Kilimo cha Tangawizi - Masoko, Mbinu na Ushauri Toka kwa Wadau

Jaguar

JF-Expert Member
Joined
Mar 6, 2011
Posts
3,437
Reaction score
1,027

Heshima kwenu wakuu.

Ninaambiwa na watu kwamba kilimo cha tangawizi kinalipa sana kwa sababu soko la uhakika lipo na ni zuri. Nimeshaelekezwa sehemu ambayo hili zao linakubali uzuri.

Ombi langu ni kwa wale wenye uzoefu na kilimo hiki wanipe A,B,C zote kuhusu kilimo cha zao hili. Ningependa kujua kuhusu gharama ninazoweza kukumbana nazo mpaka zao hili lifikie hatua ya kuvunwa toka shambani.

Thanks in advance.

MASWALI/ MAHITAJI YA WADAU KUHUSU KILIMO HIKI


MREJESHO WA WADAU


PIA, SOMA:

Kilimo Bora cha Tangawizi

UTANGULIZI:
Jina la kisayansi: Zingiber officinale
Familia: Zingiberaceae

Tangawizi ni aina ya zao la kiungo ambalo sehemu inayotumika ni tunguu (rhizome) ambalo huonekana kama mizizi ya mmea. Asili ya zao hili ni maeneo ya kitropiki ya bara la Asia na hasa katika nchi za India na China. Zao hili linazalishwa kwa wingi kutoka katika nchi ya Jamaica. Hapa nchini zao hili hulimwa katika mikoa ya Kigoma, Tanga, Morogoro, Pwani, Mbeya na Kilimanjaro.

Tangawizi hutumika kama kiungo katika kuongeza ladha, harufu na kuchangamsha katika vinywaji (kama soda, juisi, vilevi n.k) na vyakula mbalimbali kama mikate, biskuti, keki, nyama za kusaga, achari n.k. Hutumika pia katika viwanda vinavyotengeneza madawa ya tiba mbalimbali kama dawa za meno, kikohozi, tumbo na muwasho wa ngozi n.k. pia hutumika katika vipodozi kama poda n.k).

AINA ZA TANGAWIZI
Hakuna uthibitisho wa aina za tangawizi ambazo hulimwa Tanzania ila kuna dalili ya kuwa na aina za White Africa (Jamaica) na Cochin (flint).

BIOLOGIA YA MMEA WA TANGAWIZI
Tangawizi ni mmea unaotambaa chini ya ardhi, wakati wa masika hutoa majani juu ya ardhi. Jamaica ina rangi hafifu ya kahawia na tunguu fupi wakati Cochin ina tunguu fupi zaidi lenye ngozi ya rangi iliyo kati ya kijivu na nyekundu. Mmea una urefu wa futi mbili na majani yake ni membamba marefu ambayo hufa kila mwaka yakiacha tunguu ardhini likiwa hai. Maua ya mmea huu yana rangi nyeupe au manjano.

HALI YA HEWA NA UDONGO
Zao hili hustawi katika maeneo yenye hali ya kitropiki, kutoka usawa wa bahari hadi mwinuko wa mita 1,500 au zaidi. Huhitaji mvua kiasi cha mm.1, 200 - 1,800 na joto la wastani wa nyuzi za sentigredi 20 - 25. Hustawi vema katika udongo tifutifu wenye rutuba na usiotuamisha maji na wenye pH 5.5 – 6.5.

UPANDAJI
Zao la tangawizi hupandwa Kwa kutumia vipande vya tunguu vyenye kichipukizi kizuri angalau kimoja na huweza kukatwa katika urefu wa sm.2.5-5. Wakati mwingine, vichipukizi vinavyopatikana katika kumenya tangawizi huweza kuhifadhiwa na kutumika kwa kupanda. Kiasi cha kilo 336 - 680 cha vipande vya tunguu huweza kutumika kwa kupanda katika ekari moja.

Nafasi inayotumika kupanda ni kati ya sentimita 23-30 kwa 15-23 na kina cha sentimita 5-10 na mara nyingi hupandwa katika matuta, hivyo unaweza tengeneza tuta lenye upatana wa mita 1. Baadhi ya mazao huweza kupandwa katika shamba la tangawizi ili kuweka kivuli chepesi ingawa si lazima kivuli kiwepo. Inashauriwa kumwagilia maji endapo mvua inakosekana.


MBOLEA
Wiki 1-2 kabla ya kupanda weka mbolea ya samadi au mboji kiasi cha tani 10 - 12 Kwa ekari na kwa kukuzia weka kiasi cha NPK. N 40 – 48 kg, P2O5 31.2 – 32 kg, na K2O 40 – 48 kg. Mwanzoni tumia nusu ya Nitrogen na kiasi chote cha P na K, kiasi kilichobaki cha Nitrogeni kitumike siku ya 45 na 90 baada ya kupanda. Tandaza nyasi shambani kuhifadhi unyevunyevu hasa pale kivuli kinapokosekana. Palizi hufanywa mara magugu yanapoota, dawa ya kuua magugu, Kama simazine hutumika.

UVUNAJI
Tangawizi huweza kuwa tayari kwa kuvuna kati ya miezi 9-10 baada ya kupanda, wakati majani yake yanapogeuka rangi kuwa njano na mashina kusinyaa. Tangawizi inayohitajika kwa kuhifadhi kwenye kemikali (preserved ginger in brine) huvunwa kabla haijakomaa kabisa, wakati ile iliyokomaa kabisa huwa kali zaidi na huwa na nyuzi hivyo hufaa kwa kukausha na kusaga. Mavuno hutofautiana kulingana na huduma ya zao, mavuno yanaweza kuwa kiasi cha tani 8 - 12 cha tangawizi mbichi huweza kupatikana kwa ekari.

Chanzo: horttechservices.com
 

Attachments

  • ginger.jpg
    122.1 KB · Views: 37
Akhsanteni@ze marcopolo & ndoa.
 
Nataka kulima tangawizi mkoani Mbeya hususani Tunduma.

Swali kwa wataalamu; je, hali ya mkoani mbeya inakubaliana na zao hili?

Kuna jamaa kanambia kuwa zao hili linahitaji misimu miwili ya mvua kwa mwaka kwasababu tangawizi huchukua miezi nane hadi kumi kufikia hatua ya kuvunwa.

Nina hofu kama kweli mkoani mbeya mvua za vuli ni za uhakika.
Naombeni ushauri wenu wataalamu.
 
Reactions: apk
Thanks! Nimeotesha miche kama 6 kwa majaribio.
 
Je, ni wapi soko la tangawizi linapatikana kwa wingi? je kg 1 inakwenda kwa bei gani? wapi tangawizi soko lake la uhakika? Muhimi please coz nimesikia kuwa kuna viwanda vinanua Tangawizi, ningependa pia kujua bei zao kiwanda wanazonunulia.
 
Je ni wapi soko la tangawizi linapatikana kwa wingi? je kg 1 inakwenda kwa bei gani? wapi tangawizi soko lake la uhakika? Muhimi please coz nimesikia kuwa kuna viwanda vinanua Tangawizi, ningependa pia kujua bei zao kiwanda wanazonunulia.
Yeah,
Ngoja werevu wa hii issue waje.
 
Habari wandugu,

Natafuta mbegu ya tangawizi, nahitaji kupanda mwenye nayo au pia msaada wa maeneo zinapopatikana anisaidie tafadhali.
 
Habari ndugu zangu?

Kwanza mniwie radhi kwan kifaa changu kilizma chaji kabla sijapost. Nahitaji kupata maarifa juu ya kilimo cha tangawizi , je mbegu nzuri ni aina gan? Zinapatikana wap? Je huchukua muda gan mpaka kuvuna? Kama nikiweza kupata gharama Zake na faida. Nitafurahi pia kupata uzoefu mwingne juu ya kilimo hiki.

Asanteni sana
 
Wenye utaalam au uzoefu juu ya kilimo cha tangawizi, tafadhali mukuje pande hii.
 
Kwa ujumla tangawizi hustawi kwenye mwinuko kuanzia m 800 mpaka 1500 kutoka usawa wa bahari, kwa ujumla maeneo mengi inakostawi kahawa na tangawizi zinastawi.

KUANDAA SHAMBA
Andaa Shamba lako mapema, katua/lima kuanzia miezi ya
April, may au June, ni vizuri ukaanzisha Shamba jipya au lilikaa bila kulimwa kwa miaka mitatu, Lainisha udongo miezi ya August au September na kuanzia November unaweza kuanza kupanda.
.
KUPANDA

Tangawizi hupandwa kwa kuivunja vunja kwa kufuatisha mbingili zake. Panda tangawiz kwa cm 30 kati ya shina moja na jingine na cm 45 mpaka 60 kati ya mstari mmoja na mwingine. Tumia mbolea ya mboji au samadi na usitumie mbolea za kemikali kupandia, Kg 1000 za tangawiz hupandwa katika hekta moja na unaweza kuvuna kuanzia tani 10 mpaka 25 inategemea ukubwa wa mbegu, urutubishaji, kiasi cha maji na paliz.

Huchukua wiki mbili mpaka mwezi mmoja na nusu tngwz Kuota inategemea kiasi cha maji na joto kwenye udongo, ni vizuri kuzitandaza tangawz kwenye kivuli na kufunika na gunia na kuzimwagilia ili ziote kabla hujazikataka kwa ajili ya kwenda kupanda. Palilia Mara Majani yanaoota na pandishia udongo kwenye mashina ili tangawiz itanuke vizuri.

MAGONJWA
Tangawiz haishambuliw sana na magonjwa ila Mara chache hushambuliwa na kuvu (fungus).

KUVUNA
Huchukua miez 6 mpaka 18 mpaka kukomaa inategemea mwinuko toka usawa wa bahar na mvua.
Tangawiz haitaki maji yanayotuama kama vijaruba vya mpunga, maji yakituama kwenye shina la tangawiz kwa mda Fulani Majani ya tangawiz huwa ya njano na huanza kunyauka

Kuvuna Tani 10 kwa hekta moja ni kadirio la chini kabisa.. Kipindi soko linapokua zuri unaweza kupata kuanzia Mil 20 mpaka 60 kwa hekta moja, kuna wahindi ambao hununua tangawiz kwa wingi sana na wanaexport, wahindi hununua kg 1 kwa sh 3000, mpaka 3500 ukiuzia shambani. Uzuri tangawizi unaweza kusubiri soko zuri na ukauza kwa bei nzuri kwani zao hili hupanda bei haraka.

Jamani tusiogope kuwekeza, na kujaribu fursa mpya, Nina imani nimeeleweka na karibuni kama kuna maswali

Watu wengi wanashindwa kuzalisha tangawiz kwa wingi kwa kukosa mitaji ya kununulia mbegu kwani mbegu zake ni gharama, hivyo unashauriwa kununua kg chache walau kg 200 ukapanda eneo Dogo ili kuzàlisha mbegu ambazo utaweza kuzisambaza eneo kubwa, na kwa kulima eneo Dogo unaweza kupata uzoefu kupitia hapo na kujua kama eneo ulilolima ni sahihi na linafaa kwa kilimo cha tangawizi.

Sokoni tangawizi huuzwa sh 5000 mpaka 6000 kwa kg soko linapokua zuri, pia tangawz kuna msimu hushuka bei mpaka sh 2000 kwa kg. Usikatishe tamaa pale tangwiz inashuka bei mpaka sh. 1500, unaweza kusubir kwa mda mfupi na kuuza tangawiz kwa bei nzuri sana kwa kua bei yake huwa hupanda kwa haraka.
 
Hizo mbegu kwa hekta moja hugharimu shilingi ngapi?
 
Costs za kulima na kupanda mpaka unapovuna ni sh.ngapi mkuu, maana umeweka tu bei yake sokoni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…