Kevin85ify
JF-Expert Member
- Apr 6, 2019
- 2,684
- 3,429
Wacha kutoka kwa mada ulisema kibaha itakuwa barabara pana kabisa africa mashariki, ilhali itakuwa ndogo kwa Thika road ambayo ilijengwa 2010.Hii inaitwa super highway kwanini mmebadilisha iwe parking ya magari.?
NB: Hiyo msonagamano ni kwa sababu watu wamenunua magari mengi vile Uchumi wa Kenya unazidi kuimarika. sio thika road pekee hata Mombasa road, ngong road ambazo ni 6 lane highways ziko hivo masaa ya asubuhi na jioni. Hii ndiyo sababu serikali inakarabati reli ya nairobi na kununua treni 11 kutoka spain kuzuia watu kuja na magari yao mpaka CBD. Treni hizi zinatasafirisha abiria milioni tatu kila mwezi Nairobi. Pia ndiyo sababu ya serikali kujenga southern, eastern, northern na western bypass ambazo ni dual carriage highways ( 100 km) za kuzunguka nairobi. Pia inajenga waiyaki way upya kufika mpaka rironi kuwa 6 lane highway, na pia Nairobi expressway(dual carriage elevated highway) ambayo itapaa juu ya mombasa road ,waiyaki way na james gichuru.