Kilindi, Tanga: Watu watano wauawa kwenye mapigano ya Wakulima na Wafugaji

Wafugaji wasikilizwe nao wapewe mapori wanafugie huko na wapelekewe huduma za jamii za msingi kama vile shule , zahanati, hospitali, vituo vya Polisi n.k

Wafugaji wamesogea na kuishi vijijini kutafuta huduma za jamii.

Mapori ya kuchungia hakuna,

Ni kweli ni wakorofi sana na ni wababe kwa wakulima.

Halafu kwa kuwa wao wanahela ni rahisi kufanya ghiliba wanapofanya makosa.

Lakini wasikilizwe wanahoja za msingi.
 
Halafu mpuuzi mmoja atatoka huko atakwambia hii nchi imejaa watu waoga kwa kivuli cha kutunza amani. Watanzania ni wakatili lakini huwezi kujua hadi pale mtaani kwenu kibaka akikamatwa.
 
Heshima ipi aliyonayo huyo mzee na mimacho yake mikubwa? Hajawahi kuwa na heshima yoyote ni IGP wa hovyo sana aliyewahi kutokea.

He should just go to hell maana jeshi limemshinda kuongoza.
Tatizo linaanza kwa Amri jeshi MKuu yupo anasikiliza Taarabu tu.
 
Mkuu wa wilaya ya Kilindi, Abel ameongoza kamati ya ulinzi na usalama wilayani kusaka miili ya marehemu waliouawa katika mapigano ya Wakulima na Wafugaji wilayani Kilindi.

Tayari miili mitano imeshapatikana na polisi wameweka ulinzi mkali.
Wanasubiri yatokee maafa ndipo wanaweka ulinzi mkali ili iweje, where were they before? Ina maana intelligency yao inanusa vyama vya siasa tu?
 
Hizi taarifa wameziandika lakini hawaja kuzungumzia kuhusu chanzo cha mauwaji. Hawajesema kuhusu Katibu Tawala Wilaya, Afisa Mifugo Wilaya na Afisa mmoja mwingine kuwa na mgongano wa maslahi Kibirashi na hasa katika eneo la Chokaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…