Mkuu nataka kopo 10 kwanza za kujaribu. But nimekutumia meseji kwenye simu haijafika, ile namba pale juu ni sahihi?
Water pump nakushauri utafute zile za kusukwa na mafundi, huwa zinauzwa kuanzia laki 9 ila huwa ni imara na inavuta maji mengi sana, ndan ya saa moja unakua ushamwagia eneo la ekari moja. Ila hizi za madukan za laki 3 hazifai kwa kilimo serious.mkuu ninampango wakununua water pup,ila sijajua ipi ni bora na kwa garama ipi?kwa shamba la hekari 1-2.pia vipi maji yakisima chakuchimba yanaweza yakafaa..naomb unisaidie kaka.
Mbegu kwa sasa me nimeishiwa, ntaanza kuuza tena mwezi wa 11. Namba hiyo ni sahihi ila ukiona sipatikan nakua niko shamban kidogo mtandao unasumbua.
Nimekutumia pia email baada ya kuona SMS haiingii.
Pili msimu wa kilimo cha vitunguu ni kuanzia mwezi gani? Maana Nilitaka nifanye the soonest it could be.
Kwa sasa umelate kaka manake tayari watu wako mashamban ma mazao wanakaribia kuanza kuvuna. Msimu mzuri ni wa kumwaga mbegu mwezi wa 3 na kuvuna wa 7
Water pump nakushauri utafute zile za kusukwa na mafundi, huwa zinauzwa kuanzia laki 9 ila huwa ni imara na inavuta maji mengi sana, ndan ya saa moja unakua ushamwagia eneo la ekari moja. Ila hizi za madukan za laki 3 hazifai kwa kilimo serious.
Nakushukuru kaka..naomba uniongeze ninakoweza kuzipata.mi niko Mbeya..samahan kw usumbufu mkuu.
Ahsante sana Mkuu,
Sababu nataka kulima mwaka mzima (mzunguko), kwa sasa ni kilimo gani ndio kinaanza?
Pia una mbegu za kitunguu tu?
Huna za mazao mengine?
Ungekua uko dar ingekua rahisi kwangu kukuelekeza, ila hakuna shida nenda hata SIDO hapo mbeya watakusaidia. Unawaambia unataka pump ya inch nne na inayotumia diesel. Manake kama wananchi wanaweza isuka basi kwa sido sio tatizo kabisa.
Poa Mkuu,Mimi najihusisha na kilimo cha vitunguu, ufugaji wa nyuki wa kisasa na nyanya F1 tu. Msaada wangu mbadala ntakupa kwa hayo mazingira mengine.
Salama mkuu, huwa navuna miezi hiyo pia ila huwa ni maalumu kwa storage na sio kuuza manake bei yake huwa ndogo sana, kwa shamba huwa gunia linarange 45 - 55. Me vitunguu vya biashara huwa napanda mwezi wa tatu na kuvuna wasaba katikati.
Ukivuna mwezi wa 10 unaweza kuvi-store hadi mwezi wa ngapi kwenye bei? Mwezi wa saba ndo bei huwa nzuri zaidi? Nimeona mwezi wa 4 Kariakoo gunia lilikuwa linauzwa Kwa 160,000.
kitunguu kinataka mazingira ya aina gani nina shamba kubwa "marangu" na mto unaopita pembeni je mkoa huu wa kilimanjaro vitunguu vinaweza kustawi?
unajua lolote kuhusu vitunguu saumu?
Kwa bahati mbaya najihusisha na vitunguu maji tu.
Habari ndugu zangu,
Kwa jina naitwa Joseph ni mkulima na mfanyabiashara wa vitunguu. Kitunguu ni zao lenye manufaa makubwa na kipato cha hali ya juu endapo tu utafuata maelekezo ya mtaalamu.
Dhumuni langu hapa ni kuwaletea mbegu bora kabisa za vitunguu (Red Bombay) ambazo hukupa mavuno mazuri na yenye kipato kikubwa sana.
Bei ya mbegu hizi ni tsh 30,000/= kwa kopo la lita moja(1) na tsh 600,000/= kwa ndoo ya lita ishirini.
Guarantee: Ndoo ya lita 20 ambayo ni sawa na makopo 20 ya lita moja inatosha kupanda eneo la hekari 1 (m70*m70) na kiwango cha chini cha mavuno ni gunia 100 na kiwango cha juu ni gunia 110-120 ndani ya siku 90 (3 months) toka kupanda. Gunia moja sokoni kariakoo, ilala, buguruni, temeke na mabibo kwa sasa bei ni tsh 130,000/= * gunia 100 = tshs 13,000,000/= ndani ya miezi 3.
Kama utakua na swali lolote au kutaka kujua zaidi usisite kunitafuta kwa namba zangu za simu +255655003510 au e-mail address: josephkadendulah@gmail.com
Ahsanteni sana na karibuni tujenge maisha bora kwa kila mtanzani.