Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 6,236
- 10,774
Kisa cha mtoto wa kike Cwecwe, msichana mdogo wa miaka saba, ambaye amefanyiwa ukatili wa kingono, ni kesi nyingine katika mfululizo kesi ambazo zinaendelea kutuweka roho juu wazazi na walezi. Baadhi yetu tumeanza kujitoa ufahamu kuwa ulinzi wa watoto wetu ni jukumu letu la kwanza, na jukumu la msingi zaidi.
Kisa cha Cwecwe kimeacha majeraha makubwa katika jamii yetu mpaka muda huu. Ni kisa kinachotukumbusha kwamba hata watoto wadogo kabisa, wale tunaowachukulia kama wasio na hatia, wanaweza kuwa wahanga wa ukatili wa kutisha. Hii ni changamoto inayotukabili sote kama wazazi, walezi, na jamii kwa ujumla, haswa katika kipindi hiki ambacho wengi wetu tupo busy na harakati za maisha.
Hatupaswi tena kuishi kwa dhana kwamba watoto wetu wako salama kwa sababu tu wako karibu nasi. Wahalifu wapo kila mahali, wakitafuta nafasi na fursa za kutekeleza uovu wao, wapo majumbani, mashuleni,, vituo vya mabasi na kadhalika. Hivyo, tunapaswa kuwa macho na makini zaidi.
Moja ya hatua muhimu tunazopaswa kuchukua ni kuimarisha mawasiliano na watoto wetu. Tunahitaji kuweka mazingira ambapo wanaweza kujisikia wapo huru kuzungumza nasi kuhusu chochote kinachowasumbua.
Hii inamaanisha kuwa na mazungumzo ya kila siku, ambapo tunawauliza kuhusu shule, maisha yao, na shughuli zao za kila siku haswa michezo, wapo watoto wetu ambao wana michezo ya hatari wakiwa mashuleni.
Ni muhimu kuwafundisha watoto wetu kuhusu miili yao na mipaka yao. Wanapaswa kujua kwamba wana haki ya kusema "hapana" ikiwa mtu anawafanya wahisi wasiwasi au wasio salama. Tunapaswa kuwafundisha kuhusu sehemu zao za siri na kuwafanya wajue kwamba hakuna mtu anayeruhusiwa kuzigusa bila ruhusa yao.
Tunapaswa pia kuwafundisha kuhusu watu wanaowasaidia. Wanapaswa kujua kwamba wanaweza kuwaeleza watu wazima wanaowaamini, kama vile wazazi, walimu, au polisi, ikiwa wanakabiliwa na hali yoyote ya hatari.
Kwa upana wake dhana ya ulinzi wa watoto wetu sio jukumu la wazazi pekee. Ni jukumu la jamii nzima. Tunahitaji kufanya kazi pamoja ili kujenga jamii salama ambapo watoto wanaweza kuishi pasipo kuwa na hofu.
Kisa cha Cwecwe ni kilio cha kuamsha akili na ufahamu wetu. Tunapaswa kusikia kilio hicho na kuchukua hatua. Tunapaswa kufanya kila tuwezalo ili kuwalinda watoto wetu na kuhakikisha kwamba hakuna mtoto mwingine anayepitia ukatili kama huo.
Mpaka sasa mtu ambaye anahusika na tukio la ukatili dhidhi ya Binti Cwecwe bado hajakamatwa ingawa ameshajulikana. Mungu tusaidie tupate kuvilinda vizazi vyetu kwa kweli.
JUSTICE FOR CWECWE