Kilo 1 ya Nyama ya kuku Chotara au Kienyeji Buchani ni bei gani?

Kilo 1 ya Nyama ya kuku Chotara au Kienyeji Buchani ni bei gani?

INSONSILE

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2012
Posts
1,960
Reaction score
2,945
Naomba kwa wazoefu wa mikoa ya Dar, Morogoro, Dodoma, Iringa, Mbeya mnipe uzoefu wenu.

Wafugaji wengi wa kuku wanauza kuku kwa mazoea sana, mnunuzi anakuja anamshika anamtikisa kidogo hivi anakadiria uzito alafu mnaanza kubishana bei.

Ila naona huu ni wizi wa hali ya juu. Naomba nipate uzoefu kidogo humu jukwaani, wewe msomaji wa post hii tuambie mkoa gani upo na hapo ulipo kama unajua bei ya kilo moja ya nyama ya kuku chotara au kienyeji buchani, tuambie, ni bei gani?
 
Noma sana na balaa😁wanamtikisa kuku hawana huruma wanunuzi kwakweli
 
picha ya namna wanavyomtikisa huyo kuku then wanaanza kubishana bei, ina maana kuku akitikisika vizuri bei inakuwa juu
 
wafugaji wa kuku inabidi tuwe na mjadala wa kina kuhusu beu ya kuku na mazao yake. Bei ya kilo ya nyama ya ng'ombe inazidi kupaa kila kukicha, sasa hivi dar maeneo mengi ni 12,000 bei ya chini. Bei ya kuku hupanda kidogo sana kwa kilo, tatizo liko wapi?
 
Ina tegemea na maneno...Nyama hiyo hiyo ukienda Riverside unaweza uziwa 5000 ila ukienda Sinza unauziwa 30000 halafu kule posta wanauzaga kuanzia 100$.Hizo bei namaanisha Kwa gram kama sikosei 50 Hadi 200 maana hazifikagi hata robo kg sijui kama
 
Back
Top Bottom