chardams
JF-Expert Member
- May 1, 2012
- 2,439
- 1,738
Mkuu unapoamua kuwa mkulima maana yake sehemu kubwa ya nguvu kazi unatoa wewe mwenyewe na usaidizi uupate pale tu unapozidiwa. Tatizo kubwa la ninyi vijana ni kufanya kazi ya kilimo kama wewe ni mwajiri vile. Kwa mfano mimi mwaka jana nililima ekari 12@ekari sh 25,000 kwa trekta jumla laki tatu. mbegu za kupandia kila ekari mifuko mitano yaani 10kg each ekari, kila mfuko elfu sita. kwa hiyo kila ekari elfu30x12= 360.000/. kupanda nilipanda mwenyewe ekari nne na ekari nane niliweka watu kila ekari elf tano =40,000/. Kupalilia kila ekari sh 12,000x12x2= 280,000/, Gharama za kuvuna na kusoma laki sita. .Mapato nilipata magunia 230 nikauza gunia 210@ sh 90,000/ nikapata 18900000. Niliacha gunia 20 ambazo nimetumia mwaka huu kuwalipa nguvu kazi na matumizi binafsi.
N.B sikuweka mbolea ya viwandani mimi shamba langu huwa naweka samadi mara moja kila baada ya miaka mitatu. Angalia mapato na matumizi majibu unayo mwenyewe.
Mkuu ni mazao gani ulilima na ulilimia wapi, mbona gharama za nguvu kazi saidizi ni nafuu?