Kimenuka: Kamati ya maadili ya TFF yakutana kumjadili Makamu wa Rais Michael Wambura

Kimenuka: Kamati ya maadili ya TFF yakutana kumjadili Makamu wa Rais Michael Wambura

Sibonike

JF-Expert Member
Joined
Dec 23, 2010
Posts
17,296
Reaction score
18,027
Kamati ya maadili ya TFF inakutana leo Machi 14, 2018 pamoja na mambo mengine itajadili suala la Makamu wa Rais wa TFF Michael Wambura aliyefikishwa kwenye kamati kwa makosa matatu.

Kosa la kwanza ni kupokea fedha za TFF isivyo halali.

Pili kugushi barua

Pamoja na kushusha hadhi ya TFF

TFF.jpeg
 
Amefikishwa kwenye Kamati ya Maadili kuhusiana na makosa matatu. Kupokea fedha za TFF malipo yasiyo halali, kugushi barua na kushusha hadhi ya TFF.
Kwa kweli tabia haina dawa. It was only a question of time.
Evidence?.....
 
Michael wambur duuh! Yaani nilikuwa najua kabisa huyu jamaa anagombea sana kurudi TFF kwa ajiri ya kupiga pesa tu,hakuna kingine kilichokua kinampeleka pale.yaani ameshindwa kabisa kusoma alama za nyakati? Kweli mlamba asali ahachi.alishapajua kuna pesa za mchezo.
 
Huyu yuko kama alivyokuwa Rage, hawezi kuishi maisha nje ya siasa za mpira.
 
Kwa mtindo huu watafungwa wengi,bado kuna watu wanaogombea nyadhifa wakiendelea kukariri kuwa ukishakuwa kiongozi lazima utoboe kwa kupiga madili na kusahau kuwa awamu hii ni ya 'hapa kazi tu'..
 
Kabisa,maana alivyopambana kurudi pale TFF mpaka nilikua namshangaa,alishawai kuipeleka simba kwenye mashindano ya kimataifa wakati nafasi haikua yao.na alipokuja kugombea uongozi simba,akawaambia simba nipeni nafasi,mnakumbuka niliwapeleka kwenye mashindano ya kimataifa kwa upendeleo,hafai kabisa akilo yote kwenye kupiga pesa tu.
 
Wacha wanyoshwe,SOKA ya tanzania imepoteza ladha kwa ajiri ya wajinga wachache.ukimpa mpira danadana kupiga hawezi,ila kupiga pesa mafundi kweli kweli.
 
Back
Top Bottom