Kilimo na Imani za kijadi au Kiutamaduni (Mila na desturi)

Kilimo na Imani za kijadi au Kiutamaduni (Mila na desturi)

superdove

New Member
Joined
Mar 3, 2019
Posts
1
Reaction score
0
Habari za mida wana JF,


Kuna baadhi ya makabila wao kwao ni mwiko wanawake kuchuma mboga, kuingia bustanini, au mashambani wanapokuwa katika Ada ya mwezi(hedhi). Wengi hudai kuwa mazao yanaharibika ama yatavamiwa na wadudu waharibifu au kunyauka kabisa na wakati mwingine kupunguza mavuno.

Huko kwenu Jambo hili linaeleweka vipi? Hali kwenu ikoje? Je Kuna ukweli wowote?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nadhani ni nature...kuna baadhi ya wanawake kama sio wote wakiingia shambani wakati wakiwa kwenye siku zao za hedhi mazao hunyauka ama mavuno kupungua. Hiyo ni indigenous knowledge ambayo inapotea sasa mingoni mwetu
 
Wazee wetu wa zamani walikuwa wanatoa mafunzo kwa njia ya mafumbo/ulinganisho wa mambo, kwa bahati mbaya vizazi visivyohoji vimeshindwa kufumbua haya mafumbo na ndio yanatuangamiza mpk leo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom