The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,186
- 4,940
Mkuu wa mkoa wa njombe Anthony Mtaka ameshirikiana na wakazi wa njombe katika maombi ya pamoja kuwaombea waliofariki katika maandamano, huku akisisitiza wazazi kuwausia vijana sambamba na kuendelea kuliombea taifa libaki na Amani.
Katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Makambako, Mtaka amewasikiliza wakazi wa njombe ambao wamewasilisha kilio chao serikalini. Miongoni mwa mambo ya msingi waliyoyawasilisha wakazi wa njombe ni Pmoja na Serikali kujitathmini upya katika utendaji wake kutokana na kuporomoka kwa haki hali inayohaatarisha amani ya nchi. Kando na mambo hayo mengine ni pamoja na Kuzitaka mamlaka za usalama kujitathmini kufuatia mkururu wa matukio ya utekaji na mauaji ya watu ambayo wakazi wa makambako wanayataja kama chanzo hasa cha mtikisiko wa amani nchini.
Mengine ni changamoto za kiutendaji katika mamlaka ya mapato tanzania TRA wakibainisha mlundikano wa kodi zisizo na msingi, pamoja na urasimu ndani ya serikali.
Benjamin Mponda, Orlaph Mhema na Marieta Sanga wamesema serikali haipaswi kupuuza mambo haya kwani ndio msingi hasa wa amani ya Taifa. M/Kiti wa wafanyibiashara Onesmo Msigala amesema kando na kujutia mambo yaliyotokea Serikali inapaswa kuruhusu miili ya vijana waliopoteza maisha irejeshwe majumbani kwao kwaajili ya kupunzishwa katika maeneo ya familia.