Kilimo cha umwagiliaji kwa maji ya maziwa

Kilimo cha umwagiliaji kwa maji ya maziwa

Mfumo upi ni mzur wakumwagilia shamba lilopo sehem yenye mwinuko kutoka kwenye chanzo Cha maji either mto au ziwa?
 
Hizi ni nyavu zile zinazotumika kama shade zinawekwa juu ya nguzo mbili zinanasa umande na kuupeleka chini mfano wa matone yanakusanywa kisha upelekwa kwenye storage tank. Ni technology toka israel, wao wanamwagilia kwa umande.
Wanavuna ukungu
Aiseeeee
 
Technology ya kuvuna umande usaidia sehemu kame zenye shida ya maji. Mfano dodoma usiku ni baridi mchana joto ile baridi ya usiku ipo technology ya kuivuna kutumia hio ya net au wavu maalumu au ya kutumia mashine maalumu za mfano wa AC zinabadili hewa kuwa maji hii itasaidia vijiji vyenye shida ya maji angalau wapate hata ya kunywa na mifugo tu KWA sehemu zenye shida ya maji.
 
Pampu unayotumia hp ngapi uwezi kuvuta direct majitoka kwenye chanzo Cha maji mpka shamban bila kutumia tank?
Engine no ya kichina, ni 20hp, na water pump ni zaidi ya hp 15. Inavuta maji inch nne na kuyasukuma kwa inchi 2 ndiyo maana yaweza kwenda juu zaidi. Angalia icha hizi
 

Attachments

  • IMG_20220613_095940.jpg
    IMG_20220613_095940.jpg
    379 KB · Views: 42
  • IMG_20220704_115709.jpg
    IMG_20220704_115709.jpg
    454.7 KB · Views: 43
Hongera kwa hatua hio. Ila laiti ungejua mwanzoni ingetakiwa hio foundation ungeiweka chini kusingekuwa na 7bu ya kuiweka juu. Kwa uzoef wangu hio water pump inlet inatakiwa isiwe mbali na maji pia isiwe juu...
Ni sawa mkuu, ila miaka mitatu iliyopita maji yalijaa sana. Kuna mahali nilikuwa nmeweka mbao za kusimika mashine (maboriti makubwa ya inchi4 kwa 6) Yote yalifuknikwa na maji. Ni bahati kuwa mashine ilikuwa haijasimikwa kwenye zege, ningepata hasara kubwa. Wenyeji wananiambia hiyo inaweza kutokea baada ya miaka 50 Huo mpira unaouona kweney video ni aina ya koromeo inchi 4 ndio umeenda kwenye maji (ziwani) na umefungwa kwenye water pump (unaiona kwenye picha), Hiyo pump ndiyo inavuta maji 4 inchi na kuyapunguza hadi inchi 2 kuyasukuma kwenda juu Kama unavyoona total head 50m na suction ni 5 to8 meters
Mfumo huo ndio umeweza kusukuma maji kwenda kwenye kilele cha mita 42 baada ya kutandaza bomba la inchi 2 kwa umbali wa mzunguko wa mita 600
 
Mfumo upi ni mzur wakumwagilia shamba lilopo sehem yenye mwinuko kutoka kwenye chanzo Cha maji either mto au ziwa?
Pandisha maji kwenye huo mwinuko then jaza kwenye tank zilizo juu ya huo mwinuko. Kutoka kwenye hizo tanks waweza kutumia drip irrigation kama unataka kusave maji pia kutegemea aina ya mazao, au fanya furrow irrigation japo hii inatumia maji mengi laki ni ni rahisi kutengeneza majaruba.
Kama unatumia mashine ya diesel kuendesha water pump, gharama ya diesel ni kubwa sana. Kama una umeme, ni rahisi kidogo.
Mimi kwa kuwa sina umeme ninatumia diesel engine, Mahindi ya majaribio niliyolima kama ulivyoona kwenye video hapo juu, nilitengeneza majaruba nikawa najaza maji. Ni gharama kiasi gani nilitumia hizo nitazileta baadae
 
Mkuu, hivi ukitaka kufanya hivi ya kuchukua maji ziwani, unahitaji kibali chochote?
 
Changamoto za kilimo haziishi. Yaliyonikuta, mahindi bado yapo shambani hayajakauka kufikia kiwango cha kuvuna yamepigwa na upepo yamelala chini, yanaanza kuharibika. Sina stoo ya kuyaweka na jua la kuyaanika halipo. (Video clip imekuwa kubwa imekataa kuattach)
Bei yenyewe hivi sasa ni ndoo ya kilo 20 shs 3,000, mbolea eti ya ruzuku hakuna.
Karibuni kwenye kilimo
 
Back
Top Bottom