Kilimo cha nyanya msimu wa 2021/2022

Naomba kuuliza mwenye uzoefu,
1-Heka moja inaweza gharimu kiasi kuanzia mbegu mpaka kuvuna!?
2-Ubora ikizingatiwa makadirio ya chini kabisa unaweza pata tenga ngapi!?
-Nina heka kadhaa maeneo ya Kilimanjaro (maeneo ya Tpc kiwanda cha sukari), Pia nina hela kadhaa Bagamoyo (naomba ushauri eneo zuri kuweza kuweka project hii.
Kwa uzoefu mimi ni mkulima wa mpunga, hivo nahitaji ABC za kilimo cha nyanya, nimesoma humo juu ila bado sijapata mwongozi kamili

Asanteni
 
Nakubali kaka, kuhusu mbolea tokea nimeanza natumia ya kuku mpaka leo hii na mzigo now umefikia hapa....Ila kwa zao la nyanya madawa ni muhimu hususani za wadudu la sivyo unaweza toka patupu....Mungu ni mwema
Ulipata soko?
 
Hizi mbegu za epinav jamani vipi....aliyewaji kulima tanzanite1 au bansal1
 
Mkuu maeneo ya Kilimanjaro nyanya zinastawi sana na kunenepa, mavuno mengi kwa mujibu wa wakulima wa huko (rafiki na wakulima wenzangu). Changamoto ya huko wakulima wengi wa nyanya hivyo zinafurika sokoni unauza bei ndogo sana.
Maeneo ya Bagamoyo nyanya zinastawi lakini changamoto kubwa magonjwa hasa mnyauko na ukungu. Soko la nyanya maeneo hayo ni zuri kwa maana ya bei ni kubwa kuliko Kilimanjaro. hapo unaweza kupeleka Dar kwa urahisi au kutafuta mteja toka Dar akafuata shambani. Nashauri utafute mteja atakaye fuata shambani.
Tatu na mwisho nashauri utafute mbegu nzuri zinazofaa ukanda wa Pwani kama utalima Bagamoyo, pia usilime nyanya nyanya za kuvuna kuanzia mwezi wa 8 hadi wa 9 bei inakuwa chini sana.
 
Nyanya bagamoyo alime kuanzia mwezi wa tisa. Pesa ipo mpaka mwezi wa nne.
Alime mkombozi F1, Maji na madawa muhimu.
 
Nyanya bagamoyo alime kuanzia mwezi wa tisa. Pesa ipo mpaka mwezi wa nne.
Alime mkombozi F1, Maji na madawa muhimu.
VP MBEGU GANI INAPAMBANA NA UGONJWA WA MNYAUKO KWA PWANI? MM NIPO CHALINZE
 
Vipi mtu akisiha mbegu January hii?
 
Ni mbegu gani zilifanya vizuri
 
kuna mbegu zinaitwa Tomato To135 toka kampuni ya Africasia jaribuni hii nyanya ni nzur na bei yake iko chini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…