Kilimo cha Tangawizi - Masoko, Mbinu na Ushauri Toka kwa Wadau

Kilimo cha Tangawizi - Masoko, Mbinu na Ushauri Toka kwa Wadau

Habari zenu wana JF,

Naomba kama kuna mwana JF anayejishughulisha na kilimo cha Tangawizi anipatie mawasiliano yake ili niweze kununua tangawizi nitakazo weza kutumia kama mbegu shambani kwangu. Nakaribisha mawazo mbadala kuhusu namna ya kulima na soko la zao hili ndani ya nchi yetu.

Karibuni tubadirishane uzoefu kuhusu kilimo cha zao hili.

Ahsanteni
 
Habari zenu wana JF,

Naomba kama kuna mwana JF anae jishughulisha na kilimo cha Tangawizi anipatie mawasiliano yake ili niweze kununua tangawizi nitakazo weza kutumia kama mbegu shambani kwangu. Nakaribisha mawazo mbadala kuhusu namna ya kulima na soko la zao hili ndani ya nchi yetu.

Karibuni tubadirishane uzoefu kuhusu kilimo cha zao hili.

Ahsanteni
Jaribu kwenda kwenye maduka ya pembejeo za kilimo ili upate mbegu zilizothibitishwa na wataalam.
 
Samahani member aliyeomba nimfundishe kilimo cha tangawizi najaribu kuitafuta namba yako siioni naomba unitumie tena, nisamehe kwa kweli.
 
3000 per kg
Jana nilipita Soko la Ilala ni Tsh 2000-2500,Hivyo jaribu kuangalia bei ili ujue utauzaje lakini kama kungekuwa na uwezekano kupekeleka nje ya nchi ungeuza kwa bei nzuri
 
Jana nilipita Soko la Ilala ni Tsh 2000-2500,Hivyo jaribu kuangalia bei ili ujue utauzaje lakini kama kungekuwa na uwezekano kupekeleka nje ya nchi ungeuza kwa bei nzuri
Ooh dah ningepata hiyo nafasi ingekuwa poa, nimepata soko mtwara ila wanahitaji kidogo tani 25 tuu kwa bei ya 3000
 
Ooh dah ningepata hiyo nafasi ingekuwa poa, nimepata soko mtwara ila wanahitaji kidogo tani 25 tuu kwa bei ya 3000
Naam jaribu kuulizia kwa wanaopeleka mazao nje ya nchi hasa Kenya ama Kongo waweza pata soko huko kwa siku za baadae, Kilimo kinalipa kama kukiwa na soko la uhakika!Nakutakia kila la kheri Ndugu.
 
Naam jaribu kuulizia kwa wanaopeleka mazao nje ya nchi hasa Kenya ama Kongo waweza pata soko huko kwa siku za baadae,Kilimo kinalipa kama kukiwa na soko la uhakika!Nakutakia kila la kheri Ndugu
Asante sana ndugu
 
Bei ya tangawizi imeshuka mkoani kigoma,kwa sasa kilo moja ni kati ya tzs: 500 na 800, kama utaifuata katika vijiji vya Kishanga, Kalela na Kanazi. Huu ndio wakati mzuri wa kununua mbegu kwa sababu bei itapanda siku chache zijazo kwa sababu kuna wafanyabiashara kutoka Rwanda na Kenya huwa wanaifuata vijijini.
 
Habari wana JF,

Moja kwa moja kwenye hoja. Nina mpango wa kulima tangawizi maana nimesikia kinalipa ingawa sina ABC's za kilimo hicho.

Naomba kuelewa ni jinsi kilimo hiki huendeshwa na soko la tangawizi yenyewe. Nataka kuelewa kama kilimo hiki kinawezekana maeneo ya pwani kama Mkuranga, upatikanaji wa mbegu, gharama za kulima na mapato yatokanayo na kilimo.

Ni wapi naweza kupata taarifa zaidi ya kilimo hiki?

Nikipata contacts nitashukuru.
 
Back
Top Bottom