Kilimo cha vitunguu (saumu na maji): Ushauri na Masoko

Nitakupa tips chache ninazozifahamu mkuu
Kitunguu kinahitaji maji mengi wakati wa kustawi but kinapoanza kukomaa hakihitaji maji mengi. Wakati wa kuvuna kitunguu hakitakiwi kigusane na maji kikigusana kitaoza

Sasa bas sijui mkoa ulipo na mvua za masika zinaanza mwez gani
Ila ukivivusha mkuu vitakutoa maana bei yake kati sh 120000 ~180000 kulingana na eneo uliko

Mimi nategemea kupanda next week
 

Ebana shukrani asee! Soko zuri nasikia lipo dec mpka april hivi..ww unalima mkoa gn mkuu?
 
Bei imeshashuka saiv kila mtu analima.

Gunia elf 40 now full hasara.
 
Ndg. Wakulima wenzangu
Ni vema muelewe kuwa mazao ya bustan huwa yana msimu wake. Ukitaka bei nzur ya vitunguu ni mwez december~ may hapo lazima ukutane na tsh 120000/= -180000 wakat mwingine hufika 200000.

Changamoto ni moja kipindi cha dec-may huwa ni masika vitunguu huathiriwa na mvua. Na ndio huwa bei juu
 
Mkuu byakuzana huu ndio muda muafaka kwa kilimo cha kitunguu binafsi Niko kwenye maandalizi mbegu iko tayari kitunguu cha mwezi huu kawaida kinatoka mwakani mwezi Wa kwanza majira hayo sokoni hakuna kitunguu bei iko juu kikitoka vizuri lazima ucheke Mkuu zingatia matunzo dawa Na mbolea
 
@ byakuzana sawa mkuu
We piga kaz usijali. Mambo mengine nicheki pm
 
Mm nalima mwanza eka moja ardhi yake ni kama mbuga hv nishaurin ardhi hii inafaa kwa vitunguu? Mm ni mara ya kwanza kujiingiza katika kilimo
 
Misimu inatofautiana kutokana na maeneo.

Mfano kwa Ruaha msimu unaanza March hadi july. Sasa wewe anza kulima kuanzia september hadi february japo ni risky.
Ni risk zipi unazipata uanzapo kulima miezi ya September hadi february? Je unafanyaje kukabiliana na hizo risk
 
Naomba mnijuze ipi mbegu iliyo bora yavitunguu katika kupanda wakuu, naje mwezi huu wa 9 ninaweza anza kuandaa kitalu kwajili ya kusia mbegu .naomben mawazo yenu
 
Ni risk zipi unazipata uanzapo kulima miezi ya September hadi february? Je unafanyaje kukabiliana na hizo risk

January na February ni muda ambao mvua zinaanza. Na kitunguu hakitaki maji wakati wa kuvuna.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…