Kilimo cha vitunguu (saumu na maji): Ushauri na Masoko


Heka ngapi hiyo??? Unapata gunia ngapi??
 
Na pia kujua nimikoa ip inafaa haswa kwa kilimo vha vitunguu. Au ni ardh yeyote inafaa? Almrad pawepo na maji au mvua?
Kitunguu kinataka udingo usiotuamisha maji, ukiwa na ardhi yenye sifa hiyo na mtaro wa maji ukiwepo basi we lima subiri mavuno. Niliwahi lima nchi kavu uwanjani kwa maji ya bomba kama nusu eka hivi nikavuna gunia 32 na ukizingatia wezi nao walikuwa wakinyofoa usiku na kupika mitaani huko
 
jamani wadau mnisaidie nataka kuanza kilimo lakini nina laki tano tu nipo kilosa sina mwanga wa kilimo nataka nifanye kilimo cha mpunga ushauri wenu
 
jua linapiga ila tunakomaa kimtindo maana hakuna namna nyinigine. hapo kitunguu hiki nimekiacha muda kama wiki mbili hivi lakini kijana wangu wa shamba ananiambia boss hali ni nzuri tuu haina shida. nimerudi kuangalia tayar kuna tatzo. usilime kwa simu hata kidogoo shiriki shambani kikamilifuuu
 
Kwa huku kwetu Singida ni ka ifuayo
1. Mbegu lt 10 sawa na 125000/-
2.kulima kwa trekta 40000/-
3.kukodi shamba kama sio lako 60000/-
4.kung'olea majani mara 2 sawa na 60000/-

Jumla inawezafika laki 3
Naomba unitafutie hekari 5 kiongozi.
 
Mwenye uelewa kuhusiana na kilimo cha vitunguu maji,kwa heka moja inatoa gunia ngapi na huduma za mbolea na dawa kwa heka inacost vpi
 
Wivu nini kimekuleta hukuu
 
mkuu samahani ila mimi nahisi huyu bwana ni muongo na maetudanganya ndio maana ameshindwa kujibu maswali yenu kitaalamu. huwez lima kitunguu ukamuachia kijana. hilo ni ziroo kabisaa. nakijua saana kitunguu both maji na saumu. jamaa awaeleze vizur maana kuna maandalizi kibao saana kuanzia kitaluni mpaka shambani.

anya way nikirudi kwaako, siku hizi tunatumia mbegu zilizoboreshwa {F1} na mbegu hizi ndio maana zinatuhitaji kutumia mbolea za dukani pamoja na madawa yaake. hiii itatusaidia kupata maximu profit. siku nikipata muda nitawaeleza kiundani zaid kuhusu vitunguuu saum na vitunguu maji
 
Salama mkuu?? Sorry kwa kuchelewa kukujibu
Ukweli ni kwamba mbolea za asili( samadi ya kuku,ng' ombe, mbuzi, kitimoto n.k) ni nzuri sana ila tatizo ni slowly nutrient relizer,yaani zinachelewa sana kuachia virutubisho.Hivyo kunawakati unaweza zitumia kupandia mazao ya muda mfupi kama mchicha/ chinese, unaweza ona miche isiwe na afya njema. Pia mbolea za asili zinafanya kazi kwa muda mrefu lakini taratibu.Mbolea za asili pia husaidia sana kushikamanisha udongo ( Improve soil structure). Mbolea za viwandani,zinafanya kazi haraka sanaa,na unaona matokeo baada ya muda mfupi, tatizo lake ,Hazidumu kwa muda mrefu,na baadhi yake kama SA- Sulphate of Ammonia, huongeza asidi katika udongo.Kwa hiyo mara nyingi nashauri kama shamba ni lako,ni vyema ukaweka samadi mapema shambani hata 3 months kabla ya kupanda ili ioze kabisa,lakini siku ya kupanda tumia na za viwandani kama DAP,YARA MILA WINNER, NPK etc, kisha ktka kukuzia endelea kutumia za viwandani pia,coz zenyewe ziko fasta sana katika ufanyaji kazi. LAKINI tunashauri sana kupandia samadi kwa mazao yanayokaa muda mrefu sana ardhini kama vile korosho,chai,kahawa,migomba,cocoa,miembe etc, coz miche huchukua muda mrefu kuzaa na itakaa sana. Kama shamba si lako ( kukodi) ukitumia samadi, ni kwamba unamwachia faida mwenyeshamba maana wewe utavuna,wakati ardhi bado iko na rutuba.
 


Ni salama kabisa ndugu, sijuwi upande wako. Ahsante mkuu kilimomaarifa.tajiri

Kutokana na huo muongozo wako, basi nitafanya hivi: nitapandia samadi ya kuku. Then nitakuzia CAN (CAN nitaiweka maua yakianza). Nikishaanza mavuno baada ya week mbili hivi naweka tena samadi ya kuku as final fertilizer.

Vipi mkuu, hapo nipo sahihi? Zao husika ni Bamia (mbegu: royal).

Pili, naomba contact za kampuni inayoaminika kuuza MBEGU original, kwa maeneo ya Dar.

-Kaveli-
 
Kaveli

NIKO SALAMA KIONGOZI

Kutokana na huo muongozo wako, basi nitafanya hivi: nitapandia samadi ya kuku. Then nitakuzia CAN (CAN nitaiweka maua yakianza). Nikishaanza mavuno baada ya week mbili hivi naweka tena samadi ya kuku as final fertilizer.

Vipi mkuu, hapo nipo sahihi? Zao husika ni Bamia (mbegu: royal).=KIONGOZI SAMADI YA KUKU NI NZURI SANA, KWA MAANA INA NITROGEN (N) KWA WINGI SANA-HUKUZA MIMEA HARAKA, PIA SAMADI YA KUKU INASAIDIA KUIMARISHA UDONGO (WATER HOLDING CAPACITY/SOIL STRUCTURE IMPROVEMENT). LAKINI INAUPUNGUFU MKUBWA WA PHOSPHORUS (P) YA KUSAIDIA KUTENGEZA MIZIZI, LAKINI PIA MORE WORSE YA SAMADI YA KUKU, NI MBOLEA YENYE JOTO SANA, NA MARA NYINGI USIPOKUWA MAKINI HUWA INAUNGUZA SANA MAZAO KWA SABABU YA JOTO (BURN).

CHA KUFANYA KAMA UTAPENDA KUITUMIA ANDAA SHAMBA, WEKA MASHIMO DISTANCE YA 60 SENTIMITA. SHIMO HADI SHIMO, NA KUTOKA MSTARI HADI MSTARI WEKA I MITA. CHIMBA MASHIMO, KISHA WEKA HIYO MBOLEA YA SAMADI YA KUKU KWA KILA SHIMO FUKIA KIDOGO NA UDONGO, WEKA HIYO MBOLEA ANGALAU 3 WEEKS PRIOR/KABLA YA KUPANDA, NA HIZO WIKI 3 UWE UNAIMWAGIA MAJI, AU KAMA MVUA IPO ITAKUWA SAWA, ILI KUPOZA JOTO LA HIYO MBOLEA

KISHA KATIKA KUKUZIA, NAKUSHAURI USITUMIE CAN WALA UREA, TUMIA YARA MILA WINNER, AU NPK (16:16:16) AU NP YENYE NAMBA ZIFUATAZO (17:17:17). SABABU YA KUTUMIA MBOLEA KAMA HIZI, NI KUWEKA P-PHOSPHORUS AMBAYO INA KOSEKANA KATIKA MBOLEA YA KUKU, AMBAYO P- NI MUHIMU KATIKA MMEA KUWEKA MIZIZI IMARA. LAKINI KUTUMIA HIYO NPK, AU YARA MILLER WINNER ZITASAIDIA PIA KUTOA KIRUTUBISHO CHA POTASSIUM-K AMBAYO HUSAIDIA KUTENGENEZA MATUNDA, AMBAPO K- PIA KATIKA SAMADI YA KUKU IKO KIDOGO SANA

SO, PANDIA SAMADI, AFTER 3 WEEKS WEKA NPK /YARA MILLER WINNER, KISHA MAUA YAKIJA JUU PIGA BOOSTER KAMA VILE OMEX, AU WUXAL MACRO MIX, AU SUPER GRO, AU WUXAL MACRO MIX, BOOSTER HIZI HUSTIMULATE MAUA MENGI KUJA. NA UNAJUA MAUA MENGI, NDIO MATUNDA MENGI, MATUNDA MENGI NDIO MAVUNO MENGI, NA MAVUNO MENGI NDIYO PESA MINGI ETC..........


Pili, naomba contact za kampuni inayoaminika kuuza MBEGU original, kwa maeneo ya Dar.= KWA DAR HAPO NAWAAMINI, BALTON TANZANIA, WAPO KULE MWENGE KARIBU NA ITV/COCA COLA, BALTON BIDHAA ZAO NI NZURI MBALI YA KUWA NI GHALI PIA, (LAKINI KIZURI=GHARAMA), BALTON WAKO NA HUDUMA NYINGI IKIWEMO KUUZA MADAWA, PAMOJA NA MBEGU PIA. LAKINI PIA UKIWAPATA AGENT RASMI WA MAKAMPUNI MBALI MBALI KAMA WA KIBOSEED, AU SEEDCO, AU POP VRIDGE, AU AFRICASIA, MERU, ETC PIA ITAKUWA SAWA, KARIAKOO KUMEJAA UDANGANYIFU MWINGI SANA WA BIDHAAA

KILA LAHERI KIONGOZI

====================================

 


Mkuu kilimomaarifa.tajiri, mie niseme AHSANTE kwa huo muongozo wako. Well noted na nitazingatia.

In case nikahitaji kufahamu/ufafanuzi zaidi, basi naomba usinichoke.

Napanda Bamia week ijayo. Nitakupa mrejesho.

cheers kiongozi.

-Kaveli-
 
Nataman nikuone we ndugu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…