Kilimo cha zao la Ufuta: Masoko, Mbinu na Ushauri Toka kwa Wadau

Dada wa SUBA AGRO hakuwa tayari kunipa contact za mkulima, kasema niweke order na pesa niache kwake. Sijampa pesa bado. Maduka ya mbegu za ufuta yako Moro sehemu gani? Naweza kuja muda wowote. Wewe upo Moro? NimekuPM.
Thanks

Hapana mkuu nipo Dar. Nilijua upo Moro kuna MTU alitaka kuagiza
 
Napenda kujua na iringa wanaweza lima kwa kupiga dawa ya magugu? Maana kule hawajui wanapalilia mara mbili, au inategemea na udongo?
 
I mean kilimo kinakwendaje? Mi nakwenda vema nimefanikiwa kupanda.
 
Mkuu Poking hongera kwa kupanda? Umetumia spacing gani kati ya mstari na mstari na kati ya shimo na shimo (kwa Lindi 2002)?
 
Nimefanya spacing ya cm 30.ekari 15, nyingine 15 nilipiga dawa ya magugu napanda kesho.
 
Nimelima iringa eneo linaitwa mahenge, nimetumia mbegu ya lindi 2002,nilipiga dawa inaitwa round up.ufuta sasa una mwezi mmoja.
 
Nimefanya spacing ya cm 30.ekari 15,nyingine 15 nilipiga dawa ya magugu napanda kesho.

Ni namna gani nzuri yakuuwa magugu kwakutumia dawa. Mimi nimelima acre 13 katika bonde la Ziwa Rukwa.
 
Ni namna gani nzuri yakuuwa magugu kwakutumia dawa. Mimi nimelima acre 13 katika bonde la ziwa rukwa
Hiyo spacing ni recommendation yao au umeona ufanye hivyo, maana mimi nimetafuta sana vipimo sikupata ila nilitumia recommendation niliyopata kutoka site flani ya nje siikumbuki ambayo ni 45cm x 25cm.

Mimi nimepanda ila mvua ni mtihani huku,jua kali kama la mwezi October
 

Safi sana hakika huu mrejesho utanisaidia sana
 
Nipo Dodoma watu wamelima ila mvua zipo taratibu sana ni manyunyu sa hatujui kama yanafaa kwa kukuzia manyunyu.
 
Ni dawa ipi nzuri yakukuzia ufuta na hupigwa ufuta unafikisha muda gani?
 
Umelima wp?
Umetumia mbegu gani ?na dawa gani ya magugu?
I hope nawe umelima hili zao au umeshawahi kulima,mimi ni mara yangu ya kwanza kulima but mvua kidogo zinasumbua so sijui sana kipato kitakachopatikana au haina athari sana,but la muhimu ni dawa gani inatumika kudhibiti wadudu na magonjwa maana ninaona baadhi ya majani kwenye mmea yanakuwa na mabaka meusi kwamba ni dhahiri kuna ugonjwa so wadau naomba jibu ili haraka nikapige dawa maana ninapolima zao hili ni geni na wengi hawajui dawa zake hasa
 
Dodoma ni sehemu nzuri pia ya kulima ufuta na unastawi vizuri changamka tafuta shamba ulimi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…