SoC01 Kilimo cha mtaji wa Tsh bilioni 25 ndicho kilimo kitakachokuwa uti wa mgongo wa Tanzania

SoC01 Kilimo cha mtaji wa Tsh bilioni 25 ndicho kilimo kitakachokuwa uti wa mgongo wa Tanzania

Stories of Change - 2021 Competition

zambezi_21

Member
Joined
Jul 18, 2021
Posts
7
Reaction score
14
Ni kweli kwamba Dunia kwa Sasa ipo katika mapinduzi ya nne ya viwanda na sekta inayoongoza mapinduzi haya ni sekta ya teknologia na habari. Matajiri wakubwa wa Dunia kwa kiasi kikubwa ni Vijana na wazee ambao wamewekeza katika sekta hii kwa kiasi kikubwa,hapa nawazungumzia watu Kama Jeff Bezos,elon musk,mark zuckerberg,bill gates na wengine ambao ndio kwa sehemu kubwa wanamiliki utajiri wa Dunia.

Nchi nyingi za Africa Zina mchango mdogo Sana katika mapinduzi ya viwanda yanayotokea kwasasa tofauti na hapo wajasiria mali wengi waafrika imekua ni vigumu kwao kwa kupitia sekta ya teknologia na habari kutengeneza uchumi unao endana na Hawa matajiri wanao endesha uchumi wa Dunia kutokana na mifumo mibovu ya kiuchumi katika nchi za Africa lakini pia ugumu wa bidhaa zetu kuheshimika na kukubalika katika soko la Dunia.

Kwa namna moja au nyingine waafrika na watanzania hususani, inabidi kabla ya kushiriki kikamilifu katika sekta hii kiongozi ya teknologia na uchumi,tuanzie katika sekta ya kilimo Kama nchi tajiri zilipo anzia, kwa wakati huo huo tuchanganye kilimo na technologia na habari hapa ndipo tutajenga uchumi wa kweli.

Kilimo kinachoendelea hapa tanzania kwa asilimia kubwa sicho ambacho kinauwezo wa kuinua uchumi wetu na kujilinganisha na walioendelea. Tanzania tuna aridhi ambayo inafaa kilimo hekta million 13.5, zipo nchi ambazo ukubwa tuu wa nchi haufiki hecta million 13 lakini wanazalisha mazao ya kilimo Mara 2 zaidi yetu.

Uwekezaji mkubwa katika kilimo unaleta tija katika uchumi wa nchi kwani kilimo ni sekta ambayo inashabihiana mojakwamoja na ukuaji wa viwanda pamoja na mambo mengine. Katika nchi zilizoendela wakulima wanauwezo wa kuzalisha mazao pamoja na kuyaongezea thamani hapo hapo shambani mpaka kuwa bidhaa ambayo inaweza ikapelekwa moja kwa moja kwa mlaji.

Shambani la hekta 10000 linaweza kuzalisha chakula mpaka tani 110,000 Za nafaka kwa mwaka. Hili ndilo shamba la mkulima na mtanzania wakawaida anapashwa kudhamiria kuliendesha. Shamba hili pia kwa kutumia teknologia mbali mbali lina weza kuzalisha umeme wa mega watt 15 Kwa kutumia mtambo wa umeme ambao unatumia makuti ya mazao Kama mahindi,alizeti na mengine (biogas power plant au straw power plant). Kwa maana nyingine baada ya kulima mkulima atavuna kwa kutumia combine havester,ambapo kwa ukubwa huu wa hekta 10,000 combine havester aina ya (Claas Lexion 770 TT)Inaweza kuvuna shamba lote,mashine hii inavuna inapukuchua nakumwaga kwenye gari la nafaka. Baada ya hapo mkulima atatumia ( Claas Quadrant 3200 RC T) Kukusanya makuti yaliyoachwa chini. Makuti hayo baadhi yataenda kuingia kwenye mtambo wa kuzalisha umeme straw power plant au biogas power plant. Baada ya makuti haya kutumika kuzalisha umeme ule uji utakao bakia Kama taka za mwisho ni bidhaa adhimu Sana ambapo mkulima atatumia tena shambani Kama liquid fertilizer. Baadhi ya makuti yanataingizwa kwenye machine kuyakandamiza na kukausha maji halafu kutumika kutengenezea bidhaa mbali mbali Kama mbao (chip wood) au matofali (straw block)

Shambani pia mkulima ataweza kuweka viwanda mbali mbali kama kiwanda cha mafuta ya alizeti (vegetable oil distillation factory) Kiwanda cha gas (katika kutengeneza umeme wa biogas patazalishwa kwa wingi gesi ya methane ambayo utaweza kuzalisha umeme ama kuiandaa kwa ajili ya matumizi ya nyumbani) pia kiwanda cha unga (wheat and corn flour milling factory)

Shamba hili litahitaji matrekta makubwa ambayo ndiyo yanaongoza kwa ufanisi duniani. Hapa nazungumzia trakta Kama Case IH Quadtrac 620 walau moja,Case IH Quadtrac STX 375 pia moja,Case IH Maxxum 130 CVR moja na mengine pia machine za kuandalia na kupandia shamba Kama Gregoire Besson Semi Mounted Plough, Farmet Kompaktomat K1570, Bourgault 3420-100 Paralink Hoe Drill, Horsch Maestro 36 row na nyingine hizi zote ni za kuandaa shamba pamoja na kupanda

Pia shamba la ukubwa huu linahitaji Agricultural Drone Korec eeBe SQ,hii ni drone ya teknologia ya Hali ya juu Sana,kazi yake kwa kutumia kamera zake maalumu inaonesha uwiano wa maji baada ya kumwagilia,rutuba katika udongo,adhari za magonjwa na wadudu,kiwango cha mbolea kinachohitajika sehemu maalumu. Kwa kutumia GPS system technology taarifa hizi itazituma katika mashine zingine zote ili kujua sehemu fulani kipindi kingine panahitaji maji zaidi au mbolea zaidi au dawa zaidi. Na mwisho wa siku kwa kutumia data kutoka kila mashine Kama vile combine havester ambayo pia wakati inavuna inapima pia na wingi wa mavuno pamoja na ukubwa wa puche iliyovunwa kwenye GPS location flani kwahiyo unajua sehemu fulani ulipata mavuno machache au mengi kwa sababu gani. Hapa pia panahitajika Agricultural Drone DJI MG 1 walau ziwe kumi, hizi hutumika kwa ajili ya kupulizia dawa na kumwagilia liquid fertilizer, zinaruka umbali wa mita 3 kutoka kwenye mmea na moja inamwagilia upana wa mita 5, pilot mmoja anaweza kuziendesha 5 kwa pamoja. Hizi zinawasiliana na mashine zingine zote kujua wapi pakuwekwa kiasi gani cha mbolea au dawa japo pia mbolea hii unaweza pia kiimwagilia kwa kutumia irrigation system inayofungwa mwanzoni.

Shamba hili linahitaji miundo mbinu madhubuti shambani kwa maana ya barabara, silos za kuhifadhia nafaka ( grain silo plant) walau 3 za tani 5000, na 3 za tani 3000. Magari ya usafirishaji,magari ya moto (fire truck ya kuzima moto)mizani ya kupia nafaka,kituo cha kujazia mafuta,Majengo ya viwanda,Majengo kwa ajili ya kuhifadhia makuti( jengo la chuma lisilo na umeme ili kuepuka hatari ya moto) na jengo la karakana kwa ajili ya kutengeneza mbao,matofali na bidhaa zitokanazo na mbao. Pia Majengo ya makazi kwa ajili ya wafanya kazi,ofisi pia kanteen ya chakula.

Mradi wa shamba hili unahitaji walau mtaji wa billion 11 za kuanzia (initial investment)na kwa kipindi cha miaka walau mitano na kuendelea faida yake kubwa inapaswa irudi shambani ambapo kwa ukamilifu wake billion 25 zitatosha kuwa mtaji wa kuendesha shamba hili kwa uwezo wake kamilifu. Mtaji huu kwa kiasi kikubwa utategemea msamaha wa kodi katika kuingiza machine zote za kilimo nchini. Shamba hili linauwezo wa kuzalisha tani 110,000 za chakula kwa mwaka kwa ajili ya masoko ya ndani Kama azam,azania na milling factory zingine pia baadhi ya mazao kwa ajili ya masoko ya nje,hapa patalimwa mahindi,ngano,shairi,maharage,alizeti pamoja na viazi. Shamba hili linauwezo wakuzalisha tani 350,000 mpaka 400,000 za makuti ambazo zingiweza kupotea aridhi lakini hapa zitatengeneza umeme mpaka mega watt 15 au 45,000,000 Nm³ Methane gas. Kwa bajeti hiyo niliyoiweka ya kuanzia (initial investment) ya billion 11,hapa unaweza kuweka mtambo wa umeme wakuzalisha mega watt 1.5 kwa maana nyingine unaweza ukahudumia umeme kwa mkoa mzima kupitia shamba hili

Pamoja na faida zingine katika shamba hili, kwa kutumia mashine na matrekta makubwa yaliyopo shambani hapa itawasaidia wakulima wote wa pembembezoni mwa shamba wenye mashamba yenye ukubwa wa ekari 1000 na kuendelea kutumia mashine hizi wakati hazina kazi shambani,ambapo kwa muda mrefu wa kuendelea kufanya hivo wakalima Hawa watajijengea uwezo wa kuweza kuagiza mashine zao wenyewe kutoka nje za ukubwa huo. Pia umeme utakao zalishwa hapa unaweza kuelekezwa katika vijiji vya Jirani na mwingine kuwekwa katika grid ya taifa kwa makubaliano na tanesco. Pia kwa kutumia machine Kama seed dressing machine na zingine patazalishwa mbegu bora kabisa kwa ajili ya wakulima wa pembeni na kwa ajili ya biashara,pia mbolea inayotoka katika mtambo wa umeme na gesi unaweza kulitosha shamba Hili pamoja na wakulima wa pembembezoni na kwa ajili ya biashara pia.

Kiuhalisia unahitaji muda mrefu wa ujuzi katika kilimo kuweza kuendesha shamba la ukubwa huu. Hakuna linaloshindikana,kwa kupitia mashamba madogo ya hekari chini ya elfu moja watanzania wanaweza kudhamiria kujijenga kiujuzi na pia kwa kuwatembelea wenzetu na kutumia wataalamu wa ndani ikawezekana watanzania wakawaida kabisa kumiliki na kuendesha mashamba ya namna hii. Mtaji wa pesa nyingi namna hii unapatikana huko huko shambani. Wapo watanzania wengi waliowekeza katika mazao ya muda mrefu hapa nazungumzia machungwa,maembe,maparachichi mkonge na mengine tena wakiwa wameanza kwa kipato kidogo lakini leo hii wanatengeneza mabilioni ya shilingi. Bila kubadilisha mitazamo yetu katika kuiendea sekta hii ya kilimo na kuamua kudhamiria kufanya kilimo chenje kujenga uchumi wetu mkubwa wa taifa zima,wazungu wataendelea kutucheka na kutushangaa kwamba kwanini tumejifunga akili zetu na kushindwa kudhubutu kutumia aridhi yetu kujiendeleza na kuweza kushindana na mataifa makubwa kiuchumi. Binafsi nathubutu kusema kwamba aridhi tuliyonayo kwa ajili ya kilimo ni mali kubwa tuliyopewa na Mwenyezi Mungu kuliko madini,mafuta au gesi ambazo kila siku tunakimbizana nazo.


Screenshot_20210724_164838.jpg
 
Upvote 9
Acha matusi, maneno uliyoandika yanamaelezo mengi Sana kwamba wewe ni mtu wa aina gani, ni utoto na ufinyu wa fikira kumtukana mtu ambaye humjui kisa upo nyuma ya keyboard unataipu tuu utu na heshima vinakutoka.. kuna uwezekano mkubwa unayemtukana ukikutana naye utamsalimia na kumpaheshima zote kwahiyo mitandao yakijamii isikufanye kuwa limbukeni usiyekua na adabu kwa wenzako... Kuhusu unayosema kuhusu kilimo huna ujuzi navyo wala huelewi chochote kuhusu kilimo traditional na kilimo cha kisasa. Hiyo unayosema kulima eneo dogo hicho kinaitwa urban agriculture,wanalima watu waliopo mjini. Na hatasiku moja huwezi kulima nafaka ambazo ni large scale kwakutumia hicho unachoongea. Billgate ndiye raia anyeongoza kwa kumiliki aridhi kubwa marekani,analima kwa mbinu nilizo zieleza,naomba kwasababu wewe ni mjuzi Sana n updated kampe somo kwamba anakosea, una approach negative Sana ya maendeleo na huwa kawaida mtu anayeanza sentensi zake kwa kusema huwa sisi tanzania tuko hivi wale wako hivi,namuona mtu aliyebweteka,akili ndogo na ni anti change... Hili andiko halikudhamiria watu wa aina yako,endelea kuzunguka mitandaoni kuilaumu serekali nakutukana watu maana nahisi huko wewe ni mjuzi zaidi

Sent from my vivo 2015 using JamiiForums mobile app
Dogo acha hasira zenye misingi ya sheria kandamizi!! ukubwa umeuona siraha?? humu ni Jf jukwaa huru wote tuko sawa!! kimwili! kijinsia, kiumri nk! ningekutukana usingevumilia!! na zipo sheria zake umejiunga tu kichwa kichwa.....

km hujui wee mzee kutamka tu neno eti flani ''amekutukana!!..... una kosa kisheria ya jamhuri!! weye sasa ndo unatukana. km mie nina domo chafu!.. je wewe mzee mzima kumtamkia mtu usiye mjua. eti ni Limbukeni .hana utu na heshima, ufinyu wa fikra! eti ni mtoto wkt,

huyo mtu hujui kuwa, anajua matumizi ya wembe ni u-bogus zaidi ya bogus wenyewe!.... mtu km wewe hustahili heshima!! heshima ya kuwa jukwaa huru!! hata km ni vipi! ...niamini kwa hili sawa? !.... Sikia wee mzee

nina jua kilimo kuliko weye unavo dhania...kuanzia jembe la mkono, kushika plough kwa kutumia Punda, farasi, mpaka nasafu ya ng'ombe!, kienyeji zaidi!..... siyo kilimo tu!! bali hata kusaga nafaka, kusombea maji km JKT Msange 823kj tumefanya sana kazi hizi!

kukamua maziwa kienyeji na kwa mshine huniambii kitu, kuchunga mifugo hao malisho mazuri, ni kipindi gani wako onheat na wanahitaji nini! nk! zaidi ya yote nilisoma shule ya mchepuo wa Agricultural school kuleee!!! ivo najua Agromechanics vizuri, Floriculture,Oreliculturenk!

Shamba la kijiji chetu nilichozaliwa mie! ni la mfano wa kuigwa bongo nzima hakuna!! nimelima sana ki-ushirika, usinichukulie poa!! mpaka tukanunua Trekta za kijiji, mpaka leo yapo!! km hujui Drip irrigation's siyo kilimo cha mjini big no!!

ni aina ya kilimo kilichoanzia Israel ni majishamba makubwa hatare huko Negev Desert!!.... Bongo nzima hkn! usilinganishe na subsistance farming za kwenu hapo bongo!

Hao waliokufundisha eti ni kilimo cha mjini ni waongo! washtaki mahakamani ....Ok! umesema Billgate!!!!..huyu ni mtoto wa juzi juzi tu hapa!! anahitaji msaada kuwa na ardhi siyo eti ndo umekuw gwiji wa kilimo!! km yuko ivo anahitaji msaada! pamoja na uzungu wake! \

wapo wakulima hasa wana Ma bank, na wengine ndo waligundua zana za kilimo hizi tunazo tumia km Merovengian Family, Roth child inter., Henry Ford family nk, kwa uchache mno!! .....ni wakulima tangu zama za Industrial Revolution in Europe! mpaka leo!

Hao walilima kwa kuzalisha mazao mpaka nje ya mipaka ya nchi zao!! na mpaka leo wana fanya hivyo hukooo Australia, New zealand, St Hellena, SA. Kenya jirani yenu hapo, visiwa vya Mayote to mention a few!!

Wana kijiji wazee mnatabia moja mbaya sana!!....siipendi Nawashauri muiache .....vinginevyo hili jukwa si mahali sahihi kwenu!!!.... ni hii ya kulazimisha hoja zenu mfu! za nguvu, ambazo hazipigwi rungu...

yaani wewe sababu umeanza kuota vi mvi basi ukubaliwe wewe tuuuuu!! ......upigiwe makofi wewe km juha!! basi bichwa kuuubwa unaenda kumsimulia mkeo usiku nyieeeeeeee?? hee!! mna bahati sana nakwambia!.........hamna hata uvumilivu km Mimi!!!
 
maneno uliyoandika yanamaelezo mengi Sana kwamba wewe ni mtu wa aina gani
Mzee usisome kwa hasira..km vepi kunywa maji baridi kwanza jagi zima af uje usome hoja tunduizi!! usionee dagaa
 

Humu kwenye hii thread unasema kua ulikua na mpenzi anaitwa MARY, alipata ajali akiwa na mimba yako.

Hapa kwenye uzi wa watu wa kilimo, unajitapa kua na sura nzuri ya kutokuachwa ambayo ndio kwenye avatar yako..sasa wewe ni shemale? Na zaidi unasuta hata watu ..
Daaa! mie bana ndo nilivo !! nashangaa hata form za ubunge nililetewa ivivi?? kisa umaarufu! wakt nimelala! hata km ingekuwa ni kweli !!.....kwani hujawahi sikia kuna watu wana Double sex?? au wasagaji!!nk, hiyo haina maana nijitangaze!! siyo dhambi kuwa ivo!!

pia avatar yangu siyo siri kiviile yeyote anaweza akaingia akafanya yake!!! hata wewe unaweza convert avatar yangu ukafanya yako!!! kwa kuwa tu umetamani uwe-idealistic, na umaarufu wangu wangu tu baaasi!! hujasikia watu wana hack e-mail za watu wengine??

au mkuu humu ni mgeni nini?? hujui tunavoishi!! mfano lile jamaaa linalo sumbua sana Instagram mpka leo, Fb JF nk, linaitwaje lile jamaa?? ....kigogo!!!!... Magufuli na Msiba wake walipata taabu sana tena wakalitafuta weee!! mara lije dume! mara mtoto, mara mzee, mara mzungu..

kifupi lile jamaa halikueleweka mpaka leo!! hadi jiwe kaaga!!! na bado likamtoa tu!! juu ya mazishi yake!! asa huo woote ni umaarufu wake baba!! na mie ivo ivo ukienda mitandao yote ya ulaya utaniona huko!!! ukienda senate utanipata na ukienda Lesotho nk! nipo huko.....

Mara nyingi sisi watu maarufu huwa tuna fuatiliwaa sana, kwa vyovyote vile kwa sababu tu ya mawazo yetu mwanana na mapana!! sometimes hata kutupiga madongo,, kufanya ivi mara vile!! mara mtuite sie Free Manson km Diamond!! mara tumetoa kafara ndg zetu,

mara muibe avatar mfanye mnavyotaka nk ili mradi tu na wewe uwe maarufu sababu umemuongelea mtu fulani maarufu!! na mie hii ya kuwa maarufu ilianza nikiwa Bado mdogo sana chekechea hukoo paleee Kamunyonge Field force Unit kindergarten!!

leo hii sitaku shangaa weye wa mbagala!!.. si unaona Mange kaandika kidogo tu!! Maweeee! watu wakalipuka Dunia nzima Mange kaiweka kiganjani walianzaga hivi hivi!! ndo damu zetu zilivo!! na

wewe si wa kwanza kunishangaa kwa hili! na nikuulize ivi humu JF hakuna masharti kwamba Triple sex wasiingie humu??!! mbona shega tu mwana!! yaani mwana ukinikalia vibaya nashughulika kotekote na ngoma inaenda!! najua wewe si wa kwanza! umeniitaje??

ok!! so hapa ni jirani kabisa na shule ya Msingi Kamunyonge!! kwa chini hivi kuna uwanja wa ndege! unaweza kuuliza hawa wajeda wa Lugalo palee getini habari zangu pia! ukiambiwa na hawa ujue ndo haswaa mie!! lkn hao wengine wame hack!! ndo tulivo watu mashuhuri sisi!

Hiyo kwetu na kwa umaarufu wetu ni tumezoea, km wewe ulivyo fanya!! ni kawaida sana!! Na ukiona ivo umenikubali sana!! ila usiige!! humu kuna sehemu utanikuta mie huyu huyu ni Mbunge wa Cuf!! at the same time nasoma Canada endelea kutafuta!! utaniona kiivo!!

Na hii yote ni kupendwa wala si kingine!!....ndo maana nikasema mnipe ubunge tu!! Make weye nilikupa kazi ya kunijua bure!.... ulienda nyuma huko ukasoma yangu yoooote!! safi sana! endelea msome na aaa!! .....ngoja nikuache kwanza!

na kuna..
 
Back
Top Bottom