kiboboso
JF-Expert Member
- Sep 17, 2013
- 9,323
- 12,594
Nani kakuambia inachosha... ni vile tu kuna mazezeta mavivu kusoma uzi mrefu.Usijali itaendelea bila shaka ni stori ndefu kidogo ukiiweka kwa wakati mmoja inaweza kuchosha msoji
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nani kakuambia inachosha... ni vile tu kuna mazezeta mavivu kusoma uzi mrefu.Usijali itaendelea bila shaka ni stori ndefu kidogo ukiiweka kwa wakati mmoja inaweza kuchosha msoji
[emoji847]Hakuna chochote kinacho tuzuzuaga zaidi ya ujinga na ulimbukeni na hua tunakuja kukumbuka familia pale mrija wa ile pesa unavyo kuja kukata, tupo kama mi mbuzi sometimes, tena ni kipindi ambacho hua hatuhitaji kabisa ushauri[emoji848][emoji41]View attachment 2422111
Umefuraaahi, mwenyewe![emoji16]
So sad........ Inaendelea
Baada ya kuambiwa niondoke nilienda kwa mwenyekiti wa mtaa kushtaki kuwa nafukuzwa na mke wangu na nikamweleza kila kitu kama nilivyoeleza sehemu iliyopita. Mwalimu akaitwa akaulizwa kwa nini anafanya vile akasema kwa sababu ni kwake na mimi nilikaribishwa tu pale kama mchepuko. Mwenyekiti nilimweleza mpaka nilivyokuwa namwachia pesa zote ninazozipata kazini, niliulizwa kama nina ushahidi wowote nikawa sina, yule mwanamke akashinda nikaondoka.
Baada ya kuondoka pale nikawa sina pa kwenda ndugu zangu wamenitenga na marafiki pia nikawa mtu wa kuhangaika. Ndipo nikapata wazo la kumtafuta mke wangu sikujua ameenda wapi. Baadae nikaambiwa alienda Bariadi nyumbani kwa wazazi wake, kwa kuwa nilikuwa napajua nikaenda mpaka ukweni sina mbele wala nyuma. Baba mkwe aliponiona hakutaka hata salamu yangu, nilipomsalimia kabla hajajibu aliniuliza nimefata nini? Nikamwambia nimemfata mke wangu. Nikajibiwa hapa mke hayupo ameolewa na sijui ameolewa wapi, alishindwa kukaa nasi sababu ya ugumu wa maisha na kutunza watoto ilikuwa kazi ngumu kwake na sisi ni wazee hatuwezi kumsaidia kwa chochote hivyo aliamua kuolewa kupunguza ugumu wa maisha. Na watoto wako anao wanalelewa na baba wa kambo. Nilisikitika sana hasa nikikumbuka wanangu sijawatunza inavyotakiwa na uwezo huo nilikuwa nao. Leo nimeenda nikiwa mikono mitupu watanielewa kweli? Niajipiga konde moyo nikasema liwalo na liwe naenda kumtafuta mke wangu huko alikoolewa angalau niwachukue wanangu hata kama yeye nikimwacha itakuwa sawa.
Nikaanza kumtafuta bahati nzuri nilimpata nikaonana nae. Kwanza nilianza kwenda kwa siri mumewe akiwa hayupo ndiyo naenda baadae ilibidi mumewe ajue kuwa mimi ndio baba wa watoto, na alipojua hakuwa na shida yoyote aliniambia hawa wanao mimi sina shida unaweza kuwachukua au kuwaacha wakae na mama yao. Nikajisemea moyoni nikiwachukua nitawapeleka wapi sina pa kuishi naishi kama mkimbizi popote kambi, wakati mwingine naenda stendi najifanya nasafiri nalala pale asubuhi naondoka kuzurula. Niliamua kuwaacha wakae na mama yao nikawaambia naenda nyumbani nikirudi nitawachukua. Walifurahi kumuona baba yao ambao ni kama miaka mitatu nilikuwa sijawaona.
Niliondoka lakini nikiwa sina furaha moyoni, nilirudi nyumbani nikaanza maisha ya kubangaiza. Nikawa fundi baiskeli kuziba pancha na matengenezo mengine ya baiskeli. Nikasahau kuhusu watoto nikaanza maisha upya na nikasema sitaki kuwa na mwanamke tena.
Ikapita miaka kadhaa nikasikia jamaa aliyekuwa amemuoa mke wangu amefariki, nikamfata mke wangu na kumwambia kama hatojali anisamehe turudiane maisha yaendelee ili tuweze kulea watoto wetu pamoja. Kwa shingo upande mke alinielewa ila akasema kwa sababu ya watoto amekubali vinginevyo asingekubali. Maisha yakaanza tena upya kwa kweli safari hii nilimpenda japo sikuwa na kipato cha kutosha. Ufundi baiskeli ulinipa pesa ya kula tu nayo siyo ya uhakika lakini maisha yalikuwa ya furaha.
Mke wangu alipata ujauzito, hiyo ilimsumbua sana maana homa ya hapa na pale zilikuwa hazikatiki. Tulihangaika hivyo hivyo mpaka akajifungua. Alipojifungua akagundulika ana VVU. Nilijiuliza sana UKIMWI umetokea wapi nani kauleta ni mimi au mke wangu? Kumbe yule jamaa aliyemuoa alikuwa HIV+ na ndiye aliyemwambukiza hayo yote alikuwa anayajua lakini hakuniambia chochote. Sijui virusi vilikuwa na nguvu gani alikonda ghafla mpaka nywele zikawa nyepesi sana. Nikaambiwa nami nikapime ili nijue hali yangu nikaenda, sikuamini macho na masikio yangu kuona na kuambiwa kuwa nina HIV+. Nilimlaumu mke wangu lakini naye akanilaumu mimi ndiyo chanzo kama nisingemwacha asingehangaika namna ile. Aliamua kuolewa kwa sababu aliamini siwezi kumrudia tena kutokana na jinsi nilivyokuwa namtolea maneno makali tukionana. Wakati anaolewa hakujua kama huyo jamaa ni mwathirika mpaka alipougua sana na kwenda kupima.
Baada ya miezi 11 tangu ajifungue mke wangu alifariki akaniachia mtoto mdogo wa miezi 11. Nilishindwa kumlea peke yangu maana watoto wangu wawili wote walikuwa wa kike waliolewa wakiwa na umri mdogo labda sababu ya shida za nyumbani walichoka wakaona bora waolewe. Mwanangu mdogo ni wa kiume nilishindwa kukaa nae nikampeleka kwa ndugu yangu ambayo ni kaka akakae na watoto wengine wa kaka.
Kwa sasa nipo natumia dozi ya HIV na maisha bado ni magumu sana.
Najuta kwa niliyoyafanya kwa sababu nisingefanya ujinga familia yangu ingekuwa inaishi maisha mazuri hata pesa nilizopata zingetumiwa na familia yangu zikaisha zote bado furaha ya mke na watoto wangu isingepotea.
Nawaomba wanaume wenzangu ukipata pesa usimsahahu mke wako aliyekuzalia watoto na kudanganywa na vimada ambavyo kazi yao ni pesa kwanza. Ukimaliza pesa wanakufukuza.
Najuta Najuta Najuta