Kilimo cha Viazi Mviringo (Viazi Ulaya) na Masoko Yake

Kilimo cha Viazi Mviringo (Viazi Ulaya) na Masoko Yake

Unajua Zogwale shamba liko Ifunda pana udongo tifutifu mweusi sijui vitazaliwa?
 
Last edited by a moderator:
Unajua Zogwale shamba liko Ifunda pana udongo tifutifu mweusi sijui vitazaliwa?

Hapo udongo ni poa kabisa kwa kuwa una mbolea na maji yanadumu kwa muda mzuri. Kichanga na mfinyazi haufai kwa viazi mviringo or tuber crops kwa ujumla wake.
 
Habari,

Nina mpango wa kulima viazi mviringo msimu ujao wa mvua, ila sina uzoefu na wala sijawahi kulima naomba kwa yoyote mwenye kujua vya zaidi kuhusu kilimo cha viazi mviringo anijuze. Nataka kulima ekari moja, labda kwa ufupi nijue ntatumia mbegu kiasi gani? Napandaje? navuna baada ya miezi mingapi?

Asanteni kwa kunisaidia.

Unata kujuzwa utaalamu vipi soko lipo wapi ndugu sababu hata me nilikuwa na mawazo kama yako naomba tusaidiane jamani.
 
Habar zenu wanaJF,

Binafsi pia nataka kulima hili zao la viaz mvringo ila nataka kujua changamoto zake sana ni zipi? So please kwa wazoefu nahitaji sana mawazo yenu kabla sijaanza zoez hili!
 
Nataka kufanya biashara ya viazi mviringo toka mbeya kwenda Dar, kwa mlio Dar, naefahamu bei kwa gunia anisaidie, Thanx.
 
Habari zenu wanaJF,

Naombeni msaada kama kuna mtu ana namba za dalali wa mazao na vyakula vingine anaepatikana Zanzibar.
 
Naombeni kujua garama za kilimo cha viazi ulaya ukilima hekari moja. Msaada juu ya:
  • Mbegu
  • Madawa
  • Kulima
Na mengine nisiyoyajua asanteni sana, location ni Lushoto.
 
Mkuu mimi niliwahi kulima viazi ulaya mwaka juzi Eneo lilikuwa ekari Mbili,Ktk Kilimo hiki inategemea sana Nature ya Udongo wa eneo husika. Mimi nililima Njombe,Kwa kawaida Mbegu huwa ni kati ya gunia 5-7,kwa eneo la ekari moja, Mbolea ya kupandia hutumika DAP au NPK, na kukuzia ni UREA au CAN au SA, Madawa yanayotumika kwenye Viazi yapo ya Aina mbili; Dawa za Ukungu na dawa za kuua wadudu waharibifu,Dawa za Ukungu ni km vile Ridomil,Glider,Linkonil,n.k.Na dawa za kuua wadudu waharibifu ni km vile Wilcron, Banofos, Mocron, nk. Kulima kunaanza mapema kabisa kabla ya mvua za mwanzo,na ni vema Mvua ya kwanza inaposhuka kiazi kiwe tayari kimepandwa shambani.
 
Mkuu tafadhali tupe somo vizuri kuhusu hiki kilimo.
 
Mkuu mimi niliwahi kulima viazi ulaya mwaka juzi Eneo lilikuwa ekari Mbili,Ktk Kilimo hiki inategemea sana Nature ya Udongo wa eneo husika,Mimi nililima Njombe,Kwa kawaida Mbegu huwa ni kati ya gunia 5-7, kwa eneo la ekari moja,Mbolea ya kupandia hutumika DAP au NPK, na kukuzia ni UREA au CAN au SA,Madawa yanayotumika kwenye Viazi yapo ya Aina mbili; Dawa za Ukungu na dawa za kuua wadudu waharibifu, Dawa za Ukungu ni km vile Ridomil, Glider, Linkonil, n.k.Na dawa za kuua wadudu waharibifu ni km vile Wilcron, Banofos, Mocron, nk.Kulima kunaanza mapema kabisa kabla ya mvua za mwanzo,na ni vema Mvua ya kwanza inaposhuka kiazi kiwe tayari kimepandwa shambani.
Salama mkuu, faida ipo katika hiki kilimo?
 
Nimesomea uganda eneo linaitwa bukinda in kabare district. Hii sehemu wanalima sana viazi ulaya. Sisi pia kama wanafunzi wa seminary tulikuwa tukilima hivyo viazi. Yani kwa kule viazi vinalimwa bila mbolea wala dawa yoyote na mavuno nimakubwa ile mbaya.

Leo nimepitia humu jamvini nimeshangaa kuona kuwa et sikuizi viazi vinalimwa na Urea sijui CAN, sijui dawa ya ukungu. Mara wadudu?

Swali langu ni kwamba hivi hii arth ya TZ inatatizo gani?
 
panda vile vya kwenye mifuko ndo vinatoka vingi kuliko vya shambani.

Vizuri ukaenda mbeya ukatembelee wakulima wakupe semina hapa naona mabwanashamba huwa hawapiti.
Tuelekeze hivo vya mifuko
 
UTANGULIZI
Viazi mviringo ni zao muhimu la chakula na biashara katika nchi nyingi zilizoendelea na zinazoendelea. Viazi husitawi vizuri sehemu za miinuko, kati ya meta 1300 na 2700 juu ya usawa wa bahari. Hukomaa katika kipindi cha miezi mitatu hadi mitano. Viazi mviringo vina asilimia kubwa ya chakula chenye asili ya wanga. Pia vina kiasi cha kutosha cha protini, madini, vitamini na maji.

Mbegu bora za viazi: Zinatakiwa kuwa na sifa zifuatazo

· Zenye kutoa mazao mengi zaidi kutoka kwenye shina moja
· Ziwe zimechipua vizuri na ziwe na machipukizi mengi (zaidi ya manne)
· Zisiwe na wadudu au magonjwa
· Zitoke kwenye aina ambayo haishambuliwi na magonjwa kama vile ugonjwa wa ukungu na ugonjwa wa mnyauko bakteria
· Zenye ukubwa wa wastani (yaani zisiwe ndogo au kubwa sana) unaolingana na ukubwa wa yai la kuku wa kienyeji

Aina bora za viazi
Taasisi ya Utafiti wa Kilimo uyole, mpaka sasa imetoa aina sita za mbegu bora za viazi mviringo nazo ni : Baraka, Sasamua, Tana, Subira (EAI 2329), Bulongwa [(K59a (26)], Kikondo (CIP 720050)

Muda wa kupanda viazi: August hadi Septemba na Novemba hadi Decemba

Kupanda
Tumia sentimeta 60 (futi 2) hadi 75 (futi 2.5) kutoka mstari hadi mstari, nafasi kati ya kiazi na kiazi iwe sentimeta 30

Mbolea
Ili kupata mazao mengi kutoka shambani mkulima anashauriwa kutumia mbolea, aina ya samadi, mboji, majani mabichi na za viwandani (au za chumvi chumvi).

Kwa mbolea za viwandani tumia: Kilo 300 (au mifuko 6) ya mbolea ya TSP kwa hekta moja, na kilo 300 (mifuko 6) za mbolea ya CAN au kilo 400 (mifuko 8) ya SA au kilo 175 (mifuko 3.5) za Urea.

Palizi: Palilia viazi wiki mbili au tatu baada ya kuchomoza. Inulia udongo ili kufanya tuta zuri ili pawepo na unyevu wa kutosha na kufunika viazi kutokana na mwanga wa jua.

Magonjwa na wadudu waharibifu: Ili kuzuia ugonjwa wa ukungu tumia Ridomil. Changanya gramu 100 za dawa ya Ridomil katika lita 20 za maji, na nyunyizia mara baada ya viazi kuchomoza na baadaye kila baada ya wiki mbili au tatu kutegemea na hali ya hewa. Nyunyizia dawa kama Karate kiasi cha mililita 20 mpaka 40 za dawa katika lita 20 za maji ili kuzuia wadudu kama inzi weupe na wengineo. Tumia mbinu bora za kilimo kama usafi wa shamba au kilimo mzunguko kama mbinu shirikishi katika kuzuia magonjwa na wadudu.

Kuvuna na mavuno: Viazi huwa tayari kuvunwa baada ya miezi 3 hadi 5 kutoka kupanda. Muda wa kuvuna utategemea madhumuni ya zao na aina iliyopandwa. Usiache viazi shambani bila kuvifunika (kwa nyasi au udongo) kwa muda mrefu kwa sababu zifuatazo:

· Viazi vikipigwa na jua hubadilika rangi na kuwa na rangi ya kijani ambayo inavifanya visifae kwa chakula.
· Wadudu kama vile nondo hutaga mayai juu yake, yanapoanguliwa viwavi hutoboa na kuingia ndani ya viazi na kuviharibu
· Iwapo vitanyeshewa na mvua vitaharibika wakati wa kuvihifadhi ghalani.

Aina bora kama Kikondo yaweza kutoa gunia 70 hadi 100 kwa ekari ikilimwa na kutunzwa vizuri.

Kuhifadhi: Viazi vya chakula vihifadhiwe kwenye ghala yenye hewa ya kutosha, pasiwe na unyevu, joto kali. Unapohifadhi viazi vya mbegu, aina mbalimbali zitengwe kwa kutumia vichanja au masanduku (maalum ya kuhifadhia) tofauti.

Shukrani za dhati kwa mtaalamu wa Kilimo mifugo na mazingira&Mratibu wa program ya CHEMA jimbo katoliki la Rulenge-Ngara padre Anthony Ndikumulimo na Mtaalam Jonas B..Kizima kutoka Chuo Kikuu cha SOKOINE SUA.
 
Back
Top Bottom