Kilimo cha Tangawizi - Masoko, Mbinu na Ushauri Toka kwa Wadau

Kilimo cha Tangawizi - Masoko, Mbinu na Ushauri Toka kwa Wadau

Nimependa hayo matangawizi pichani. Kumbe mtu akikwambia "midole kama tangawizi" hajakutendea haki kabisa.

Wataalamu wa hili zao mje jamani kutuelimisha.

Asante mtoa mada.
 
Kwa wingi linalimwa alikokuwa mbunge mke wa Malechela. Ameweka initiative kubwa sana na kuna kiwanda cha tangawizi kilikuwa kianzishwe huko.
 
Tangawizi ya pili kwa ubora maana ina maji inatokea Mkongotema wilaya ya Madaba. Bei inategemea na msimu kwa kuanzia 800 tsh mpaka 1200 tsh
Madaba ruvuma, same. Muda wa kuvuna miezi 6-8-12. Bei ya shambani kilo 1000-1500
 
Maeneo yanayolima Tangawizi sehemu kubwa ni maeneo ya mwinuko aidha kwa mlimani au kutokea usawa wa bahari na udongo maeneo hayo ni ule wa kivolkano au asidi mfano ni Madaba-Ruvuma,kilosa,Moro vijijini-Morogoro,muheza,lushoto-Tanga,Mamba,Same-Kilimanjaro.
Tafadhalini wadau naomba kupata maelezo juu ya kilimo cha tangawizi kwa vipengele vifuatavyo:-
1/ Maeneo yanakolimwa hapa Tanzania. 2/ Muda wa kulima hadi kuvunwa 3/ Soko lake likoje hapa nchini
 
Kilimo cha viungo mara nyingi hatutumii sumu za viwandani na mbolea pia.
Point to note.
Salamu,
Kuna vitu vingine sio vya kuuliza,kwa maswali yako wala usijaribu kulima,
"
Kukodisha Shamba lake sh...?

Kulima Heka 1 sh...?

Mbolea sh ngapi....?

Heka 1 Kupalilia sh...?

Heka 1 kuvuna sh....?

Ni mikoa gani inasitwi",
Kwanza kabisa jua Hekta moja ni ekari kiasi gani, hakuna mkulima mtaongea kwa hekta, kila mmoja ataongelea ekari,
Shamba katufute utakapo pata uta negotiate bei ya kukodi, kulima shamba bei ni moja Tanzania nzima kwa jembe la kwanza na la pili, nenda shambani utakapo pata utajua kutokana na umbali trekta zinapopatokana, Kuvuna ni wewe kutafuta wavunaji, kila sehemu inategemea, ingia shambani fanya research mwenyewe.

Kupalilia bei ni standard Tanzania nzima, nenda shambani utajua na sio whatsapp, Mbolea bei ni moja Tanzania nzima, pata shamba utajua gharama za kufikisha shambani toka uliponunua, utapata gharama halisi.

Nakushauri usiingie, kilimo kinataka utayari na ku-focus kwenye challenge na sio mauzo.

Karibu.
 
Back
Top Bottom