Kilimo cha Viazi Mviringo (Viazi Ulaya) na Masoko Yake

Kilimo cha Viazi Mviringo (Viazi Ulaya) na Masoko Yake

Wadau nahitaji kulima viazi mviringo maeneo ya mbeya au njombe hivyo naomba mwenye information zitakazoweza kunisaidia anijuze kwani sijawahi kulima hata Mara moja.
 
Nimesomea uganda eneo linaitwa bukinda in kabare district. Hii sehemu wanalima sana viazi ulaya. Sisi pia kama wanafunzi wa seminary tulikuwa tukilima hivyo viazi. Yani kwa kule viazi vinalimwa bila mbolea wala dawa yoyote na mavuno nimakubwa ile mbaya. Leo nimepitia humu jamvini nimeshangaa kuona kuwa et sikuizi viazi vinalimwa na Urea sijui CAN, sijui dawa ya ukungu. Mara wadudu?

Swali langu ni kwamba hivi hii arth ya TZ inatatizo gani?
Rutuba imeisha na pia mabadiliko ya sura ya nchi. Jua pia Ug hutumia sana mazao yenye GMO.
 
Habari zenu wanajamii,naomba ushauri wenu mimi nina heka mbili ambazo zimepitiwa na maji ya jirani yangu aliyepitisha bomba la maji kati kati ya shamba langu na kufanya hekari moja kuwa chini na nyingine kuwa juu,sasa nataka kufanya kilimo cha umwagiliaji na nilitamani sana kutumia mipira ya dripping pamoja na kuweka tenki ila mtaji wangu ni mdogo sasa nilikuwa nafikiria ninunue pampu ya MONEY MAKER kwa ajiri ya kuweka kibarua amwagilie sasa najiuliza je hizi pampu zinafanya vizuri kwenye mazingira kama hayo ukizingatia ndo naanza kilimo?
 
Hivi mbegu za viazi mviringo Dar es Salaam vinapatikana?
 
Ndio,pumpu za money maker ni bora na ni sahihi kwa matumiz ya bustani,pump hz zinauwezo mkubwa wa kuvuta maji na kusafirisha maji umbali merefu zaid
Nashukuru,kiongozi ila nilitaka kujua kama naweza ku-connect zile springer kama sita kwenye bomba moja sijui kama itafanya kazi,tatizo sijapata mtu mwenye nayo kuweza kujaribu kama inaweza kunifaa au la kwa huku kwetu.
 
Kwa Dar sijajua maana mimi niko nje ya huo mji, ila nahisi kupatikana inawezekana sema gharama itakuwa juu.
Huko ulipo mbegu zinapatikana kwa bei gani? Natafuta kiasi tuu za kujaribu kupanda hapa Dar.
 
Nilipanda Tigo ekali moja gunia tano baada ya miez minne nilivuna gunia 48
Mi bado natatizwa na gunia la viazi,hivi huwa na debe ngapi? Na pia naomba kusaidiwa mbolea unatumia mifuko mingapi kwenye kupandia?

Asante
 
Kilimo cha viazi kusini i.e Njombe, kwa eka moja
  • Kukodi 100000-150000
  • Kulima-Elfu 50
  • Mbolea elfu 50-70 (inategemeana aina ya mbolea na umenunua lini)
  • na si chini ya mifuko miwili ya kupandia
  • Mbegu gunia 7@elfu 40-50 or above
  • Mbolea ya kukuzia elfu 60 or above mara mifuko 3
  • Madawa ya ya ukungu, fanya elfu 40
  • Hela ya palizi elfu 50
  • Mengineyo 100000
Masoko yapo hasa kwa mwaka huu gunia la debe 6 lilifika 60 kwa sasa sipo sijui ni shingapi.

Changamoto kubwa ni ardhi iliyochoka na mabadiriko ya tabia ya nchi ambayo hupelekea viazi kutoota vizuri, ila ukipanda wakati mvua zimeanza kunyesha una uhakika wa kuvuna.

Mavuno inategemeana kama ulizingatia vigezo; lakini ni kati ya gunia 20-60 au zaidi za debe 6.
 
Kilimo cha viazi kusini i.e Njombe :
Kwa eka moja,
Kukodi 100000-150000
Kulima-Elfu 50
Mbolea elfu 50-70 (inategemeana aina ya mbolea na umenunua lini)
na si chini ya mifuko miwili ya kupandia
Mbegu gunia 7@elfu 40-50 or above
Mbolea ya kukuzia elfu 60 or above mara mifuko 3
Madawa ya ya ukungu,fanya elfu 40
Hela ya palizi elfu 50
Mengineyo 100000
Masoko yapo hasa kwa mwaka huu gunia la debe 6 lilifika 60 kwa sasa sipo sijui ni shingapi.
Changamoto kubwa ni ardhi iliyochoka na mabadiriko ya tabia ya nchi ambayo hupelekea viazi kutoota vizuri,ila ukipanda wakati mvua zimeanza kunyesha una uhakika wa kuvuna.
Mavuno inategemeana kama ulizingatia vigezo;lakini ni kati ya gunia 20-60 au zaidi za debe 6
Mkuu naomba unijuze mfano nikivuna viazi na kuvihifadhi vinaweza kukaa mda gani pasipo kuharibika?
 
Kilimo cha viazi kusini i.e Njombe :
Kwa eka moja,
Kukodi 100000-150000
Kulima-Elfu 50
Mbolea elfu 50-70 (inategemeana aina ya mbolea na umenunua lini)
na si chini ya mifuko miwili ya kupandia
Mbegu gunia 7@elfu 40-50 or above
Mbolea ya kukuzia elfu 60 or above mara mifuko 3
Madawa ya ya ukungu,fanya elfu 40
Hela ya palizi elfu 50
Mengineyo 100000
Masoko yapo hasa kwa mwaka huu gunia la debe 6 lilifika 60 kwa sasa sipo sijui ni shingapi.
Changamoto kubwa ni ardhi iliyochoka na mabadiriko ya tabia ya nchi ambayo hupelekea viazi kutoota vizuri,ila ukipanda wakati mvua zimeanza kunyesha una uhakika wa kuvuna.
Mavuno inategemeana kama ulizingatia vigezo;lakini ni kati ya gunia 20-60 au zaidi za debe 6
Mwaka jana nililima huko Njombe hivyo viazi ila mwisho wa siku nimetapeliwa na aliyekuwa msimamizi maana nilikuwa bize sana
Nilitumia zaidi ya M12 lakini sijavuna hata mia, njombe matapeli sana aiseeh
 
Back
Top Bottom