Inategemea na unapopanda lakini gharama zake sio chini ya 2,700,000/= kuanzia kukodi shamba hadi kuvuna kwa Ruaha Iringa. Mauzo yake hutegemea sana upatikanaji wa vitunguu kwenye soko.
Ukiwezakuvuna na kuuza mwenyewe rejareja bei inaanzia 100/= kwa kilo kama utauzia shambani bei inaanzia 50,000/= hadi 230,000/= kutegemea na uwingi wake sokoni. Mavuno inategemea na matunzo yako na vita ulivyopambana na wadudu waharibifu pia "imani yako" na mbegu uliyotumia. Kifupi ni biashara inayohitaji kujidhatiti hasa kwa kuwa na ufahamu wa kila kitu na usimamizi mzuri kuanzia mwanzo hadi siku unafikisha sokoni mzigo maana risk zipo nyingi.
Kuna wanaofanikiwa hasa pale utakapoweza kucheza vizuri timing ya mvua na forces za demand and supply, pia usikutane na pembejeo feki