Kilimo cha zao la Ufuta: Masoko, Mbinu na Ushauri Toka kwa Wadau

Kilimo cha zao la Ufuta: Masoko, Mbinu na Ushauri Toka kwa Wadau

Dada wa SUBA AGRO hakuwa tayari kunipa contact za mkulima, kasema niweke order na pesa niache kwake. Sijampa pesa bado. Maduka ya mbegu za ufuta yako Moro sehemu gani? Naweza kuja muda wowote. Wewe upo Moro? NimekuPM.
Thanks

Hapana mkuu nipo Dar. Nilijua upo Moro kuna MTU alitaka kuagiza
 
Napenda kujua na iringa wanaweza lima kwa kupiga dawa ya magugu? Maana kule hawajui wanapalilia mara mbili, au inategemea na udongo?
 
Mkuu Poking hongera kwa kupanda? Umetumia spacing gani kati ya mstari na mstari na kati ya shimo na shimo (kwa Lindi 2002)?
 
Nimefanya spacing ya cm 30.ekari 15, nyingine 15 nilipiga dawa ya magugu napanda kesho.
 
Nimelima iringa eneo linaitwa mahenge, nimetumia mbegu ya lindi 2002,nilipiga dawa inaitwa round up.ufuta sasa una mwezi mmoja.
 
Nimefanya spacing ya cm 30.ekari 15,nyingine 15 nilipiga dawa ya magugu napanda kesho.

Ni namna gani nzuri yakuuwa magugu kwakutumia dawa. Mimi nimelima acre 13 katika bonde la Ziwa Rukwa.
 
Ni namna gani nzuri yakuuwa magugu kwakutumia dawa. Mimi nimelima acre 13 katika bonde la ziwa rukwa
Hiyo spacing ni recommendation yao au umeona ufanye hivyo, maana mimi nimetafuta sana vipimo sikupata ila nilitumia recommendation niliyopata kutoka site flani ya nje siikumbuki ambayo ni 45cm x 25cm.

Mimi nimepanda ila mvua ni mtihani huku,jua kali kama la mwezi October
 
Nimeanza kuvuna ufuta shambani kwangu, kwa sasa nafanya comparison ya bei na wanunuzi. JF ni jungu kuu naombeni member wenye kujua wanunuzi mbali mbali wanipe contacts zao ile nilinganishe bei nifanye right choice ktk kuuza mzigo.
Thanks wadau wote.


Mrejesho:

  • kati ya eka 30 nilizopanda ufuta ulistawi vzuri na kuvunwa eka 17..hii ilisababishwa na uangalizi mbovu wa aliyekuwa ananisimamia shamba.
  • kila eka nilivuna wastani wa kilo 350, kipindi hiki ( july 2011-2012) wanunuzi binafsi hawakuruhusiwa lindi kununua ufuta, so niliuza kwa utaratibu wa stakabadhi ghalani @ 1200/= kwa kilo jumla nilipata kama milion 7 kwa msimu mmoja (gharama za kusafisha msitu wa eka 30, mbegu na malipo ya wafanyakazi zilikuwa ni 3.5 milion), sikuingia gharama ya kusafirisha kwa kuwa walinifata shambani.
  • Mwaka 2013 sikulima nilipumzisha shamba kwa kulisafisha eka zangu zote 50 na kutanua kidogo (hili shamba lilikuwa ni msitu wakati nalichukua)
  • mwaka huo wa 2013 ulikuwa ni mzuri sana kwa upande wa bei, chomachoma (wanunuzi binafsi) waliruhusiwa na ufuta ulipanda bei hadi kufikia 2500 kwa kilo na unalipwa cash hapo hapo. waliolima walipata pesa nzuri tu.
  • mwaka huu vijana wanamalizia kupanda shamba nimelima ekari 35, nilibadili team ya wafanyakazi wa shamba kwa kuwa wengi walinikwamisha kwa kuendekeza starehe badala ya kazi. natumaini wanunuzi binafsi wataruhusiwa.
  • watu wengi kutoka mikoa mbali mbali (wachaga kibao) wameanza kuvamia misitu na kuiuza au kulima so kwa sasa kumechangamka sana tofauti na 2011 wakati naanza.
  • expectations zangu mwaka huu ni ........35(eka) x 400(kg) x 2500(bei/kg)=35,000,000.
  • NB: 400kg kwa eka ni kiwango cha chini cha mavuno, wataalamu wa chuo cha naliendele waliniambia kwa mbegu zao za lindi 2002 na malada natakiwa nipate 1200kg kwa eka. Vijana wapo shamba wanachakarika na mi nipo mjini namtumikia mkoloni (ajira).


Thanks kwa wote:

UKITAKA KUUJUA UTAMU WA NGOMA .......UINGIE UCHEZE.

Safi sana hakika huu mrejesho utanisaidia sana
 
Nipo Dodoma watu wamelima ila mvua zipo taratibu sana ni manyunyu sa hatujui kama yanafaa kwa kukuzia manyunyu.
 
Nilifanya kilimo eneo la wilaya ya masasi mtwara . Nw changamoto kubwa ua mwaka huu ni kutokanama na kwamba watu wengi sana walilima na hii ni kutokama na bei nzuri ya mwala jana. Changamoto ni kuwepo kwa gharama nyingi za maandalizi mpaka siku ya mwisho ya kuuza unatumia pesa. Mfano unahitaji kuwa na shamba kufyeka 60,000 kwa ekari kung'os visiki 30,000 kwa eka kulima 60,000 kwa eka kupanda 15,000 kwa eka kupalilia 20,000 kwa eka upuliziaji dawa 15,000 kwa ekari dawa ya kuua wadudu, dawa ya kukuzia 20,000 kwa ekari dawa ya kuua magugu kabla ya kulima 15,000*2 kwa eka na gharama nyingine za upepetaji ufuta nk. Na mwisho ni changamoto ya bei pis inabidi kuwa mwangalifu katika kuacha nafasi kati ya shina na shina na mwisho ni bei ya kuuzia ambayo inayumba sana kutegemeana na soko.
Ni dawa ipi nzuri yakukuzia ufuta na hupigwa ufuta unafikisha muda gani?
 
Umelima wp?
Umetumia mbegu gani ?na dawa gani ya magugu?
I hope nawe umelima hili zao au umeshawahi kulima,mimi ni mara yangu ya kwanza kulima but mvua kidogo zinasumbua so sijui sana kipato kitakachopatikana au haina athari sana,but la muhimu ni dawa gani inatumika kudhibiti wadudu na magonjwa maana ninaona baadhi ya majani kwenye mmea yanakuwa na mabaka meusi kwamba ni dhahiri kuna ugonjwa so wadau naomba jibu ili haraka nikapige dawa maana ninapolima zao hili ni geni na wengi hawajui dawa zake hasa
 
Dodoma ni sehemu nzuri pia ya kulima ufuta na unastawi vizuri changamka tafuta shamba ulimi.
 
Back
Top Bottom