- Source #1
- View Source #1
Jeshi la Polisi limekamata kilo 50 za dawa za kulevya ndani ya jengo linalomilikiwa na Kanisa la Ufufuo na Uzima, linaloongozwa na Askofu Josephat Gwajima, katika operesheni ya kushitukiza iliyoendeshwa mwishoni mwa wiki.
Tukio hilo limeibua maswali mazito kuhusu uhalali na maadili ya baadhi ya viongozi wa kidini nchini, hususan kwa Gwajima ambaye kwa miaka ya hivi karibuni amejitokeza kama sauti yenye ushawishi mkubwa katika siasa na mijadala ya kijamii.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni SACP Mtatiro Kitinkwi dawa hizo zilipatikana katika moja ya vyumba vya kanisa hilo vilivyokuwa vimefungwa kwa muda mrefu. Uchunguzi wa awali unaeleza kuwa chumba hicho kilikuwa kikiendeshwa kwa siri na watu waliodaiwa kuwa wafanyakazi wa ndani wa taasisi hiyo.
“Tunachunguza kwa kina kuhusiana na uhusiano wa wahusika na uongozi wa kanisa. Hakuna mtu aliye juu ya sheria,” alisema kamanda huyo.
Tukio hili limezua taharuki miongoni mwa waumini na wananchi kwa ujumla, huku wengi wakitaka Gwajima kujitokeza na kutoa maelezo ya kina. Wapo wanaodai kuwa tukio hilo linaweza kuwa njama dhidi yake, huku wengine wakisisitiza kuwa ni ishara ya kuporomoka kwa maadili ndani ya taasisi za kiroho.
“Tunajiuliza, je, bado tunaweza kuwaamini watu wanaojiita wachungaji wakati maeneo ya ibada yanageuzwa maficho ya uhalifu?” alihoji mmoja wa wakazi wa Kinondoni. Hadi kufikia jana jioni, hakuna taarifa rasmi iliyotolewa na Askofu Gwajima wala uongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima kuhusu tukio hilo.
Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi na limeahidi kuweka wazi ukweli utakapopatikana.
Ikumbukwe Mnamo mwaka 2016 Mchungaji Gwajima aliwahi kupekuliwa na kukutwa na bastora aina ya Baretta yenye namba CAT 8802 akiwa hospital ya TMJ ambapo zoezi hilo la likifanywa chini ya aliyekuwa kamanda wa upelelezi wa kanda maalum ya Dar es Salaam SACP Costantine Massawe ikiwa ni tukio linaholusishwa na kumiliki genge la wahalifu,kujipatia fedha kwa njia isivyo halali na kukutwa na dawa za kulevya.
Mbali na Gwajima, washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni msaidizi wa askofu huyo, Yekonia Bihagaze (39), mfanyabiashara George Mnzava (43) na mkazi wa Kimara Baruti, Geoffrey Milulu (31). Aidha, inadaiwa washtakiwa hao walikuwa wakimiliki isivyo halali risasi tatu za bastola pamoja na risasi 17 za bunduki aina ya shotgun. Gwajima anadaiwa kushindwa kuhifadhi silaha katika hali ya usalama.

- Tunachokijua
- Juni 2, 2025 msajili wa jumuiya za kiraia aliandika barua ya kulifungia kanisa la Askofu Josephat Gwajima kwa madai ya kujihusisha na siasa. Askofu Gwajima pia ni mbunge wa jimbo la Kawe kupitia CCM.
Mara baada ya taarifa hiyo polisi walifika kwenye kanisa la Askofu Gwajia maarufu kama kanisa la ufufuo na uzima na kuendelea na shughuli zao za kipolisi
Madai
Ipo grafiki inayosambazwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii inayoonekan kuwa na nembo ya Millard ayo huku ikiwa na ujumbe unaosomeka “POLISI WAKUTA KILO 50 ZA DAWA ZA KULEVYA KANISA LA GWAJIMA”
Uhalisia wa taarifa hiyo
Ufuatiliaji wa JamiiCheck umebaini kuwa Mwanamtandao maarufu nchini Tanzania na Mtangazaji wa Clouds FM, Millard Ayo hajachapisha taarifa hii kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii kama ambayo utambulisho wake umetumika kwenye taarifa hiyo.
Kuanzia asubuhi ya leo, Juni 3, 2025, hadi saa 12:45 Jioni, Kurasa za Millard Ayo zilikuwa zimechapisha taarifa moja tu inayomhusu Mchungaji Gwajima ikielezea jinsi Polisi walivyoweka Ulinzi kanisani hapo. Rejea hapa
Katika kuchunguza zaidi, JamiiCheck imejiridhisha kuwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, SACP Mtatiro Kitinkwi hajazungumza hadharani juu ya uwepo wa taarifa hizo.
Asubuhi, Juni 3, 2025, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Muliro Jumanne Muliro alizungumza na vyombo vya Habari ambapo pamoja na mambo alitoa taarifa ya kukamatwa kwa baadhi ya waumini wa kanisa hilo, lakini hakuzungumzia chochote juu ya kukamatwa kwa dawa hizo za kulevya.
Taarifa iliyowasilishwa na mdau inaeleza kuwa "Jeshi la Polisi limekamata kilo 50 za dawa za kulevya ndani ya jengo linalomilikiwa na Kanisa la Ufufuo na Uzima, linaloongozwa na Askofu Josephat Gwajima, katika operesheni ya kushitukiza iliyoendeshwa mwishoni mwa wiki".
Sehemu hiyo ya taarifa unaonesha upotoshaji kwani polisi walienda kanisani hapo Juni 3, 2025 siku ya jumatatu ambayo ni mwanzoni mwa wiki na hakuna taarifa ya wazi kuonesha kuwa polisi walifika polisi hapo mwishoni mwa wiki licha ya kushindwa pia kueleza ni mwishoni mwa wiki ya tarehe na mwezi upi?.