KERO Kilio cha Wakulima na Wafugaji: Mkwamo wa Mfuko wa Pembejeo (AGITF) na Ucheleweshaji wa Miongozo ya Mikopo

KERO Kilio cha Wakulima na Wafugaji: Mkwamo wa Mfuko wa Pembejeo (AGITF) na Ucheleweshaji wa Miongozo ya Mikopo

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Leo nataka kugusia jambo ambalo linatupa wakati mgumu sisi wadau wa kilimo na ufugaji tunaotafuta mitaji kupitia Mfuko wa Pembejeo (AGITF).

Ukiingia kwenye tovuti ya AGITF (www.agitf.go.tz) unakuta kila kitu kimepangwa vizuri sana. Kuna fomu za kupakua (download) na maelezo ya wazi kabisa yanayoelekeza kuwa mwombaji ajaze fomu, azipitishe kwa Afisa Mifugo wa Kata, kisha Wilaya, na mwisho kwa Mkurugenzi wa Halmashauri husika.

Maajabu yanayoendelea:
Tukienda kufuata taratibu hizi wilayani, tunakumbana na ukuta. Maafisa wa wilaya wanadai kuwa hawajapewa taarifa yoyote rasmi wala miongozo ya sasa kuhusiana na hiyo mikopo. Inakuwaje taasisi iweke miongozo na fomu mtandaoni lakini isitoe maelekezo ya utekelezaji kwa watendaji wa ngazi ya chini ambao ndio walengwa wa fomu hizo?

Hoja yangu:
  1. Uratibu upo wapi? Kwa nini kuwe na utofauti mkubwa kati ya kile kinachotangazwa kwenye tovuti na hali halisi ya ofisi zetu za Halmashauri?
  2. Kupoteza muda wa wananchi: Inachosha na kukatisha tamaa kutumia rasilimali kuandaa maandiko ya miradi na kujaza fomu ambazo wahusika wa kuzipokea wanadai hawazitambui.
  3. Kilio kwa AGITF: Tunaomba AGITF wasifanye kazi "mtandaoni" pekee. Hakikisheni miongozo iliyopo kwenye tovuti yenu inafika na kueleweka kwa Wakurugenzi na Maafisa wa Halmashauri zetu.
  4. Mawasiliano duni: Namba za simu za ofisi za AGITF hazipatikani kirahisi, na hivyo kukatisha tamaa wafugaji na wakulima waliopo mikoani wanaohitaji taarifa.
Sisi tuko tayari kutoa ajira na kuongeza uzalishaji, lakini urasimu huu wa mawasiliano kati ya taasisi kuu na Halmashauri unaturudisha nyuma.
 

Mkanganyiko wa Mikopo ya AGITF: Website inaonyesha fomu na taratibu, lakini Halmashauri hawajui lolote!​

Ndugu zangu wa JamiiForums,

Leo nataka kugusia jambo ambalo linatupa wakati mgumu sisi wadau wa kilimo na ufugaji tunaotafuta mitaji kupitia Mfuko wa Pembejeo (AGITF).

Ukiingia kwenye tovuti ya AGITF (www.agitf.go.tz), unakuta kila kitu kimepangwa vizuri sana. Kuna fomu za kupakua (download) na maelezo ya wazi kabisa yanayoelekeza kuwa mwombaji ajaze fomu, azipitishe kwa Afisa Mifugo wa Kata, kisha Wilaya, na mwisho kwa Mkurugenzi wa Halmashauri husika.
Maajabu yanayoendelea:Tukienda kufuata taratibu hizi wilayani, tunakumbana na ukuta. Maafisa wa wilaya wanadai kuwa hawajapewa taarifa yoyote rasmi wala miongozo ya sasa kuhusiana na hiyo mikopo. Inakuwaje taasisi iweke miongozo na fomu mtandaoni lakini isitoe maelekezo ya utekelezaji kwa watendaji wa ngazi ya chini ambao ndio walengwa wa fomu hizo?
Hoja yangu:
  1. Uratibu upo wapi? Kwa nini kuwe na utofauti mkubwa kati ya kile kinachotangazwa kwenye tovuti na hali halisi ya ofisi zetu za Halmashauri?
  2. Kupoteza muda wa wananchi: Inachosha na kukatisha tamaa kutumia rasilimali kuandaa maandiko ya miradi na kujaza fomu ambazo wahusika wa kuzipokea wanadai hawazitambui.
  3. Kilio kwa AGITF: Tunaomba AGITF wasifanye kazi "mtandaoni" pekee. Hakikisheni miongozo iliyopo kwenye tovuti yenu inafika na kueleweka kwa Wakurugenzi na Maafisa wa Halmashauri zetu.
  4. Mawasiliano duni: Namba za simu za ofisi za AGITF hazipatikani, na hivyo kukatisha tamaa wafugaji na wakulima waliopo mikoani wanaohitaji taarifa.
Sisi tuko tayari kutoa ajira na kuongeza uzalishaji, lakini urasimu huu wa mawasiliano kati ya taasisi kuu na Halmashauri unaturudisha nyuma.
 
Back
Top Bottom