King kingo
JF-Expert Member
- Sep 6, 2010
- 401
- 26
Sisi mabepari utatuweza lakini? Au unasema !!!!!!!
Kama unataka kwenda Ruaha Mbuyuni kwa ajili ya kitunguu nenda,ukiweza nenda Kibakwe Mpwapwa pia kuna bonde zuri sana na wanalima pia kibiashara. Nenda Mbeya vijijini kuna kitunguu cha kufa mtu au kajichanganye Karatu( Mang`ola),
Maeneo hayo bei ziko juu, kama hutajali nenda kafanye survey bonde moja huko Kipatimu, watu wanalima vitunguu pia,huko bei ya ardhi inaweza kuwa karibu na bure.
Shime nenda shambani leo usingoje kesho.
Sisi mabepari utatuweza lakini? Au unasema!
Kama unataka kwenda Ruaha Mbuyuni kwa ajili ya kitunguu nenda,ukiweza nenda Kibakwe Mpwapwa pia kuna bonde zuri sana na wanalima pia kibiashara. Nenda Mbeya vijijini kuna kitunguu cha kufa mtu au kajichanganye Karatu( Mang`ola),
Maeneo hayo bei ziko juu,kama hutajali nenda kafanye survey bonde moja huko Kipatimu, watu wanalima vitunguu pia, huko bei ya ardhi inaweza kuwa karibu na bure.
Shime nenda shambani leo usingoje kesho.
Kipatimu ipo wilaya ya Kilwa,ukitoka Dsm kwenda Lindi,unaweza kuingilia Somanga au Njia Nne na ukiwa usafiri wako unaweza toka Dsm asubuhi na jioni uko Dsm bila taabu.
Nimejikita apo Mahenge na kilimo cha kitunguu. Tena last week tuu kuna mtu alikuwa anauza shamba maeneo ya ruaha mbyuni. Unaweza nipm tukabadilishana mawazo
Mkuu nikitaka kufika huko nafikaje Kilosa npafahamu na nimeshawahi kufika ila huiko mwega/malolo ndio sipajui nipe direction mkuuCheck mwega/malolo-kilosa district kuna skimu ya umwagiliaji kule kitunguu inakubali saaana.mpaka mwezi wa nane 2010. Kitunguu gunia moja likiwa kijijini mwega 120,000-150,000.
Hayo ni moja ya maeneo yangu ya kazi
ni km ngapi kutoka bandari iliyo salama mpaka kipatimo,labda tunaweza tia miguu mafuta tukaja wekeza
Check mwega/malolo-kilosa district kuna skimu ya umwagiliaji kule kitunguu inakubali saaana.mpaka mwezi wa nane 2010. Kitunguu gunia moja likiwa kijijini mwega 120,000-150,000
hayo ni moja ya maeneo yangu ya kazi
Mkuu kuna eneo lina maji mengi sana yasiyo kauka na kijito kizuri, unaweza kulima kilimo cha umwagiliaji. Eneo hili lipo km 75 toka Dsm njia ya Mkuranga. Udongo ni mzuri na barabara ipo. Eneo hilo linafaa pia kwa mifugo mbalimbali.Nashukuru sana kwa taarifa kama hii.
Ekari moja wanakodisha au wanauza kwa bei gani?
Gharama za kulima, kutunza shamba la ekari moja hadi kuvuna ni sh. ngapi?
Ekari moja inatoa gunia ngapi?
Naweza kupata eneo zuri lenye maji yasiyokauka nilime kilimo cha umwagiliaji kwa mashine ya kuvta maji?
Contacts zangu ni: 0767 919923, 0784 593005, 0716 889705, richkety@yahoo.co.uk
Wakuu ; baada ya tukio la ajali kesi yangu ilipangiwa wilayani Kilosa; na hivyo nililazimika kusafiri hadi mjini Kilosa, naweza kusema safari yangu ya Kilosa was a blessing in disguise, njiani nimekutana na mabonde mengi sana na mambwawa kedede yaliyojaa maji mapaka sasa pia ardhi nzuri kwa kilimo cha nyanaya na vitunguu na hasa katika vijiji vya Kilangali na Lyamuhaa (Kama sijakosea jina). Natafuta wasaa wa kwenda tena Kilosa na kama kuna mdau analifahau vizuri eneo hilo atujuze zaidi.
Kwanza pole kwa ajali mkuu,
Nilibanwa hadi nikasahau kuuliza habari za afya yako tangu siku ile. Kuna jamaa yangu ana makazi huko Kilosa,nitajaribu kumchimba ili asaidie ni maeneo gani sugu kwa mafuriko, ugomvi kt ya wafugaji na wakulima, na yepi yamechukuliwa na wakubwa. Akinipa jibu nitakupasha ili usiingie matatizoni. Ila safari ya Iringa ilikuwa na matunda kwangu na wenzangu.
Asante!
Nasikitika kuwa ajali ilinizuia nisijiunge nanyi huko Iringa; Mungu atatupatia wasaa mwingine tena! Namalizia kujipanga ili nirudi mstari wa mbele