Kilimo cha vitunguu (saumu na maji): Ushauri na Masoko

Nina mzigo utatoka January kama gunia 200 ntakucheki wakati ukifika
Mkuu ulifanikiwa kutoa kitunguu January? Vipi Bei yake ilisimamaje? Nataka nianze mkulima ili nije kutoa hiyo miezi ila natamani kujua bei uwa kwa kipindi hiko zinakuwaje
 
Mkuu ulifanikiwa kutoa kitunguu January? Vipi Bei yake ilisimamaje? Nataka nianze mkulima ili nije kutoa hiyo miezi ila natamani kujua bei uwa kwa kipindi hiko zinakuwaje
Bei ya vitunguu hsifanani, msimu wa mvua bei iko juu sana na miezi kuanzia April hadi June.
Kwasasa inachezea 70 hadi 90k
 
Malila unaweza kunipa mwanga kidogo kuhusu bei za hayo maeneo ya Ruaha na hayo mengine kama unafahamu. Nataka nikasurvey na angalau kabla sijaenda huko nijue bei ya kununua kwa eka au ya kukodi kwa eka.

Kilimo Kwanza!
umeshapewa direction unataka upewe nn ,funga safari nenda
 
Mkuu unachosema kinaweza kuwa kweli mimi nikijana wa 20+ ila nimelima misimu mitatu katika Mkoa wa Dodoma nachoweza kusema Jambo lolote la kuleta mafanikio lazima ulilinde maana husda ya binadamu katika maisha yetu ni KUBWA
Nilianza kulima nikiwa na miaka 20 ufuta ekari 5 sikupata vizuri nikandondoka ila nikajaribu dengu ekari 18 nikapata magunia 48 hela msimu unaofata nikalima dengu tu ekari 30 nikapata magunia 90 but yote ilikuwa mavuno ya chini ila kujipa moyo kilimo cha mvua.... sasa niliishiwa nguvu mwaka unaofata ile nasema nayanyuka kwa nguvu nikajaribu ekari 50 za dengu hakuna kitu kilichoota kabisa pale hahaha mpaka leo sijawahi kulima tenah ila kilimo kina pesa sana me nimeiona katika umri mdogo sana na naamini nitarudi tenah now acha nitafute nguvu kwa kuendesha bolt na vibarua tofauti tofauti ila unachosema wewe ni kweli kilimo ushirikina sana sana ila ndo jamii zetu lazima ulinde mali kaka la siivyo wachawi ni wnegi na wamangati ndo wanaongoza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…