sky walker
JF-Expert Member
- Feb 3, 2018
- 1,160
- 831
Kamefika kwenye kutoa mchanganuo wa mapato kakalala mbele! Naona article kaliyokuwa kame-copy na kupaste haina mchanganuo huo!
Na angemalizia faida na bei zake ingekuwa poa sana.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kamefika kwenye kutoa mchanganuo wa mapato kakalala mbele! Naona article kaliyokuwa kame-copy na kupaste haina mchanganuo huo!
Kwa mujibu wa data zake mbegu 2 million, na ndio inaleta jumla husika.Mbegu ni laki 2 au million 2?
Nataka kujua mauzo ya heka moja faida inakuwa ni sh ngapi?Kwa mujibu wa data zake mbegu 2 million, na ndio inaleta jumla husika
Hilo ni swali ambalo wengi wetu tunahitaji majibu. Mtoa mada hajaweza kuainisha mavuno yanakuwaje kwa hekari hapo ndipo tungeweza kukokotoa makadirio ya faida.nataka kujua mauzo ya heka moja faida inakuwa ni sh ngapi
Maana wengine tuna taka tutoke kwa kilimo sasa bila kukaa chini na kuchambua vizuri inatupa wakati mgumuHilo ni swali ambalo wengi wetu tunahitaji majibu,,,mtoa mada hajaweza kuainisha mavuno yanakuwaje kwa hekari hapo ndipo tungeweza kukokotoa makadirio ya faida
Kwa uzoefu wangu kwa eka moja unahitaji si chini ya kg1,000 ya mbegu, afadhali kg 1,300. Na kama umelima vizuri na ardhi yako inakuwa nzuri na umepalilia ipasavyo unaweza kupata kati ka kg 6,000 mpaka 9,000 kawaida.
Ukiacha tena kwa ajili ya mbegu kg 1,300 utauza kg4,700 mpaka kg7,700 ya tangawizi mbichi sokoni. Ila mwaka wa kwanza ni majaribio unaweza kupata chini ya hayo sababu ya kukosa uzoefu wakati wa kupanda au kupalilia au mengineyo. Bei ya Kg moja ya mbegu inategemea lini unapojaribu kuinunua.
Kwa mfano mwaka jana tumenunua kwa Tsh800 kg moja, mwaka huu inawezekana bei ya kg ni tsh1,000 hapo Madaba. Faidha ipo sana, lakini unahitaji muda wa kujifunza na pia kutafuta soko. Miaka mengine wanunuzi watakuja mpaka shamba lako mengine inabidi uwatafute sana.
Kwa ufupi mtaji wa kuanzia ni kubwa kidogo lakini faidha ni kubwa sana ukijitahidi kulima vizuri na kuitunza (shamba lako likiwa mbali na bila ulinzi wezi wanaweza kuja na kuiba tangawizi lako). Wengine wamelima eka nyingi na saizi wanakuwa na pesa ya kutosha.
Mimi binafsi silimi, analima mke wangu, lakini baada ya Miaka miwili tangu alipoanza anaweza kujenga nyumba nzuri kijijini na analeta pesa ya kutosha kwa familia Dar es salaam.
Kama ni kilo 1000 na bei huwa ina range kwenye 800,1000, hadi 1300 sidhani kama inafika naona jamaa alipigia bei ya kawaida buku mbili.Sidhani kama kuna uhalisia wa bei ya tshs milioni mbili kwa ekari moja,mwaka mmoja uliopita,nilijaribu kulima robo eka Mkoani Kilimanjaro,nilitumia debe mbili za mbegu ambazo hazikzidi hata laki moja. Labda utofauti wa maeneo huenda ukasababisha bei iwe tofauti lakini si kwa kiasi kikubwa hivyo......
Ila tangawizi si unaweza uka zihiifadhi na zisiharibikebei tatizo mwaka jana tanga bei ilishuka hadi kilo 650
Na kilimo cha tangawizi kina chukua mda gani hadi kutoka shambani?Kwa uzoefu wangu kwa eka moja unahitaji si chini ya kg1,000 ya mbegu, afadhali kg 1,300. Na kama umelima vizuri na ardhi yako inakuwa nzuri na umepalilia ipasavyo unaweza kupata kati ka kg 6,000 mpaka 9,000 kawaida. Ukiacha tena kwa ajili ya mbegu kg 1,300 utauza kg4,700 mpaka kg7,700 ya tangawizi mbichi sokoni. Ila mwaka wa kwanza ni majaribio unaweza kupata chini ya hayo sababu ya kukosa uzoefu wakati wa kupanda au kupalilia au mengineyo. Bei ya Kg moja ya mbegu inategemea lini unapojaribu kuinunua. Kwa mfano mwaka jana tumenunua kwa Tsh800 kg moja, mwaka huu inawezekana bei ya kg ni tsh1,000 hapo Madaba. Faidha ipo sana, lakini unahitaji muda wa kujifunza na pia kutafuta soko. Miaka mengine wanunuzi watakuja mpaka shamba lako mengine inabidi uwatafute sana.
Kwa ufupi mtaji wa kuanzia ni kubwa kidogo lakini faidha ni kubwa sana ukijitahidi kulima vizuri na kuitunza (shamba lako likiwa mbali na bila ulinzi wezi wanaweza kuja na kuiba tangawizi lako). Wengine wamelima eka nyingi na saizi wanakuwa na pesa ya kutosha.
Mimi binafsi silimi, analima mke wangu, lakini baada ya Miaka miwili tangu alipoanza anaweza kujenga nyumba nzuri kijijini na analeta pesa ya kutosha kwa familia Dar es salaam.
Hey, please tuchambulie kidogo hii kwa kweli, inavutia niliskia sehemu juu juu, tupe hadi ghrama za kujenga bwawa.Kilimo chenye tija ni KILIMO cha samaki tu! Karibuni tulime samaki (Sato, Kambale n.k)
Mbegu; 1000kg*5000= 5,000,000/= hizo ni mbegu tu kwa heka moja
Kukodisha Shamba lake sh...?
Kulima Heka 1 sh...?
Mbolea sh ngapi....?
Heka 1 Kupalilia sh...?
Heka 1 kuvuna sh.....?
Ni mikoa gani inasitwi
Je aina hipi ya mbegu ni nzuri...?
Mtoa mada mnisaidie hapo na ingekuwa vizuri utupie namba yako ya simu.
Call me if possible whatsup 0784584871
Elewa kilicho andikwa ndo upate cha kuuliza, sio kuuliza tuu ili mradi, mana wote maswali yenu yapo kwenye maelezo, hesabu ndogo tuu ya kuzidisha, kujumlisha na kutoa, na sio mi maswaaali na kutujazia SERVER.Nataka kujua mauzo ya heka moja faida inakuwa ni sh ngapi