SoC03 Kilimo mkombozi wa nchi

SoC03 Kilimo mkombozi wa nchi

Stories of Change - 2023 Competition

Vanessa Swai

New Member
Joined
Jul 5, 2023
Posts
1
Reaction score
0
Kama ningepewa nafasi kuongea na viongozi wangu wa Tanzania kuhusu sekta moja inayo hitaji uwajibikaji kati ya sekta nyingi zenye chanagamoto ningechagua kilimo. kwani haya ndio ndio natamani kuyajadili zaidi.

Tanzania ni moja ya nchi duniani zinazo sifika kwa kilimo. Mazao kama mahindi, karanga,mchele,ndizi, miwa na maharage ndo zimeipatia sifa hizi nchi hio kwani uzalishaji wake nchini Tanzania ni wa kiwango cha tofauti na nchi zingine zinazo zalisha mazao sawa.hii ni kutokana na sababu mbali mbali kama hali ya hewa na rutuba zipatikanzo arthidhini.

Pamoja na Tanzana kua na faida hii kilimo hakijawa kikisaidia kwa asilimia za juu kama ipasavyo.

Tanzania ina matatizo kadha wa kadha ambayo yanaweza kusaidiwa na kilimo.

Ukosefu wa ajira ni moja ya tatizo kuu nchini Tanzania, ni tatizo kuu kwa sababu uwepo wake huzaa matatizo mengine mengi ,kama umaskini na uwiano wa utegemezi amabapo kwa pamoja matatizo haya huzuia Tanzania kufikia kiwango chake stahili cha mafanikio.

Tanzania inaweza kuokoa janga hili kwa kuwezwsha kilimo nchini, kwa kuwezesha kilimo viongozo wa Tanzania wapaswa kukabiliana na chaangamoto za kilimo ili kilimo kipanuke na kuweza kuibeba nchi kwa asilimia kadhaa.

Kilimo cha Tanzania kinakua pungufu kwa sababu mbali mbali kama zifuatazo

Ukosefu wa elimu kwa wananchi;

Wananchi wote wa Tanzania wanapaswa kupewa elimu kuhusiana na kilimo kwani kilimo ni mgongo wa Tanzania. Kuna aina mbili za elimu wanachi wanapaswa kupewa elimu ya umuhimu wa kilimo na elimu ya kilimo bora.

Elimu ya umuhimu wa kilimo; hii ni kwa ajili ya kuelimisha wananchi faida za kilimo na kuondoa propaganda zilizo sambazwa mitaani kama kilimo sio cha wasomi,watanshati na matajiri. Elimu hii ni vema kufundisha mashuleni kwani wanafunzi ndio viongozi na taifa la baadae.elimu hii inapaswa kua tofauti na ile ya madarasani kwani hii yapaswa kua kiundani na kiualisia zaidi.

Lakini pia elimu hii yapaswa kufundishwa kwa wananchi kwenye vijiji mbali mbali kwani yapata kuwapa muonekanompya kwa sekta hii ya kilimo. Kwa elimu hii kuleta mabadiliko ya mtazamo wa kilimo kwa wanafunzi na wanchi wasio na ujuzi wa kilimo yapaswa kugaiwa na wakongwe wa kilimo walio faidika na kilimo cha mazao tofauti tofauti.ili kuwapa picha halisi kutokakwa uzoefu wao.

Elimu ya kilimo bora; elimu hii ni pana zaidi kwani inashika Nyanja mbali mbali kama makosa ya kilimo,namna ya kutatua matatizo na ushauri wa namna ya kilimo.

Kwa kuanza na makosa ya kila siku kama kama kutumia dawa na mbinu za asili kulinda mazao dhidi ya wadudu na magonjwa ya mazao badala ya kutumia dawa na mbinu za kisayansi zilizo fanyiwa uchunguzi na utafiti. hii ni kwa sababu ya watanzania wengi wanaofanya kilimo vijijini kua wenye umri mkubwa hivyo bado kuamni na kushikilia milana desturi za kale huku wakihofia mabadiliko.

Pia kosa la kutumia mbegu kwa mazoea na imani bila ya kufanya utafiti mbegu husika huota na kuchanua vizuri kabisa kwenye mazingira gani na matunzo gani. Kosa hili hutokana na wakulima kulima kwa mazoea kwani wanaamini tetesi na sio elimu na uchunguzi, huku wengine wakiamni mazoea na miaka yao mingi ya kujihusisha na kilimo.

Makosa haya hutatuliwa kwa wakulima kupewa elimu ya aina ya mazao na tabia ya mazao kwani kwakujua hayo wataweza kuelewa mbegu ipi ni nzuri zaidi kwa mkoa gani na matunzo gani. Elimu hii itasaidia wakulima wa eneo Fulani kua na aina moja ya zao lenye ubora sawa kwani limezalishwa kwa ustadi na usawa sahihi.hii husaidia zao hilokueza kusafirishwa kwa ujazo mwingi na kutoka kwa wakulima mbali mbali wa eneo moja.

Ukosefu wa teknolojia sahihi.

Tanzania ni moja ya nchi za kiafrica zenye teknolojia ya chini,hivyo kushindwa kushindana nan chi zilizo endelea kwenye uzalishaji.

Teknolojia ni pana sana kwani kwa kutatua tatizo hili tatizo la vifaa sahihi pia lina suluhishwa pamoja na kutumia kilimo cha sayansi ya mbele.

Kilimo cha sasa kinatumia teknolojia sana kwana mazao yanazalishwa kwa wingi zaidi na yanatakiwa kuwa na ubora zaidi kwani husamabazwa duniani kote.

Kilimo cha Tanzania kina matatizo mengi zaidi ya haya mawili lakini kwa kuanza na haya kilimo cha Tanzania kitapiga hatua kubwa sana na ya mbali.

Serikali kwa kushirikiana na wananchi wake inaweza kutatua majanga haya kwa mibadala tofauti,kwa mfano kuanzisha program za kuendeleza kilimo,kuomba msaada wa elimu ya kilimo kutoka kwa nchi zilizo endelea kwenye sekta hii kutuzidi lakini pia ni kusukuma wananchi kufanya tafiti mbali mbali kuhusiana na kilimo kablaya kukubali ugumu na kukata tama.

Kilimo kikizingatiwa kwa usawa na viongozi na wananchi wake ni sekta itakayo leta mabdiliko chanya zaidi kwenye uchumi wetu wa Tanzania na kuondoa changamto kama ukosefu wa ajira na umaskini lakini pia kupinguza njaa nchini.

Kilimo kama sekta nyingne mbali mbali ina changamoto zake kama hasara mara moja moja vitu kama hali ya hewa visipo enda sawa na mipango. Lakini changamoto hizi huepikika na haziliningani na faida
 
Upvote 1
Back
Top Bottom