Kilimo cha Tangawizi - Masoko, Mbinu na Ushauri Toka kwa Wadau

Kilimo cha Tangawizi - Masoko, Mbinu na Ushauri Toka kwa Wadau

Inakaa shambani muda gani tangu kuoteshwa? Bei yake kwa gunia ni bei gani?
 
Kilimo cha Tangawizi/ Ginger Farming

UTANGULIZI
Tangawizi ni aina ya zao la kiungo ambalo sehemu inayotumika ni tunguu (rhizome). Ambao huonekana kama mizizi ya mmea. Mmea huu kitaalamu huitwa zingiber officinale.

Asili ya mmea huu sehemu za kitropiki za bara la Asia hasa nchi za china za india. Zao hili huzalishwa kwa wingi nchini Jamaica.

Hapa nchini zao hili huweza kustawi katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya Ruvuma, kigoma, Tanga, Morogoro, Pwani, Mbeya na Kilimanjaro.

MATUMIZI
Tangawizi hutumika kama kiungo katika kuongeza ladha, harufu na changamsha katika vinywaji (kama soda, juisi, vilevi n.k) na vyakula mbalimbali kama mikate, biskuti, keki, nyama za kusaga, n.k

Hutumika pia katika viwanda vinavyotengeneza madawa mbalimbali kama dawa za meno, kikohozi, tumbo na muwasho wa ngozi n.k.

KILIMO CHA TANGAWIZI SONGEA MADABA
Madaba ipo mkoa wa Ruvuma, wilaya ya Songea vijijini, ipo njiani inapotokea Njombe kwenda Songea mjini hivyo kifupi inapatikana katikati ya Njombe na Songea. Iyo huifanya Madaba kuwa na hali ya Hewa mbili ile ya Njombe na Songea. Pia Madaba ina rutuba ya kutosha kuweza kuhimiri mazao mengi ya kibiashara kama kahawa, Tangawizi, Ufuta, Soya, Ulezi n.k na ya chakula kama Mahindi, Maharage, Mpunga n.k hustawi maeneo ya Madaba .

Rejea kichwa cha habari, Tangawizi ilianzwa kulimwa Madaba kama moja ya zao la kibiashara mwaka 2013. Hivyo kuwapatia wakazi wengi wa madaba fursa hii ya kibiashara na kila mkazi asiye lima basi huwa na ndoto hii kuwa ‘’ili nitoke kimaisha basi nijitahidi nilime Tangawizi’’. Basi Tangawizi ni uti wa mgongo kwa mkazi wa Madaba.

Fursa hii pia inakujia wewe pia mwananchi wa Tanzania popote ulipo, kwa kufuata ushauri na utaalamu wa wakazi wa Madaba pia unaweza kuwa na ndoto zile zile za ‘Tangawizi mkombozi’.

Basi nami kama rafiki wa Tangawizi nimekuandalia ‘’ kiarticle’’ hiki basi ili nawe uweze kuwa rafiki ya Tangawizi pia.

TABIA YA MMEA
Kama nilivyodokeza hapo juu, mmea huu huvunwa kama Tunguu hivyo basi; hutambaa chini ya ardhi, wakati wa masika hutoa majani juu ya ardhi.

Ingawa hadi sasa kitaalamu haijasibitishwa kuwa ni aina gani ya tangawizi hulimwa hapa Madaba. Wengine husema ni white Africa (Jamaica) na wengine husema cochin (flint).Ambazo ndio maarufu hapa nchini Tanzania.

Kikubwa sio aina ya mmea bali uwezekano wa kustawi na kutoa matunda mazuri, aina hizi hutofautiana tu katika majani na ukubwa wa tunguu. Ambapo Jamaica ina rangi hafifu ya kahawia na tunguu fupi wakati cochin ina tuguu fupi zaidi lenye ngozi ya rangi iliyo kati ya kijivu na nyekundu.

HALI YA HEWA YA UDONGO
Zao hili hustawi katika maeneo yenye hali ya kitropiki, kutoka usawa wa bahari hadi mwinuko wa mita 1500 au zaidi. Huitaji mvua kiasi cha mm.1200-1800 na joto la wastani wa nyuzi za sentigradi 20-25. Hustawi vyema katika udongo tifutifu wenye rutuba na usiotuwamisha maji.

UPANDAJI
Zao la tangawizi hupandwa kwa kutumia vipande vya tunguu vyenye kichipukizi kizuri angalau kimoja na huweza kukatwa katika urefu wa sm.2.5-5. Wakati mwingine, vichipukizi vinavyopatikana katika kumenya tangawizi huweza kuhifadhiwa na kutumika kwa kupanda. Kiasi cha kilo 800-1000 cha vipande vya tunguu huweza kutumika kwa kupanda katika hekari moja.

Nafasi inayotumika kupanda ni kati ya sentimita.23-30 kwa 15-23 na kina cha sentimita.5-10 na mara nyingi hupandwa katika matuta. Baadhi ya mazao huweza kupandwa katika shamba la tangawizi ili kuweka kivuli chepesi ingawa si lazima kivuli kiwepo. Inashauriwa kumwagilia maji endapo mvua inakosekana.

Wiki 1-2 kabla ya kupanda weka mbolea ya samadi au mboji kiasi cha tani 4-8 kwa hekari na kwa kukuzia weka kiasi cha NPK kwa uwiano wa kilo 36:36:80. Tandaza nyasi shambani kuhifadhi unyevunyevu hasa pale kivuli kinapokosekana.

Palizi hufanywa mara magugu yanapoota, na kawaida ni mara nne (4) wakati huo katika palizi ya tatu na ya nne hushauliwa kupandishia udongo kwa kila china la mmea ili kuupa mmea nafasi ya kutoa tunguu kubwa na nene

Pia dawa ya kuuwa wadudu kama simazine hutumika.

MAGONJWA NA WADUDU
Madoa ya majani yanayosababishwa na viini vya magonjwa viitwavyo Colletotrichum zingiberisna Phyllosticta zingiberi.

Kuoza kwa tunguu; kunasababishwa na viini viitwavyo Pithium spp.

Mizizi fundo; inasababishwa na viini viitwavyo meloidegyne spp.

UVUNAJI
Tangawizi huweza kuwa tayari kwa kuvuna kati ya miezi 9-10 baada ya kupanda, wakati majani yake yanapogeuka rangi kuwa njano na mashina kusinyaa. Tangawizi inayohitajika kwa kuhifadhi kwenye kemikali (preserved ginger in brine) huvunwa kabla haijakomaa kabisa, wakati ile iliyokomaa kabisa huwa kali zaidi na huwa na nyuzi hivyo hufaa kwa kukausha na kusaga. Mavuno hutofautiana kulinganana na huduma ya zao, mavuno yanaweza kuwa kiasi cha tani 8-12 cha tangawizi mbichi huweza kupatikana.

USINDIKAJI
Tangawizi ikisindikwa utapata unga, mafuta maalum (essential oils) n.k. Tangawizi iliyovunwa huweza kumenywa, kukatwa na kukaushwa juani au mara nyingine huchovywa katika maji yaliyochemka kwanza na ndipo kukaushwa au hukamuliwa mafuta. Pia tangawizi husindikwa na kuhifadhiwa kwenye chupa zikiwa zimechanganywa na sukari na/au chumvi. Hata hivyo tangawizi ina Kiasi cha mafuta cha 16%-18%.

SOKO LA TANGAWIZI
Soko la Tangawizi lipo ndani na nje ya nchi, Hapa nchini huuzwa kwa bei ya Tshs. 2000 - 4000/= kutegemea msimu.

GHARAMA ZA UZALISHAJI NA MAPATO
(Gharama ya hekari moja)

Kukodi shamba Tshs.=100,000/=
Mbegu 2,,000, 000/=
Kulima 100,000/=
Kupanda 100,000/=
Kupalilia x 4 @ 90,000/= jumla = 360,000/=
Mbolea / samadi 150,000/=
Jumla 2,810,000/=

Mapato kwa hekari.

Gharama hizi hutegemea sana na msimu zinaweza shuka au kupanda zaidi.
 
Jamaaa kafika mwishoni akala kona ndo tatizo la copy and paste

Mbegu 2000, 000/=
 
Asante sn kwa Article yako nzuri. Mimi nna ndugu yangu analima Tangawizi Madaba, ila tatizo kubwa linalowakabili ni Ukosefu wa Soko na Bei ndogo ya zao hilo wakati wa Kuuza. Ningeomba nipate Ufafanuzi kutoka kwako Soko la Tangawizi lipo wapi hasa?
 
Kwa sasa changamoto kubwa imekuwa ni upatikanaji wa soko la uhakika kwa hiyo limekuwa sio zao la kumkomboa mkulima tena, hivi sasa kilo moja ya TANGAWIZI ni 1000/
 
Kilimo chenye tija ni KILIMO cha samaki tu! Karibuni tulime samaki (Sato, Kambale n.k)
 
jamaaa kafika mwishoni akala kona ndo tatizo la cpy and paste

Mbegu 2000, 000/=
Kamefika kwenye kutoa mchanganuo wa mapato kakalala mbele! Naona article kaliyokuwa kame-copy na kupaste haina mchanganuo huo!
 
Back
Top Bottom