Kabula Aaron Elias
New Member
- Dec 16, 2018
- 1
- 0
Kilimo ni uzalishaji wa mazao ya chakula na yasiyo ya chakula kwenye mashamba na ufugaji wa wanyama wanaofugwa. Lakini pia kilimo kinahusisha ufugaji wa nyuki na ufugaji wa samaki.
Aidha kilimo ni moja ya sekta kuu ya maendeleo kwa nchi na hivyo basi inatakiwa kuangaliwa na kufatiliwa kwa makini. Ili kupata matokeo chanya ni muhimu kujua mambo yanayoathiri kilimo.
Kilimo kinaathiriwa na mambo makuu yafuatayo;
Hali ya hewa; Kila kilimo kina joto lake sahihi kwa ajili ya kuzalishwa lakini hali ya hewa ya saa hivi imeathiri sana uzalishwaji wa mazao kutokana na klorofluorocarbons amazo zimechangia kuongezeka kwa joto duniani na hivyo kupunguza mvua na hivyo mazao kupungua. Hata hivyo haijaathiri mazao peke yake lakini pia ufugaji wa nyuki kwa nyuki nao hutegemea mimea kuzalisha asali mimea kama zao la alizeti na hivyo kuathiri kilimo cha nyuki na kusababisha nyuki amabo husaidia katika uchavushaji wa mimea kupotea na kupungua kwa kasi wa wadudu wa nyuki na hivyo kufanya kilimo cha ufugaji wa nyuki kua mgumu. Lakini pia huathiri mifugo kama ng'ombe, mbuzi na kondoo kwa kusababisha hali duni kwa mifugo lakini pia malisho yao kua duni na hivyo kusababisha hata kupungua kwa thamani yao katika soko .
Magonjwa; Kama inavyojulikana magonjwa ni moja ya sababu kuu katika kurudisha nyuma kilimo. kwa sehemu ya mimea hua wanashambuliwa sana na wadudu na hivyo huhitaji mbolea bandia ambayo huua wadudu hao lakini sio mazao pekee yanayoshambuliwa na wadudu na magonjwa pia hata mifugo kwa mfano ng'ombe wanaathiriwa na mafua ya ini na hivyo kusababisha thamani ya maini yao kupungua sokoni lakini hata samaki nao wanaathiriwa na magonjwa na vimelea kama minyoo na hivyo kuathiri ukuaji na idadi ya samaki. Hata hivyo nyuki nao wanaathiriwa na wadudu kama sisimizi na magonjwa yanayosababishwa na kuvu(fangasi).
Rutuba ya udongo; Katika kilimo cha mazao urutubishaji wa udongo ni muhimu sana ambapo ikiaathiriwa hupunguza uzalishwaji wa mazao. Kupungua kwa rutuba ya udongo husababishwa na vingi kama ukuaji wa viwanda inayosabisha uchafuzi wa hewa na kusababisha mvua ya tindikali na hivyo kupunguza rutua ya udongo wa mazao lakini pia utumiaji wa mara kwa mara ya dawa za kuulia wadudu mashambani husababisha uharibifu wa muundo wa udongo na hii hali hupunguza thamani na idadi ya uzalishwaji wa mazao.
Kutokana na sababu hapo juu zifuatazo ni athari chanya zitakasosaidia kilimo kwa ujumla yaan mazao, mifugo, samaki na hata nyuki.Athari hizi pia zitakuza uzalishwaji wa mazao, mifugo, samaki na hata nyuki;
Utupaji mzuri wa viwanda; Viwanda vinatakiwa kupewa sheria kali juu ya utupaji wa taka zako na kwenye mfumo wa gesi zenye sumu kila kiwanda kiwe na kichomea moto na hata hivyo uzalishwaji wa gesi zenye sumu zipunguzwe kama kuchanganya na gesi ambayo sio ya sumu na hivyo kutengeneza gesi isio na sumu hii itapunguza mvua za tindikali na urutubishaji wa udongo wa mazao itaongezeka.
Utumiaji ya mbolea ya kikaboni; Mbolea hii ni aina ya mbolea ya asili iliotengenezwa asilia na haina kemikali hivyo kuua wadudu na kupunguza magonjwa lakini pia haiharibu muundo wa udongo wa mazao. Hii mbolea hua ni ghali sana na hivyo kufanya wakulima wa mazao kushindwa kuinunua na mbadala kutumia mbolea bandia ambayo ni bei rahisi hivyo upunguzwaji wa bei wa mbolea ya kikaboni itasaidia kupunguza wadudu na magonjwa lakini pia hulinda muundo wa udongo na hivyo kusababisha ongezeko la uzalishwaji la mazao.
Ardhi ya kilimo; kutokana na ongezeko la watu na hivyo makazi yameongezeka pia na hivyo eneo la kilimo kupungua. kilimo cha aina yoyote kinahitaji ardhi iwe cha mazao, ufugaji wa mifugo na samaki na hata ufugaji nyuki inahitaji ardhi itakayofanikisha kilimo na hivyo basi ni vyema kutenga ardhi kwa ajili ya kilimo.
HITIMISHO; Mwisho kilimo ni moja ya sekta kuu itakayoleta maendeleo hasa tukifikia lengo la kusafirisha nchi zingine bidhaa zetu na hivyo hatuna budi kuongeza thamani ya mazao yetu. Lakini pia kilimo kina changamoto kama wakulima kutokua na elimu ya kutosha kuhusu kilimo kwa ufasaha bali hufanya kwa mazoea lakini pia dawa za kilimo kua na bei juu na miundombinu mibovu kama barabara na sehemu ya kuhifadhia bidhaa zitokanazo na kilimo na kusababisha athari kubwa kwa bidhaa hizi.
Name ; Kabula A Elias.
phone number; 255674986050

Upvote
0