Agricultural Reseacher
Member
- Jun 7, 2022
- 14
- 22
HISTORIA YA ZAO LA MKONGE
Zao la mkonge liliingizwa nchini Tanganyika mwaka 1892 na mtaalamu wa kijerumani Dr. Richard Hindorff ambaye alikuwa ni mtafiti wa mimea na udongo.
Mtaalamu huyo alichukua miche 1000 kutoka Pwani ya Mexico kwenye jimbo la Yuctan na kuisafirisha kupitia Frolida, Marekani na Humburg Ujerumani. Kati ya miche 1000, ni miche 62 tu ndiyo iliyofika Tanganyika na ilipandwa sehemu iitwayo Kikokwe huko Pangani Tanga.
Uzalishaji wa mkonge nchini Tanzania ulianza mwishoni mwa karne ya 19 na ulisimamiwa na Kampuni ya serikali ya kikoloni ya kijerumani iliyoitwa German East Africa.
Wakati wa uhuru mwaka 1961, Tanzania ilikuwa muuzaji mkuu wa mkonge duniani na sekta hiyo iliajiri wakulima na wafanyakazi wa viwandani zaidi ya milioni 1.
Baada ya uhuru, Uzalishaji wa mkonge ulianza kupungua kutokana na kushuka kwa bei ya soko la dunia huku kukiwa na mbadala wa bidhaa zinazotokana na mkonge.
Hata ivyo mageuzi ya kiuchumi yaliyoanza miaka 1980 ambayo yalilenga katika ubinafisishaji na biashara huria.
Uhuru wa taasisi za kifedha za ndani na nje ya nchi yalifufua kilimo cha mkonge na hasa kukamilika kwa ubinafishaji mwaka 2005 uzalishaji umepanda hadi kufikia tani 40,000 mwaka 2015 hii inatokana na kuongezeka kwa mahitaji ya mkonge na bidhaa zake pamoja na kupanda bei kwenye soko la ndani na nje.
na mabadiliko ya hali ya uchumi nchini Tanzania, serikali ya Tanzania ilipitisha Sheria ya Sekta ya Mkonge, 1997; ambayo iliruhusu ubinafsishaji wa viwanda vinavyomilikiwa na serikali na kuanzisha Bodi ya Mkonge Tanzania.
Uzalishaji wa mkonge tangu wakati huo umekuwa thabiti, na kumekuwa na mafanikio mazuri katika uzalishaji.
Tanzania kwa sasa inashika nafasi ya pili kwa uzalishaji wa mkonge duniani baada ya Brazil. Katika miaka ya hivi karibuni serikali imeingiza fedha kusaidia kufufua sekta ya mkonge.
◦
Kwa nini Mkonge sasa?
Kutokana na mabadiliko makubwa ya tabia nchi kwa sasa, wakulima wamekuwa wakikosa mavuno.
Kwa sababu hii, TARI kwa kushirikiana na Bodi ya Mkonge Tanzania imeazimia kuhamasisha kilimo cha Mkonge kwa wakulima wadogo katika maeneo mbalimbali Tanzania ili zao hili litumike kuwaongezea wananchi kipato.
Umuhimu za kilimo cha zao la mkonge:-
-Mkonge ni zao ambalo halina msimu maalumu wa kupanda na linapokuwa tayari kwa kuvunwa pia linaweza kuvunwa wakati wowote bila kuathirika. Hivyo ni zao ambalo linaweza kumpatia mkulima kipato cha uhakika katika kipindi chote cha mwaka.
-Mkonge ni zao linalo stahimili magonjwa na halidhuriwi kirahisi na magugu na majanga mengine kama moto.
- Pembejeo kama mbolea, viuagugu na viuatilifu katika mazingira ya kawaida sio lazima kutumika ingawa matumizi yake yanaongeza uzalishaji na mavuno ya mapema
-Ni zao rahisi kulilima na kulitunza na halina upotevu wa mazao baada ya kuvuna (no post-harvest losses).
-Zao la Mkonge linaweza kuchanganywa na mazao mengine ya msimu kama kunde, mahindi, maharage, alizeti, njegere, karanga, n.k.
-Hii inamuwezesha mkulima mdogo kupata mazao ya chakula na biashara kwa kipindi ambacho Mkonge unakuwa bado haujakomaa.
-Hivyo, kumpatia mkulima mdogo kipato cha ziada kwa eneo moja.
-Mkonge una matumizi mengi, unaweza kutumika katika tasnia ya kilimo, nishati, ujenzi, famasia, magari, meli, majumbani, ofisini na mazingira. Hivyo ni zao ambalo kwa sasa soko lake ni la uhakika.
-Mmea wa Mkonge unaweza kuishi kwa kipindi cha miaka 10-25, hivyo kumuhakikishia mkulima kipato cha uhakika na kwa muda mrefu.
HITIMISHO
Mkonge ni moja ya mazao machache ulimwenguni yasiyo na muda maalum wa kupanda wala kuvuna linaloweza kuchanganywa na mazao mengine bila kuathiri uzalisha na au tija.
Hivyo kuwahusisha wakulima wadogo katika zao hili ni kuwahakikishia wakulima hao uhakika wa chakula na kipato cha kaya zao.
ITAENDELEA....................................
+255674086892
Karibu tukuhudumie,,,,,,,,