Mi nadhani maadam ni biashara yake na amewekeza.mwacheni muda utafika atatamani kuwapata wabongo wakati huo
watakuwa wamemtenga ndipo atalia kilio cha mbwa koko.
Hoteli zote zinaitwa kwa kiingereza '' hospitality industries'', nakumbuka miaka ya 90's enzi za sheraton Dar es salaam
ukiajiliwa lazima upige week mbili za training inayohusu mambo ya costumer care,na tuliambiwa usibague mtu yeyote
kwa muonekano wake,japo kulikuwa na maeneo kama vyumba ''suites'' ambavyo kama una hela fupi wewe mwenyewe utajibagua.Enzi hizo tulifanya biashara sana na watu wa nje walikuwa wengi kuliko waswahili,ila hakuna mswahili hata mmoja alibaguliwa kwa rangi yake.