Kilometa za Magari yanayouzwa bongo zina uhalali?

Kilometa za Magari yanayouzwa bongo zina uhalali?

byakunu

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2016
Posts
583
Reaction score
1,318
Wanajamvi habari zenu...

Nina jambo linanipa ukakasi kidogo, kuhusu haya magari yanayo uzwa na wabongo wenzetu kwenye page mbali mbali kama insta na kwingineko, ukakasi huo upo hasa kwenye uhalali wa Mileage ya gari husika au kilometa za gari linalouzwa. Japo kuna ukakasi mwingi zaidi ya mileage...

Ipo hivi gari nyingi za SUV mfano Subaru Forester, Harrier, Vanguard, Landcruiser, Dualis, na zinginezo. Gari hizi ukiziangalia kwenye mtandano Befoward. SBT, na page zingine za Japan kwa gari za bei affordable unakuta nyingi gari hizo zina kilometa nyingi kuanzia 110,000 nakuendelea. Zenye mileage ndogo lazima utakuta bei yake imesimama sana na kupelekea kushindwa kuinunua kutoka Japan

Ukija kutafuta au kuangalia hizi za Bongo watu wanaagiza huko Japan, wanatumia then wanaziuza kwa sababu zao mbali mbali kupitia madalali wa page za insta,zoom na kupatana, sasa hizi gari cha kushangaza zina kuwa na low mileage kupita uhalisia, mfano unakuta ina 75,000 kms, na bei anayo kuuzia ni ya kawaida tu, na gari namba ya plate sio ya muda mrefu sana, yaani namba D...,

Hapa nina wasiwasi saana kuwa hizi gari zinashushwa kilometa kwahyo tunapigwa sana,nimeweka mifano kwa picha, tusaidiane mawazo
IMG_7151.jpg

IMG_7150.jpg

IMG_7149.jpg
 
Ndugu yangu ata Japan wenyewe kuna baadhi ya makampuni yana tabia ya kubadilisha - yaani kupungua kiasi cha KMs ambazo gari imeshatembea. Iliwahi kunipata nilibaki kuwawakia kwenye simu. Bongo nadhani inaweza kuwa zaidi .

Ni fraud mbaya sana hizi kufanyika kwa level ya kampuni. Nakumbuka kuna jamaa yangu alininua IST Befoward akijua ni low mileage kumbe ducuments za inspection zimeonesha paper mileage ni kms 106,000 ila kwenye odometer gari ina soma 6,000kms na gear lever imechakaa kinoma , kapeti ya miguu karibu na accelerator pedal imelika kwa kisigino[emoji23]
 
Wanajamvi habari zenu...

Nina jambo linanipa ukakasi kidogo, kuhusu haya magari yanayo uzwa na wabongo wenzetu kwenye page mbali mbali kama insta na kwingineko, ukakasi huo upo hasa kwenye uhalali wa Mileage ya gari husika au kilometa za gari linalouzwa. Japo kuna ukakasi mwingi zaidi ya mileage...

Ipo hivi gari nyingi za SUV mfano Subaru Forester, Harrier, Vanguard, Landcruiser, Dualis, na zinginezo. Gari hizi ukiziangalia kwenye mtandano Befoward. SBT, na page zingine za Japan kwa gari za bei affordable unakuta nyingi gari hizo zina kilometa nyingi kuanzia 110,000 nakuendelea. Zenye mileage ndogo lazima utakuta bei yake imesimama sana na kupelekea kushindwa kuinunua kutoka Japan

Ukija kutafuta au kuangalia hizi za Bongo [emoji23] watu wanaagiza huko Japan, wanatumia then wanaziuza kwa sababu zao mbali mbali kupitia madalali wa page za insta,zoom na kupatana, sasa hizi gari cha kushangaza zina kuwa na low mileage kupita uhalisia, mfano unakuta ina 75,000 kms, na bei anayo kuuzia ni ya kawaida tu, na gari namba ya plate sio ya muda mrefu sana, yaani namba D...,

Hapa nina wasiwasi saana kuwa hizi gari zinashushwa kilometa kwahyo tunapigwa sana,nimeweka mifano kwa picha, tusaidiane mawazo
View attachment 1800662
View attachment 1800663
View attachment 1800664
hapana!! wachina wana vibox vipo vingi tu kwa sasa hapa Tanzania! ukitaka ata kuifanya gari iliyotumika japan kisha Dubai isome KM 2000 au 200. una click Maus ya Computer yako😁😁
 
Kwa tanzania hii ukinunua gari kwa kuangalia km ilizotembea au plate namba mfano D, utakuwa umepigwa kidole..

Watanzania wanacheza na mileage za gari na kuzishusha...

Unaweza kukuta gari uhalisia wake ni Km 180000 lakini wahuni wanachokonoa na kushusha moaka km 40000....
Boya akijichanganya anapigwa, anaenda kushangaa mbona gari lake halina performance nzuri kama magari mengine..

Kumbe kauziwa mkweche
 
Niliiona TOYOTA ALPHARD HYBRID, usajili DTV, Eti imetembea kilometa 42000, nikatabasamu moyoni tu, arif eti inauzwa milioni 14(maongezi yapo) [emoji23]
Nina mwenzangu alinunua IST namba C kwa mtu eti in KM 40000....Ngoja sasa iwashwe injini invyolia kama trekta...mvua ikinyesha ile gari ilikuwa inavuja sana maji yanajikusanya kwenye kale kasehemu ka kuhifadhia spea tairi..

Siku moja tukaikagua injini...ile gari ilikuwa imegongwa mbele ikanyooshwa...
.Ilikuwa inamoa mawazo..
 
[emoji23] [emoji1787]
 
[emoji849][emoji849][emoji849]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama mfuko ukiwa njema sioni sababu ya kununua gari za showroom au mkononi mwa mtu wanazifanyia michezo mingi ni kheri mara elfu nijikamue nichukue iliyotumika nje
 
Nina mwenzangu alinunua IST namba C kwa mtu eti in KM 40000....Ngoja sasa iwashwe injini invyolia kama trekta...mvua ikinyesha ile gari ilikuwa inavuja sana maji yanajikusanya kwenye kale kasehemu ka kuhifadhia spea tairi..

Siku moja tukaikagua injini...ile gari ilikuwa imegongwa mbele ikanyooshwa...
.Ilikuwa inamoa mawazo..

Aaah jamaa walimpiga vibaya sana.. hizi gari zilizotembea bongo ni nuksi sana unakuta zimeshapita kwa watu kama 7 na bado wale wa kukata masega hawajafanya yao
 
Nimekuja na uzi mwingine, ukiona mtu kapost chassis namba ya gari na ile gari kaiagizia Befoward.. ichukue ile chassis number kama ilivyo igoogle, ilegari itakuja kama ilivokua listed na Befoward wakati inauzwa ikague zile picha nenda mpaka kwenye picha inayoonesha odometer reading utacheka ufe.. nakupa mfano gari hii apa chini naipost.. na nnaenda kuitafuta befoward ilivokua listed. Jaman tuache ukitonga na uvivu wa kutafta maarifa mapya, haya magari tuyaagize wenyewe tu hakuna mateso yoyote unayoweza kuya pata kwa kusubiri meli ifike mwezi mmoja mpaka miwili.
IMG_0167.jpg

Gari inauzwa na dalali wa kibongo anaandika uongo uongo. Ukiichukua hiyo chassis namba ukaweka google ngoma zinakuja kama hivi chini[emoji116][emoji116][emoji116][emoji116] cheki mileage halisi ya gari, jamaa kaamua kuficha hiyo laki kasema gari ina 51000km[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
IMG_0168.jpg

IMG_0169.jpg

IMG_0170.jpg

IMG_0171.jpg
 
Back
Top Bottom