SoC02 Kilimo kama suluhu kwa changamoto ya ajira kwa vijana, wahitimu wa Vyuo Vikuu na Vyuo vya Kati Tanzania

Stories of Change - 2022 Competition

Sumu ya nyigu

Member
Joined
May 18, 2019
Posts
60
Reaction score
111
Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012, Zaidi ya asilimia 77 ya wakazi wa Tanzania ni vijana. Serikali ya Tanzania imezidi kupanua wigo kwa vijana kupata elimu, kwa kutoa elimu bila malipo kuanzia kidato cha kwanza hadi kidato cha sita.

Pia imewawezesha wahitimu kuendelea na elimu za juu kwa kuwakopesha fedha kupitia bodi ya mikopo kwa ajili ya kumudu gharama za masomo. Kila mwaka wahitimu Zaidi ya 100,000 kwa ngazi mbalimbali wanarejea kutoka vyuoni baada ya kuhitimisha masomo yao. Idadi hii imekuwa ikiongezeka kutokana na juhudi mbalimbali zinazofanywa na serikali katika kuhakikisha kuwa vijana wengi Zaidi wanapata fursa ya elimu.

Licha ya juhudi hizo, bado serikali imeshindwa kutengeneza mitaala yenye kuwajengea misingi bora na imara kwa vijana hao ili waweze kupambana na changamoto za ukosefu wa ajira mara baada ya kuhitimu masomo yao. Mpaka sasa asilimia kubwa ya wahitimu wa vyuo mbalimbali nchini bado wana fikra za kuajiriwa, hasa na serikali.

Kwa idadi kubwa ya wahitimu wanaozalishwa na vyuo mbalimbali nchini na kuhitimu kila mwaka idadi inayoongezeka kila mwaka, ni vigumu kuajiriwa na serikali au hata na sekta binafsi. Kuna haja ya sisi vijana kuangalia fursa mbalimbali zilizopo katika mazingira yetu hasa katika kilimo ambacho ndio uti wa mgongo kwa uchumi wa taifa letu. Pia kilimo hicho kinaweza kwenda sambamba na biashara na ufugaji hivyo kuongeza tija Zaidi.

Licha ya bei ya pembejeo kuwa juu kwa sasa, kilimo bado kina tija kubwa kama kitafanywa kwa umakini kadri ya ushauri wa wataalamu. Kwa mfano kilimo cha alizeti ni fursa kubwa sana iliyopo katika kilimo kwa sasa. Zao hili limeibuka kuwa dhahabu muhimu sana nchini. Viwanda vinahitaji zao hili kama malighafi muhimu kwa ajili ya uzalishaji wa mafuta ya kula. Pia masalia yake ni kiambata muhimu kwa ajili ya utengenezaji wa chakula cha mifugo. Kilimo hiki kinaweza kufanywa kwa mtaji mdogo wa kuanzia shilingi za kitanzania 100,000/= hadi 500,000/= tu, na baada ya mavuno mkulima anaweza kupata mpaka shilingi 1,000,000/= itakayomuwezesha kuongeza kiwango cha uzalishaji katika msimu unaofuata hivyo kupata kipato kikubwa Zaidi.

Kwa wastani hekta moja ya shamba huhitaji kilo moja na nusu hadi mbili za mbegu na mfuko mmoja wa mbolea ya kupandia wa kilogramu 50. Unaweza kutumia mbolea ya kupandia tu, au ukatumia na ya kukuzia na kuzalishia ili kupata mavuno zaidi. Pia kama una samadi ya ng’ombe hufaa Zaidi kwani inahifadhi udongo na virutubisho vyake hukaa kwenye udongo kwa muda mrefu Zaidi ikilinganishwa na mbolea za viwandani. Alizeti huhitaji wastani wa palizi mbili tu, pia unaweza kutumia kemikali kukausha magugu katikati ya mimea kadri ya ushauri wa wataalamu. Mavuno kwa hekta huweza kufikia mpaka gunia 10 za debe 10.

Nimependa kutolea mfano huu wa kilimo cha alizeti kwa zababu nina uzoefu nacho. Mbali na zao hili yapo mazao mengine mengi yenye tija, kama maharage, nyanya na parachichi licha ya changamoto zilizopo kubwa ikiwa ni ukosefu wa mitaji.

Ningependa kutoa ushauri wangu kwa serikali, mashirika binafsi na wadau mbalimbali kuwawezesha vijana wapate mitaji ya kilimo, biashara na ufugaji, iwe katika vikundi au mtu mmoja mmoja, ili waweze kupambana na changamoto ya ukosefu wa ajira na kujikwamua kimaisha. Pia kuna haja kubwa ya kuboresha mitaala ya elimu ili iendane na hali halisi iliyopo kwa sasa.

Mitaala inayotumika kwa sasa huwaandaa wahitimu kuajiriwa kwa asilimia kubwa. Serikali ina jukumu kubwa la kuwatengenezea mazingira wezeshi zaidi ikiwa ni pamoja na mitaji na masoko vijana, akina mama, na watu wenye ulemavu ili kupunguza kiwango cha utegemezi nchini. Kwa hali iliyopo sasa vijana wengi hasa wahitimu wa vyuo wanakuwa tegemezi kwa miaka hata Zaidi ya kumi baada ya kuhitimu masomo yao, kutokana na kutojengewa msisingi imara ya kujiajiri wawapo vyuoni, ikiwa ni pamoja na kuwaanda kisaikolojia na wimbi la ukosefu wa ajira.

‘‘Vijana ni taifa la kesho’’. Msemo huu hauwezi kuwa sahihi kwa vijana wanaotegemea kuajiriwa na serikali au sekta binafsi na kusubiria mshahara mwisho wa mwezi baada ya kuhitimu masomo yao. Tunahitaji vijana wawekeze nguvu kazi yao, ikiwa ni pamoja na kutumia maarifa wayapatayo vyuoni katika Nyanja mbalimbali za kiuchumi ili kuuishi msemo huu kwa maendeleo endelevu ya taifa letu yenye matokeo chanya na manufaa kwa taifa la kesho na vizazi vijavyo.

Vijana tunalalamika na ukosefu wa ajira na ugumu wa maisha. Hili halina ubishi ni ukweli unaoishi, maisha ni magumu. Ajira hakuna ila kuna fursa za ajira. Tunahitaji kuwezeshwa ili tubadili fursa kuwa ajira. Tunaiomba serikali ifanye nafasi yake nasi tutafanya nafasi yetu na malalamiko yatapungua au kukoma kabisa.
 
Upvote 4

Vijana tunalalamika na ukosefu wa ajira na ugumu wa maisha. Hili halina ubishi ni ukweli unaoishi, maisha ni magumu. Ajira hakuna ila kuna fursa za ajira. Tunahitaji kuwezeshwa ili tubadili fursa kuwa ajira. Tunaiomba serikali ifanye nafasi yake nasi tutafanya nafasi yetu na malalamiko yatapungua au kukoma

Naombeni sana kura zenu kwenye huu uzi, na mwenyezi Mungu atawabariki. Ahsanteni🙏
 
Hakika kina saidia mno...na mimi nimeandika makala kuhusu kilimo na manufaa yake kwa vijana basi nomba pia kura yako
 
Back
Top Bottom