Kilimo na Biashara: Kipi kinalipa kwa siasa za Tanzania!

Kilimo na Biashara: Kipi kinalipa kwa siasa za Tanzania!

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2016
Posts
17,434
Reaction score
27,177
Maisha ni sias and vice versa. Je, kwa kijana aliyetoka chuo na kupata uridhi wa milioni 5 kwa wazazi wake, aingize kwenye kilimo au biashara?

ROBERT:
Amehitimu UDSM kitengo cha Sheria, akaingiza milioni 5 kwenye kununua mahindi Songwe ili asafirishe Malawi, kufika mpakani kakuta hakuna kibali cha kuuza nje, gharama ya kurudisha shambani ni kubwa kuliko ya kununulia. gharama ya kuweka ghala nayo ni kubwa.
Sabau ya kuzuiliwa ni El Nino ambayo mara nyingi huja kama ghadhabu ya Mungu kwa mambo flani flani[watu wana amini hivyo].

JOHN:
John amehitimu IFM na amepata mkopo wa milioni 5 toka kwa shemeji yak aishiye Dar es salaam .Katika mkopo huo, John ameamua kufanya biashara ya duka, Kanunua kva za simu za laki moja, miwani za laki 2, Screen protector za laki 2, charger za iphone, type c, fast chager, raba za uturuki kwa jumla kachukua pair 20, mashati ya nice, juml ni pqir 50 na fremu kodi elfu 50 kwakuwa anauzia Buza kwa lulenge, pamoja na pikipiki ya umeme kumfikisha kazini.​

Je, bada ya mwaka mmoja kati ya Robert na john , nani atakuwa kafanikiwa kimaisha?
 
We acha tu yani ukiweza kushinda changamoto na ukapatia soko basi umeweza ila kila sehemu kuna changamoto zake.
Hujaona tangazo la kuzuia mahindio kuuzwa kwasababu ya El Nino? Utashindaje hapo?

Umeshawahi kuona tangazo la kuzuia screen protector au cover zisiuzwe kwakuwa watu hawana hela?
 
Hakuna hata mmoja hapo anayelima wote wanafanya biashara sema ni biashara tofauti tofauti
Kilimo kinalipa kama unamtaji mkubwa japo risk ni kubwa pha
 
Back
Top Bottom