Kimataifa: Yanga wachezaji 12 waitwa Afcon, Simba 6 tu

Iyo ndiyo tofauti kati ya quality na lundo la wachezaji, hapo makocha wa timu tofauti wamepembua pumba na mchele wakatoka na jibu Moja ambalo ni UBORA!
 
Yanga wako 15 bro.
 
Ni heri Simba wameitwa wachache maana timu za taifa zinasababisha sana majeraha kwa wachezaji. Kapombe alipotea kwa muda mrefu baada ya kuumia akiwa Stars, na Manula hadi leo anapambana kurudi baada ya kuumia akiwa na Stars. Inonga pia aliumia akiwa DR Congo. Kunawatu watarudi na pancha kibao
 
[emoji32][emoji32]
 
Mimi nashukuru sana Simba kuitwa wachache timu za Taifa. Mwaka jana tulikuwa na mechi mbaya dhidi ya Wydad Casablanca, wakati huo wachezaji wametawanyika kwenye mataifa yao mbalimbali kutumikia timu zao. Yaani ilibidi wawe wanaunganisha juu kwa juu wakaungane na wenzao ili kukutana Morocco. Kwa miundombinu ya Afrika, mchezaji akisafiri kuitumikia timu yake ya Taifa inabidi uwe unaombea mechi ya klabu yako inayofuata isiwe dhidi ya timu ngumu, au isiwe na umuhimu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…