Kimbuga jobo hukujipanga na sidhani kama shughuli zako utazifanya vyema hapo Tz.

Kimbuga jobo hukujipanga na sidhani kama shughuli zako utazifanya vyema hapo Tz.

Watanzania tunamcheki tu kama tulivyo mcheki corona. taratiiibu atapita zake
 
Ndugu yangu jobo kwanza salamu!

Pili napenda kukupa pole hasa kwa kuchagua siku isiyo rafiki kwa kufanya shughuli zako hapo Tanzania.

...aliyekudanganya uje kufanya shughuli zako siku ya Jumapili hakukujuza kwamba Tanzania kuna manabii na mitume wasiyo na idadi na kwalo siku hiyo ndiyo wao huitegemea?!

...yaani Gwaji & Co wasipige $ kisa wewe eti ili ufanye shughuli zako?!

Pole sana ndugu yangu jobo na mlaumu sana aliyekushauli eti shughulizo ukizifanya J'pili Tanzania zitafanikiwa.

Ulipaswa uwasiliane na mpwa wako Corona kwanza yule angalau angekupa picha halisi ya mitume na manabii wa Tz kabla ya wewe kutaka kuja kichwa-kichwa.

Kwa ninavyo wajua wa bongo usitarajie mteremko.Jipange.

Staki nikukatishe tamaa wewe kuja njoo lakini sidhani kama utafanikiwa kufanya shughuli zako kwa utulivu hapo Tz.

Kazi njema Jobo.
Asante hayati rais Magufuli kwa kutuachia wosia wa kuacha hofu na kumtegemea Mungu kwa kila jambo.

Kimbunga Jobo na Corona wamekiona cha mtema kuni Tanzania.
 
24 April 2021
Dar es Salaam, Tanzania

KIMBUNGA JOBO Chafanyiwa DUA NZITO, SHEIKH KISHKI



Sheikh azungumza - "HAKIWEZI KUZUIA MASHINDANO" KUELEKEA Kilele cha mashindano ya kitaifa ya kuhifadhi 'QURAAN' , muandaaji wa shindano hilo, Sheikh Kishki akiwa pamoja na washiriki wote, wamezungumza na wanahabari na kuelezea namna walivyojiandaa..
Source : Global TV online
 
23 Apr 2021
Utabiri wa Hali ya Hewa wa saa 24 zijazo kuanzia saa 3 usiku wa leo tarehe 23/04/2021 unaowasilishwa na mchambuzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania. Tarehe 25 April 2021 kimbunga kitafika rasmi pwani ya Mashariki ya Tanzania kikifuatana na upepo mkali, mawimbi makubwa na mvua hivyo wananchi wameombwa kuchukua tahadhari na kufuatilia matangazo za Mamlaka hiyo ktk tarehe zote hizo mbili.


Source : meteo Tanzania
 
Kunakijiwe nimepita nikakuta jama mmoja Ni chadema anaongelea hiki kimbunga

Aisee chadema Kuna vilaza si utani

Hv watu mkilala na kuamka mnawazaga siasa tu, hata kwenye mambo ambayo siyo ya msingi😂😂😂😂
 
we jamaa ulinisababishia ban ya wiki tatu kwa thread zako za kipimbi kama hizi....
 
Mungu wetu atunusuru!!!Tunahitaji rehema zake tu kwa sasa maana bila yeye peke yetu hatuwezi!!
 
24 Apr 2021
Mombasa, Kenya

Mamlaka ya Bandari Kenya KPA yatoa tahadhari kwa wenye vyombo baharini


KPA yatoa tahadhari ya hali mbaya ya anga na upepo mkali pwani Hii ni kutokana na kimbunga kutarajiwa kutua pwani ya Tanzania kesho KPA imewatahadharisha wanaotumia bandari kuwa waangalifu siku tatu Meli zimetakiwa kuimarisha udhibiti wa meli zilizotia nanga Wananchi wametahadharishwa dhidi ya upepo mkali na mafuriko
Source : Kenya CitizenTV
 
24 April 2021

UTABIRI WA HALI YA HEWA 24-04-2021​


Utabiri wa hali ya hewa wa saa 24 zijazo kuanzia saa 3:00 usiku wa leo 24/04/2021 umeletwa na mchambuzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.

Source : Meteo Tanzania
 
24 April 2021
Zanzibar

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Yatoa Tamko La Tahadhari Juu ya Kimbunga JoBo

Watu waambiwa Hameni, vyombo vya majini vyapigwa marufuku kungoa nanga, mikusanyiko...

Source : millard ayo
 
Back
Top Bottom