Habari ya mida hii wanafursa wenzangu. Nadhani vanilla sio zao geni hapa jukwaa letu wana kilimo. Nadhani kwa sasa na siku za usoni vanilla ndio zao lenye bei kubwa zaidi kwa mazao yanayolimwa hapa Tanzania. Kwa sasa vanilla mbichi iliyokomaa vizuri kilo 1inanunuliwa kati ya sh 150,000/= hadi 180,000/= kwa vanilla kavu imefikia U$D 600 zaidi ya sh 1,200,000/ kwa kilo.
Unaweza kupitia huu hmuzi uliowahi kuwekwa na mdau mmoja
Vanilla; yafika $600 kwa kg 1 ikiyapiku madini ya silver yanayouzwa $550 kwa kilo - JamiiForums
Kwa wale wenye mashamba/ ardhi ya kwao katika mikoa ya Kagera, Kilimanjaro, Mbeya, Iringa, Morogoro vijijini na baadhi ya maeneo yanayopata mvua ya kutosha zao hili linaweza kulimwa na kustawi vizuri sana.
Tunauza miche/marando marefu (kuanzia mita 2) kwa bei nzuri ukilinganisha na bei za miche yenyewe. Tunatoa elimu ya kupanda, kuhudumia shanba hadi kuvuna. Tupo Bukoba na tunatuma mkoa wowote ulipo kwa gaharama za mnunuaji. Pia tunamhakikishia soko la vanilla mkulima. Atakayenunua miche tutanunua vanilla yake yote kwa bei itakayokuwa sokoni wakati husika.
Tunaweza kuwasiliana via whatsapp au kwa kupiga via 0712016405. Usitume sms tafadhali.
Sharing is caring. Asanteni