Kilimo cha nyanya msimu wa 2021/2022

Kilimo cha nyanya msimu wa 2021/2022

Naomba kuuliza mwenye uzoefu,
1-Heka moja inaweza gharimu kiasi kuanzia mbegu mpaka kuvuna!?
2-Ubora ikizingatiwa makadirio ya chini kabisa unaweza pata tenga ngapi!?
-Nina heka kadhaa maeneo ya Kilimanjaro (maeneo ya Tpc kiwanda cha sukari), Pia nina hela kadhaa Bagamoyo (naomba ushauri eneo zuri kuweza kuweka project hii.
Kwa uzoefu mimi ni mkulima wa mpunga, hivo nahitaji ABC za kilimo cha nyanya, nimesoma humo juu ila bado sijapata mwongozi kamili

Asanteni
 
Nakubali kaka, kuhusu mbolea tokea nimeanza natumia ya kuku mpaka leo hii na mzigo now umefikia hapa....Ila kwa zao la nyanya madawa ni muhimu hususani za wadudu la sivyo unaweza toka patupu....Mungu ni mwema
Ulipata soko?
 
Hizi mbegu za epinav jamani vipi....aliyewaji kulima tanzanite1 au bansal1
 
Naomba kuuliza mwenye uzoefu,
1-Heka moja inaweza gharimu kiasi kuanzia mbegu mpaka kuvuna!?
2-Ubora ikizingatiwa makadirio ya chini kabisa unaweza pata tenga ngapi!?
-Nina heka kadhaa maeneo ya Kilimanjaro (maeneo ya Tpc kiwanda cha sukari), Pia nina hela kadhaa Bagamoyo (naomba ushauri eneo zuri kuweza kuweka project hii.
Kwa uzoefu mimi ni mkulima wa mpunga, hivo nahitaji ABC za kilimo cha nyanya, nimesoma humo juu ila bado sijapata mwongozi kamili

Asanteni
Mkuu maeneo ya Kilimanjaro nyanya zinastawi sana na kunenepa, mavuno mengi kwa mujibu wa wakulima wa huko (rafiki na wakulima wenzangu). Changamoto ya huko wakulima wengi wa nyanya hivyo zinafurika sokoni unauza bei ndogo sana.
Maeneo ya Bagamoyo nyanya zinastawi lakini changamoto kubwa magonjwa hasa mnyauko na ukungu. Soko la nyanya maeneo hayo ni zuri kwa maana ya bei ni kubwa kuliko Kilimanjaro. hapo unaweza kupeleka Dar kwa urahisi au kutafuta mteja toka Dar akafuata shambani. Nashauri utafute mteja atakaye fuata shambani.
Tatu na mwisho nashauri utafute mbegu nzuri zinazofaa ukanda wa Pwani kama utalima Bagamoyo, pia usilime nyanya nyanya za kuvuna kuanzia mwezi wa 8 hadi wa 9 bei inakuwa chini sana.
 
Nyanya bagamoyo alime kuanzia mwezi wa tisa. Pesa ipo mpaka mwezi wa nne.
Alime mkombozi F1, Maji na madawa muhimu.
 
Sawa lakin naona kama umeiwahisha sana, kwan nyanya za saizi hiyo huenda zikawa nyingi, mara nyingine tegea uwe unapandia mwezi januar katikati za kuivia mwezi wa tatu bei yake huwa imechangamka sana. Ambapo unakuwa ulisiha mbegu mwezi wa 12 katikati.
Vipi mtu akisiha mbegu January hii?
 
Habarin Wana Jf, naomba msaada wa upatikanaji wa wanunuzi wa nyanya....nategemea KUVUNA mwanzoni wa mwezi wa KUMI panapo majaliwa, ukubwa wa shamba ni hekari moja, mbegu nilizotumia ni ASILA F1 na IMARA F1 nilichanganya mbegu japo nilizipanda kwa utofauti ili kujua mbegu Bora kwa msimu mwingine....Eneo nilipolimia ni BAGAMOYO.....ahsanteni
Ni mbegu gani zilifanya vizuri
 
kuna mbegu zinaitwa Tomato To135 toka kampuni ya Africasia jaribuni hii nyanya ni nzur na bei yake iko chini
 
Back
Top Bottom