KERO KILIO CHA WANANCHI: Huduma za Vyeti Mtandaoni Tandahimba Hazifanyi ipasavyo

KERO KILIO CHA WANANCHI: Huduma za Vyeti Mtandaoni Tandahimba Hazifanyi ipasavyo

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Naomba mamlaka husika zichunguze huduma za vyeti mtandaoni katika Wilaya ya Tandahimba. Niliomba cheti cha kifo tarehe 11 Juni 2026, lakini hadi leo 8 Julai 2026 sijakipata, na status ya maombi haibadiliki hadi mwombaji aende ofisini.

Pia, kuna taarifa kutoka kwa wananchi kwamba kwa sasa waombaji wengi hawapati vyeti vyao hadi wafike ofisini, licha ya kuomba kupitia mfumo wa mtandao. Ikiwa ni kweli, hali hii inafanya huduma ya mtandaoni kupoteza maana yake. Naomba suala hili lifuatiliwe na mfumo uboreshwe ili utoe huduma kwa ufanisi.
 
Back
Top Bottom