Kimbuga jobo hukujipanga na sidhani kama shughuli zako utazifanya vyema hapo Tz.

Watanzania tunamcheki tu kama tulivyo mcheki corona. taratiiibu atapita zake
 
Asante hayati rais Magufuli kwa kutuachia wosia wa kuacha hofu na kumtegemea Mungu kwa kila jambo.

Kimbunga Jobo na Corona wamekiona cha mtema kuni Tanzania.
 
24 April 2021
Dar es Salaam, Tanzania

KIMBUNGA JOBO Chafanyiwa DUA NZITO, SHEIKH KISHKI


Sheikh azungumza - "HAKIWEZI KUZUIA MASHINDANO" KUELEKEA Kilele cha mashindano ya kitaifa ya kuhifadhi 'QURAAN' , muandaaji wa shindano hilo, Sheikh Kishki akiwa pamoja na washiriki wote, wamezungumza na wanahabari na kuelezea namna walivyojiandaa..
Source : Global TV online
 
23 Apr 2021
Utabiri wa Hali ya Hewa wa saa 24 zijazo kuanzia saa 3 usiku wa leo tarehe 23/04/2021 unaowasilishwa na mchambuzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania. Tarehe 25 April 2021 kimbunga kitafika rasmi pwani ya Mashariki ya Tanzania kikifuatana na upepo mkali, mawimbi makubwa na mvua hivyo wananchi wameombwa kuchukua tahadhari na kufuatilia matangazo za Mamlaka hiyo ktk tarehe zote hizo mbili.

Source : meteo Tanzania
 
Kunakijiwe nimepita nikakuta jama mmoja Ni chadema anaongelea hiki kimbunga

Aisee chadema Kuna vilaza si utani

Hv watu mkilala na kuamka mnawazaga siasa tu, hata kwenye mambo ambayo siyo ya msingi😂😂😂😂
 
we jamaa ulinisababishia ban ya wiki tatu kwa thread zako za kipimbi kama hizi....
 
Mungu wetu atunusuru!!!Tunahitaji rehema zake tu kwa sasa maana bila yeye peke yetu hatuwezi!!
 
24 Apr 2021
Mombasa, Kenya

Mamlaka ya Bandari Kenya KPA yatoa tahadhari kwa wenye vyombo baharini

KPA yatoa tahadhari ya hali mbaya ya anga na upepo mkali pwani Hii ni kutokana na kimbunga kutarajiwa kutua pwani ya Tanzania kesho KPA imewatahadharisha wanaotumia bandari kuwa waangalifu siku tatu Meli zimetakiwa kuimarisha udhibiti wa meli zilizotia nanga Wananchi wametahadharishwa dhidi ya upepo mkali na mafuriko
Source : Kenya CitizenTV
 
24 April 2021

UTABIRI WA HALI YA HEWA 24-04-2021​

Utabiri wa hali ya hewa wa saa 24 zijazo kuanzia saa 3:00 usiku wa leo 24/04/2021 umeletwa na mchambuzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.

Source : Meteo Tanzania
 
24 April 2021
Zanzibar

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Yatoa Tamko La Tahadhari Juu ya Kimbunga JoBo

Watu waambiwa Hameni, vyombo vya majini vyapigwa marufuku kungoa nanga, mikusanyiko...
Source : millard ayo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…