lakini juu kwenye introduction nimemzungumzia mtu Kama Elon Musk ambaye yeye ameweza kufanya mambo ambayo nchi ndio zinashindana kufanya,yeye anafanya pekee yake tena nazaidi,anarusha marocket huko space na anandoto kujenga mji sayari nyingine,lakini tukumbuke huyu ni muafrika mwenzetu, kaondoka Afrika akiwa na miaka nafikiri 12,na yeye mwenyewe anasema hana hata degree ya eurospace engineering ni amejifunza na kuwekeza muda mwingi kujielimisha na nguvu ya kudhubutu.

So Vijana wa Kitanzania pia tunapaswa kuwa na hizi mindset ya kutaka kujenga mambo makubwa zaidi yetu na kuweka malengo ya muda mrefu,hapa serikali itatumia nguvu ndogo kumuwezesha mtu ambaye already anajua anapoenda na amedhamiri kufika kwa njia yoyote Ile.

Sorry gazeti limekuwa refu sana
 
Niongeze ideas matrekta makubwa bei ipo juu Sana si chini ya milioni 200 hapa unazungumzia angalau hp 150 hadi 400.
Cha kufanya nunua horse truck yaani kichwa cha truck mfano HOWO, MAN, BENZ, KAMAZ, nk unapata hadi HP 350,450,500 ukiagiza na ushuru kuanzia milioni 50,60,80 kutegemea na ubora hizi zinavuta majembe yenye tela au kifaa chochote cha shambani bila tatizo lolote.

Ukipata mavuno machache mswahili atakwambia umelogwa Shamba lilipeperushwa mazao atawahi kwa mganga kupigwa chale atapigwa ndumbaa heee na still matatizo yapo pale pale. Mswahili ni mtu duni Sana hawezi tatua matatizo kwa akili yake
 
Hekta elf 10 ni SAwa na kilometa ngapi?
Nikizipata hizi napanda michikichi na minazi zote
 
Vijana wengi wa Kitanzania hawana mwamko wa kufanya long-term investment,wengi wanapendelea kupata return ya pesa ya chap chap. Mradi Kama huu wa hecta 10000 za shamba kwa mtu mmoja ni mradi ambao unapata chance ya kuufanya au kuujariba Mara moja in ur life. Unahitaji maandalizi ya muda mrefu,nimezungumzia hapo kwamba mtaji unaweza kupatikana katika miradi ya kulima mazao ya muda mrefu Kama maparachichi au mkonge n.k

Now kwa mfano mtu anayelima mkonge uwekezaji wake mkubwa ni kupata shamba nakulisafisha na kupanda,baada ya hapo ni palizi tuu.. ni uwekezaji simple lakini itakubidi usubiri 3 years kupata return. Heka moja pekee unapata ml 2-3 per mvuno mmoja na unavuna twice per year. Ukiwa na heka 10 ni 40+ ml per year.

Huwezi kuanza na shamba kubwa la namna hii kabla hujaweza kurun shamba la hata heka 500. Mazao utakayolima itabidi ufanye research mbali mbali upate tofauti ya kilimo cha kisasa na kilimo traditional nakujua changamoto zote,hizi research sio za kusoma tuu nakusafiri kuobserve,inabidi uingie field ufanye,u will need at list 10+ years kujijenga kuweza kuwana uwezo.

dio Mana nimesema nikitu ambacho unapata chance ya kukifanya once in your life time kwa sababu kinahitaji muda mrefu... Lakini juu kwenye introduction nimemzungumzia mtu Kama Elon Musk ambaye yeye ameweza kufanya mambo ambayo nchi ndio zinashindana kufanya,yeye anafanya pekee yake tena nazaidi,anarusha marocket huko space na anandoto kujenga mji sayari nyingine,lakini tukumbuke huyu ni muafrika mwenzetu, kaondoka Afrika akiwa na miaka nafikiri 12,na yeye mwenyewe anasema hana hata degree ya eurospace engineering ni amejifunza na kuwekeza muda mwingi kujielimisha na nguvu ya kudhubutu.

So Vijana wa Kitanzania pia tunapaswa kuwa na hizi mindset ya kutaka kujenga mambo makubwa zaidi yetu na kuweka malengo ya muda mrefu,hapa serikali itatumia nguvu ndogo kumuwezesha mtu ambaye already anajua anapoenda na amedhamiri kufika kwa njia yoyote Ile.

Sorry gazeti limekuwa refu sana
True pia kulingana na upatikanaji rahisi wa taarifa ni rahisi kufanya chochote utakacho na sio lazima uwe umekaa darasani.kupitia youtube ni rahisi kujifunza KILA kitu na kuwa utakavyo
 
Kuna kupata faida ya milioni 4 kwa eka moja,ndani ya miezi 3 hadi 6 kupitia kilimo tena kwenye maeneo Kavu yenye mvua haba. Taweka andiko lisaidie watu jinsi ya kujinasua na umasikini kupitia kilimo cha mazao ya nyonyo upate mafuta kisha mafuta hayo utengeneze sabuni.Then kupitia sabuni ndio upate return. Eka kumi pata milioni 40 ndani ya miezi 3 hadi 6.
Tafundisha jinsi ya kutengeneza mashine rahisi ya kukamua mbegu za mafuta na mashine rahisi za kutengeneza sabuni.Mmea wa nyonyo ni kusafisha Shamba panda palilia mara moja subiria mavuno ukianza kuvuna baada ya miezi 3 utaendelea kuvuna hadi miaka 2.So possible kwa heka 10 kupanda milioni 200 ndani ya miaka 2 kupitia kutengeneza sabuni.
Sabuni ni basic needs haikosi soko KILA siku utauza.
 
Back
Top Bottom