Kilimo cha vitunguu (saumu na maji): Ushauri na Masoko


Aisee! Kumbe! Jamaa mwezi wa nne wamelamba pesa nzuri sana Dar, 160,000/= Kwa gunia. Ukiwa na magunia 300 Kwa ekari 4 hapo unakuwa milionea ghafla.
 

mapinga kitunguu kinastawi?
 
Mkubwa nina maswali mengi?....Tokea uanze kushughulika na kilimo cha vitunguu ni changamoto gani umekua ukipata katika biashara hiyo???

Changamoto zipo nyingi ila kubwa zaidi ni wafanyakazi na kwa sokoni mwanzoni utapata shida ya madalali wasiowaaminifu.
 
Aisee! Kumbe! Jamaa mwezi wa nne wamelamba pesa nzuri sana Dar, 160,000/= Kwa gunia. Ukiwa na magunia 300 Kwa ekari 4 hapo unakuwa milionea ghafla.

Ni kweli kitunguu cha msimu kina pesa nzuri sana. Ila pia kinahitaji umakini manake kuna misimu huwa mambo yanageuka. Mfano msimu wa mwaka juzi hadi mwezi wa 3 unafika bei ziligoma kupanda zaidi zikawa zinashuka. Kwahiyo umakini unahitajika
 
Sehemu ya shamba nnayotarajia kuanza kuvuna mwezi wa saba. Hapo vitunguu vilikua na umri wa week tatu tokea kupandikizwa. Nawashauri kutumia mbegu bora ili kupanda matokeo mazuri.
 
Ndg Madiba na Ndg Mossa naombeni msaada wa namba zenu maana nimeguswa sana na fursa hii.
please call me or text me via 0765824897 au 0655123413 or email me via ngalipamdogo1988@gmail.com
 
kwahiyo bwana Joseph hicho kilimo unafanyia dar au mikoan? nitakupm
 
Hii ndo gold ya mkulima, ila niko na maswali machache. Umeelezea vizuri ila hukufafanua/hukutoa mchepuo wote, yaani garama ya mbegu, garama za kutayalisha shamba na utunzaji wa shamba hadi kufikia kuvuna
sasa naomba utupe ufafanuzi ukizingatia point nilizoweka hapo juu
Shukrani
 
Natamani ningeweza kuweka maelezo yote hapa ila ni ngumu manake kuna vitu vingine ni rahisi kumuelezea mtu mkiwa face to face, pale nilijaribu tu kuweka kiasi cha pesa ambacho unatakiwa kukitumia kuhudumia acre 1 ambacho jumla ya gharama ni kama 2.5M ambayo inaweza kuzidi au kupungua kutokana na usimamizi wako wa shamba. Natumai nimejaribu kujibu swali lako kaka
 
Ni mawazo mazuri kwa wote waliotoa, pongezi kwako mtoa mada na mlio changia, mhesima katoa ufafanuzi mfupi wa mbegu, ila kwenye kilimo kuna zaidi ya mbegu, hivyo kwa kuwa yeye ni mkulima mzoefu wa zao hili katoa mawasiliano yake pale, barua pepe na kilongalonga hivyo ukimtafuta auatapa maelekezo yote na kama una swali unamuuliza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…